Inanisikitisha sana

BRO LEE

JF-Expert Member
Dec 25, 2011
826
600
Kuna jambo ambalo huwa linanisikitisha sana ninapohudhuria baadhi ya misiba, jambo hilo hunifanya hata nitokwe na machozi hata kama wahusika wa msiba si wa2 wa karibu. Jambo hilo nimekutana nalo tena leo hii si msibani bali katika dadadala.

Kuna mama m1 alikuwa analia kuwa kwikwi na kwa uchungu mkubwa, ikabidi abiria wa karibu amwulize kulikoni, ndipo alipofunguka kwamba amepewa taarifa kwamba mumewe amefariki!, ikabidi abiria waanze kumpa pole na kutupa lawama kwa aliye mtaarifu kwa njia ya simu. Mama huyu alipokuwa anafarijiwa ndipo alipoaanza kulia zaidi na kusema mumewe kamwachia watoto wa4 na wa kwanza yupo darasa la nne atawatunza vipi.

Suala la wanawake wanapofiwa kulia kwa uchungu kwa kuwaza mzigo wa familia ulioachwa na marehemu ndo huniumiza, mara nyingine utamsikia mama anasema kwanini umeniachia huu mzigo, bora ningetangulia mm, nilikwambia tufanye... ukabisha sasa watoto nitawapeleka wapi n.k.

Napenda kufahamu kutoka kwako je mazingira haya ya kuliliwa ukifa kwa minajili ya matatizo utakayoacha nyuma unayaona/kumlilia marehemu mumeo kwa mzigo wa familia anayoacha unayaona? Kwa wewe ambaye mme akiondoka duniani leo bado utakuwa hutatetereki kwa maswala ya kiuchumi unashauri nini?

Nini kifanyike katika familia ili mmoja anapotangulia mbele ya haki anayebaki amkose/am-miss kwa yale mambo ambayo ni passion zaidi? mf. mke alie akisema mme wangu umeondoka tabasamu lako nitalipata wapi, upole wako nitaupata wapi? n.k
 
Mambo mengine sio rahisi kuyasema kwa sauti; lkn nina uhakika kila anavyokuwa mwenyewe analia kwa ajili ya hayo na mengine tusoyajua!
 
inabidi kama ni mwanaume na mkeo ni mama wa nyumbani,tafuta ka shughuli/kibanda.... ka kumzoeza mkeo kuwa na financial freedom hii itamjengea kujiamini zaidi....
 
hili liko kwa namna tofauti sana, inategemea aliyekufa kaenda akiwa na umri gani na aliowaacha wakoje kimaisha. kama akiondoka baba kaacha watoto wadogo ni dhahiri kuwa mama atalia kwa mengi. na hata kama atakuwa hajaacha tegemezi la kimaisha basi mkewe atalia kwa kukumbuka upendo na huruma za mumewe and this applies the same anapokufa mama
 
inabidi kama ni mwanaume na mkeo ni mama wa nyumbani,tafuta ka shughuli/kibanda.... ka kumzoeza mkeo kuwa na financial freedom hii itamjengea kujiamini zaidi....

hiyo inaapply padogo sana ma dia nimewahi kushuhudia mtu anahela but alilia kwasababu ndugu siku hiyo hiyo walitia kufuli nyumba. wewe bwana hasa akina mama wanalia kwa mengi
 
hiyo inaapply padogo sana ma dia nimewahi kushuhudia mtu anahela but alilia kwasababu ndugu siku hiyo hiyo walitia kufuli nyumba. wewe bwana hasa akina mama wanalia kwa mengi

Hebu funguka, imagine hutaki hilo litokee kwako utafanya nini?
 
Hebu funguka, imagine hutaki hilo litokee kwako utafanya nini?

Broo lee kitu binafsi mimi na mr huwa tunashirikiana kwa kila jambo kiasi kwamba kila kitu tunakifanya sisi peke yetu. hatunaga 3rd person kwetu. hii inanipa confidence on what we possess as our assets. pia inawanyima ndugu nafasi ya kuyaingilia maisha yenu
 
kuna baadhi ya akina baba wanawafanya wake zao hama watumishi wa ndani.

Hawataki wamiliki hata kikombe.
 
gemezi ndo unaowaumiza walio wengi..lakin akiwa kama mama wa kujituma atalia kumpoteza mumewe na sio ataleaje watoto.
 
Kulea hao watoto hadi wajitegemee si lelemama mfano alizoea kula vyuku mmewe ndo mtafutaji ni mzigo.nashauri wapendwa tuweke akiba benki za watoto tuwekeze nguvu kujijenga mfano ukiweza nunua hata viwanja vitano jenga pangisha au kodisha watu walime as means of income kwa familia.
 
kwa kweli hii kitu kipo na kinaumiza sana hata kama humjui aliyekufa, ni kwamba huyo marehemu anakuwa hajaweka wazi mambo yake kwa mkewe na ndio maana mama hajui pa kuanzia ni vyema akinababa mkashirikisha akina mama kwa kila kitu hata kama ukifa talia kwa sababu sitakuona tena lakini sio ntaishi vp na watoto.
 
Kwani hao wanawake wanashikiliwa mikono wasimiliki mali? Eboo! Saa ingine wanawake tunajilegeza mno bana!
kuna baadhi ya akina baba wanawafanya wake zao hama watumishi wa ndani.

Hawataki wamiliki hata kikombe.
 
Kama una mali na kauwezo fulani, wekeza akiba benki ya watoto ya hapo baada ikiwezekana andika wasia hii itawalinda watoto na mama yako endapo itatokea kinyang'anyiro cha mali toka kwa ndugu wa mume.

Kama hauna chochote hapo ndo kasheshe mwache mama alie bwana.....kama walivyosema atalijua jiji
 
aisee kitu kama hicho kinasikitisha sana ndio maana nchi zilizoendelea wana life insurance ambayo wanalipa pesa kidogo kwa mwezi kwa hiyo hata siku mwanaume ukirudisha namba..una uhakika kua wife na kids wako taken care of... but kwa hapa bongo inasikitisha sana...watoto wanne usawa huu unaanzaje anzaje...its a very sad situation and i really feel for the woman and her family:thinking:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom