Inakera sana: Ndugu kugombea maiti.....

Inakera sana: Ndugu kugombea maiti.....

Ndiyo tatizo la kuabudu wafu na mizimu, mali kitu gani ukauweka ubin adamu mbali?
aibu kubwa hii lakini wewe na mimi tumejifunza nini?
 
Tatizo hapo ni kuabudu mizimu ya wafu, Wachaga badilisheni mfumo wa imani, mnaitia aibu tanzania
 
yani ni aibu tupu na akuna jingine zaidi ya mali sikweli wanagombea maiti
 
Ni aibu....imenikumbusha mizunguko yangu Tanganyika. Nilikuta kijiji fulani kuna wazee wamemkalisha Kidevu kisa eti mti wa muembe uliopo shambani kwake ni wa ukoo asipunguzie matawi. Kidevu aliwajibu shortly kuwa huu ni unyanyasaji hakuna mtu hata mmoja amewahi kuja kupalilia huu mti tangu nikabidhiwe shamba na baba over 20 yrs ago, iweje leo mlete habari za kuwa eti ni muembe wa ukoo? Sasa nasema yeyote mwenye mawazo hayo nitakula hitma yake......!Nilikuja kusikia baada ya mwezi mmoja jamaa mmoja katika wale alivuta.....Kidevu mwenyewe nilipomuuliza alisema hahusiki ni Mungu tu mwenyewe kazi yake! Dhuluma mbaya ni laana....tuache
 
Tatizo kubwa lililopo hapo ni hali duni ya maisha ya mtanzania. Familia inakuwa na watoto wengi, haiwezi kuwaendeleza wote. Wachache wanaoendelea wengine wanawa-mind.

Pia mfumo wa serikali ni batili. Kama watu wangekuwa wanalipia mali wanazomiliki kila wanachotakiwa kulipia, wangeona hadha ya kumiliki mali. Walioendelea hawana hata mawazo ya kujenga (waliowengi) wao ni kupanga tu. Hawana haja ya kumiliki gari wao ni usafiri wa umma. Ila huku kwetu ni kinyume kabisa. Sidhani kama tutaendelea.

Jaribuni kutafuta hii kitu inaitwa maisha katika Kibutz mtaelewa nina maana gani.
 
Hilo la ushirikana sina uhakika nalo ila kwa nchi inayokaribia Nigeria kwa mambo ya uchawi na utabiri siwezi kushangaa.

Hii tabia ni ya kawaida sana mkoani Tanga. Mgonjwa anatelekezwa na kutunzwa na hospitali pale Bombo, ila akifariki tu na maiti kupelekwa mortuary wanajitokeza ndugu hadi ukoo mzima kiasi ambacho huwezi kuamini.

Halafu nasikia huwezi kuzika binti wa Kibondei. Wanakupa mtoto wao unatunza na kutesa naye ila akifariki warudishie maiti ikazikwe Bonde. Nadhani yapo mengi kwenye hii issue. Ngoja tuwasikilize watu wengine, labda tutapata updates toka Usukumani, kwa Wagogo, Wanyalu n.k.


Duh! Hiyo ni mpya kwangu!

Leka
 
Back
Top Bottom