Inakuwaje Mambo haya?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje Mambo haya??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Apr 6, 2011.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wapendwa wangu
  Its my greates hope kuwa mu wazima kabisa. Nimewamisije mwenzenu?

  Nway nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu kuhusu mahusiano najikuta natoka kapa. The more you struggle to understand it, the more confused you become.

  Najua karibia wote tunajua uchungu wa kupenda mtu ambaye mapenzi yake yako kwa mtu mwingine, na mbaya zaidi pamoja na kujua hilo bado tunajitahidi kumpenda na kufanya juu chini abadili mwelekeo wa mapenzi yake toka kwa huyo mtu mwingine yarejee upande wako.

  Wengi tumejikuta (au wamejikuta) wanapenda mahali palipojaa yaani kama ni kazi basi twaomba sehemu ambako tayari nafasi zishajaa lakini tunajipa moyo na kuhangaika kuwin that heart. Si hivyo tu kwa wale ambao tayari wako kwenye relationship ya pamoja kuna wanaojikuta wenzi wao wanafall kwa third person na bado tunafanya juu chini kumnyakua kutoka huko alikofall kwa mtu wa tatu arudi kwetu.

  Hii mambo kwangu ni ngumu..........nawaza kama kafall kwa mwingine in the first place.......kwa nini usiushurtishe moyo wako umwachie aende kuliko kustruggle ili arudi (wengine huenda extra miles kwa waganga!!)

  Inakuwaje mambo haya??

  Mimi nakumbuka there was this guy...oh my GOD.....yaani alifikia hatua ya kunipa ratiba kabisa kuwa leo ninakwenda kwa flani nami nikajikuta nakubali na kuhangaika kumwonyesha mapenzi but at the end of day I lost him completely.......
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Love is blind....!!!

  though kung'ang'ania usipotakiwa kuna sababu nyingi....kutokujiamini,kuchoka kuwa na mahusiano,sababu za kiuchumi na kijamii mfano kama uko kwa ndoa wengine hujiuliza watu watanionaje,watoto wangu watalelewa bila baba etc.

  Kusema ukweli nimewahi kupenda sana ila hakuna ambapo nimeng'ang'ania baada ya kugundua jamaa ana mwingine....no second thoughts!!!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Michelle........... Aksante mydia
  Huwa nachoka pale tunapovumilia na visivyovumilika....mie hadi leo hii na uzee wangu nikikumbuka nloyafanya kwa kijana yule enzi zile loh nashikwa na hasira haswa!! But it was a good lesson kwangu...... never repeated again ......akisema ana mwingine ntatoa baraka zangu zote lol
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuna watu hua wanaamini wanaweza kumfanya mtu awapende kwahiyo hawakati tamaa..kuna wale wanaomini hamna mwingine kama huyo or atleast mwenye vigezo vilivyomvutia kwake on the first place..kuna kutojiamini..kupenda kwa upofu..kukataa matokeo yani kuna watu hawakubali kushindwa..woga!
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Hizo hasira tunazo wengi ila ndo hivyo.....you can't turn back the days....hilo tu ndo waga linanipa shida...natamanigi ningezaliwa upya...!!!!:bored::bored:
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inakera sna kupenda usipo pendeka
   
 7. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhh
  Mambo kama haya yaposana
  Lakini kitu nilichogundua huwezi
  king'ang'ania penzi ..utahangaika
  juu chini kumshikilia lakini kama penzi halipo
  hatashikika...

  Borea uishi pekee
  Yako .kuliko kuishi na mtu
  Ambaye mwili tu ndo uko hapo
  akili, mawazo, roho, na kila kitu
  internally kiko kwa mtu mwingine..

  o sababu mbili tu
  zinazofanya watu wasiopendana
  Kuishi pamoja nazo ni mali na familia.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hii inaweza kumkumba wa jinsia yoyote. Jamaa mwanamume ninayemfahamu, aligombana na mpenzi (mke) wake, yule binti akakimbilia kwa bwana mwengine, ambaye alikuwa rafiki wa wote, na hii ndio ilokuwa sababu ya ugomvi wao wa siku nyingi. Marafiki zake wakamwambia bibi yuko wapi, akajipeleka akawakuta wote wawili. Yaliyoendelea ni udhalilishwaji; kwa hiyo kwa nini uendelee kung'ang'ania na kudhalilishwa? Ikiwa ni mapenzi na/au usaliti, bado ukweli unabakia palepale kuwa "ikiwa mapenzi ni maua, tusiangalie kuchanua tu, vilevile tukubali yanakufa", tukubali matokeo na kujipanga upya.

  Mara nyengine mwenza wako, m'mume au m'mke, anatumia watoto kama njia ya kukutishia ikiwa mtaachana atakwachia watoto. Let her/him go to hell. Better be alone than in a bad company. Kwanza watoto ni wenu wote, kwa hiyo ikiwa ni zaidi ya mmoja mnagawana, ikiwa ni mmoja kubali dhamana lakini usikubli katu kudhalilishwa.
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, uzuri ni vile siku hazigandi, na mwanadamu ameumbiwa kusahau.
  Lakini kwa kweli hakuna maumivu makali kama ya kuupenda moyo, usiokupenda.
  Nafsi na akili ambavyo wewe, ukiwaza mashariki, vyenyewe vinawaza kaskazini. Dah!!!!
  Tusonge mbele tu, ya kale yamepita MJONE.
   
