Inakuwaje mafisadi kugombea ubunge ikiwa walishaonekana hawafai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje mafisadi kugombea ubunge ikiwa walishaonekana hawafai?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyadhiwa, Sep 27, 2010.

 1. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi inakuwaje Lowasa ambaye alilazimika kuachia ngazi ya uwaziri mkuu kwa makosa aliyoyafanya anendelea kugombea?
  Je ni uhaba wa watu safi wenye uwezo wa kugombea, au ni ufinyu wa mawazo ya wanaohusika kuchunguza mambo hayo?

  Je kuna kupiga vita ufisadi kweli ktk nchi hii? Na je watakuumbatiwa mpaka lini?
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mafisadi wana nguvu sana ndani ya CCM, Chama hiki kimekosa mtu hata mmoja wa kukemea mambo haya na ndiyo maana kinajiendea tu kama gari lisilo na mwelekeo.

  Kila mtu amekuwa msemaji wa chama, JK na Makamba ndiyo wahusika wakuu kuchangia kukivuruga na kusababisha kikose Mvuto, Uaminifu kwa wananchi na hii ni turufu tosha kwa CHADEMA kutumia golden chance hii kushika hatamu kwani wana support kubwa ya Umma wa watanzania na DR. Slaa anaaminiwa sana.

  CCM haiwezi kusema chochote juu ya vigogo hawa
  1. Edward Lowassa (Richmood)
  2. Endrew Chenge (Rada)
  3. Rostam Aziz ( Kagoda)

  Hawa ndiyo walikuwa mstari wa mbele kuiweka serikali ya sasa madarakani sasa unategemea nini hapa?
   
 3. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jambo ambalo bado watz hawaelewi ni kwamba wooooooooooooote wanaogombea kupitia CCM, kwa namna moja ama nyingine wanahusika na rushwa. Rejea zifuatazo zitawapa mwanga ndugu zangu:
  Andrew Chenge: Akihojiwa na waandishi wa habari pale Mwl. Nyerere Int. Airport kuhusu tuhuma za US$ 1,000,000/- kukutwa kwenye akaunti yake nje ya nchi, aliwajibu "mnashangaa kwa hivi vijisenti tu, mkisikia hao wenye mahela huko nje". Hajazikana, hajaulizwa kazipata vipi, na wala hajashitakiwa chini ya sheria ya utoroshaji wa fedha (Watu wa sheria msaada pls).
  Sophia Simba: Wakati wa mfarakano wa wabunge wa CCM, bi. Sophia Simba alinukuliwa akisema, katika wabunge wa CCM hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole, kwani wote walipata ubunge kwa kusaidiwa na hao wanaowaita mafisadi. Akaenda mbali zaidi na kumtuhumu John Malecela kuwa hata harusi yake na Anne Kilango, alipewa hela na mmmoja wa mafisadi.
  Makongoro Mahanga: Katika mfarakano huohuo wa wabunge wa CCM, alisema nawashangaa watu wanajifanya wanapambana na mafisadi, yupi kati yetu anayeweza kumsema mwenzie fisadi?
  Edward Lowasa: Baada ya ripoti ya Richmond kutolewa na Mwakyembe, katika utetezi wake alisema "tukianza kunyosheana vidole humu ndani hakuna atakayebaki msafi".
  Makamba: Baada ya mchakato wa kupata wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi kupitia CCM, alinukuliwa akisema wagombea wote walitoa rushwa walichozidiana ni kiasi tu. Hajakanusha hiyo kauli mpaka leo. Zingatia huyu ndie mtendaji mkuu wa chama hivyo kauli yake kwa masuala ya chama chake ni kauli ya chama.

  Akili kumukichwa ndugu yangu, kama utaamua kuwachagua viongozi rushwa ama utachagua viongozi makini.
   
 4. M

  Msharika JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huu ndio wakati muafaka wa kumchagua Silaa, mwenye uthubutu wa kusema bila kumumunya baada ya kufanya tafiti na kuwa na data za kuthibitisha.
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Malaria Sugu tunaomba mchango wako kwenye mada hii tafadhari
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  wamasai Kule jimboni they dont care lowassa fisadi au kafanya nini? Wakimtoa Lowassa kule Basi CCM wamekosa ! sijui kawapa nini wale masai kule.. wameridhika naye kabisa:confused2:
   
 7. Kakati

  Kakati Senior Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  If we do what we always did, we will get what we always got. I mean, if we choose the same corrupt people to be our leaders we will always be led in the same corrupt way.
   
Loading...