 10. k

  kisukari JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,762
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  mmmh,yameshanikuta hayo.ila baadae unajifunza kutokana na makosa na kujiuliza ilikuwaje nilikuwa mjinga kiasi hicho?
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lizzy umesema kweli loh yaani kuna wakati nilikuwa ninafikiria hayo kuwa hapana huyu nitamwonyesha kuwa nina uwezo wa kumrudisha kwenye himaya yangu loh...........I tried weeeee but where (wanajisemea watoto wa mjini!!) ila ajabu nilipoamua kukata tamaa ndo naye akazinduka usingizini loh lakini nilishajichukia kwa upuuzi wote nloufanya kumuwin back......miaka imekwenda na uzee umekomaa eti bado ananikumbuka na kukumbuka penzi langu jamani!! .........sasa sijui ni penzi lipi lile la mwamzo au lile la ziada.
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwali usinchekeshe asa ukizaliwa upya si utakuwa malaika?? Maana ushayajua maovu yote na tricks zote nani atakuchakachua?? but wengi tunawish tungeweza kurudisha nyuma siku tukarekebisha pale tulipokosea......wapo wanaotamani ili wawapate tena wenzi wao, na wapo wanaotamani siku zirudi ili wabatilishe maamuzi yao ya kuwa na wenzi walionao sasa!! Haya mahusiano haya!!
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Umeona eeh Maria Rosa?
  Yaani inakera but ajabu ni kuwa wakati ule wala huioni ile kero au ni kwa vile sometimes unajiblame kwa makosa yasoyako na unafeel kuwa wewe ndio chanzo cha mwenzi wako kumfuata that other person hivyo ni wajibu wako kumwonyesha kuwa unampenda na umejirekebisha ili arudi kwako!!!

  Laiti moyo ungekuwa na kifuniko, tukaweza kufunua mioyo ya wenzetu na kujua yaliyomo tusingekuwa twaghangaika hivi.
   
 14. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ni maisha...tunakua sensitive sana kutoa ushauri na kuelekeza wenzetu pindi yakiwafika na we wish wachukue ushauri wetu pasi kuu-edit...well ni kitu kizuri! Kimbembe ni pale yanapotufika wenyewe...hatushauriki maana tunakuja na solutions zetu km afadhali kukesha baa,natafuta mke/mume,nitakua womanizer n so forth ...yote tisa ukwel ubaki pale pale kwamba ni mzigo mkubwa sana kungangania tusipopendeka! Mapenzi si ugomvi ni maridhiano ya nafsi so moja ikichoka let it go ya nini malumbano banaaa! Salaam zenu wajumbe wa jukwaa pendwa!
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,053
  Likes Received: 24,056
  Trophy Points: 280
  Mjukuu mtiifu, babu ako haelewi maana ya hiyo hapo kwa red (damn uzee)...waweza kunidadavulia wakati naendelea kuielewa hii thread yako? Ahsante kwa kunielewa.

  Wakati naendelea kuielewa, ngoja nikunong'oneze (Samahani sijapiga mswaki)......unajua kuwa mapenzi ni upofu na ukiziwi kwa apendaye pale asipopendwa?...atafanyiwa kila visa lakini atakuwa haoni, ataambiwa kila uchafu lakini atakuwa hasikii......

  Sasa hii ya kurudi mara ya pili, baada ya wewe kumtapika, ukweli ni kuwa wakati ulivyokuwa ukimpenda ulikuwa unampa vitu vyote (ili usimpoteze, siyo?) Kama ni kitandani ulikuwa unawajibika ipasavyo, kama kiuchumi ulikuwa unamkabidhi kipato chako ili atumie atakavyo....... Kwa kifupi ulikuwa unampa kila kitu kwa gharama ya juu ili usimpoteze......Sasa huko aliko hapatiwi vitu hivyo, au alikuwa anapatiwa na sasa amenyimwa ghafla wakati bado ana kiu navyo.......... atapiga mahesabu yake na kuku-kumbuka "mjinga wake"......Atatafuta njia zote akurudie, atajifanya anajutia mabaya aliyokutendea, atamsingizia shetani, ataapa kwa miungu ya kwao kuwa hatakuumiza tena.........

  Mjukuu mtiifu, amini, amini nakuambia.... Akirudi huyo usijidanganye, ukampa kama zamani, kiu yake ikikatika atakupiga pigo jingine kuu. Na mara nyingi pigo la pili laweza kuleta maafa makubwa zaidi.........usithubutu kukutwa, watakucheka watu!

  Narudi kitandani kumalizia usingizi wakati nikiendelea kuielewa hii sredi.
   
 16. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  it pains,but let it go n start afresh! Mungu ameumba binadamu wengi kwa hiyo bado kuna chance ya kupata rum to someone else!
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,053
  Likes Received: 24,056
  Trophy Points: 280
  I have a room for you darling....Kimey akikuletea za kuleta, you know where to find me.
   
 18. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mapenzi UPOFU! Akiwa na CHONGO wasema KENGEZA.... We Acha tu...
   
 19. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  thx darling,ur so considerate,,,,ntakuja fasta hope u won't break my heart,
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Apr 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  MJ1,
  Where does fall in love with a person who doesnt love you stop? which is the cut off point??? at tender age or even after becoming old as we are(50yrs)??? I wish I could know the limit...From what i have been seeing, probably I miss a point!!!!
   
Loading...