Inakera sana: Ndugu kugombea maiti..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakera sana: Ndugu kugombea maiti.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Jan 22, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa TBC Taifa wanajadili tatizo linalozidi kushamiri hapa Tz la ndugu kugombea maiti. Hii inafuatia jamaa mmoja kupoteza maisha baada ya kushinda kesi aliyofungua wakati akigombea maiti ya ndugu yake. Wadau wanatoa michango mingi na mizuri ila sikuweza kuisikiliza yote.

  Naomba nasisi tujadili kwani hii tabia inanikera sana.
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Aliyefariki ni aliyeshinda kesi ya kuzika dada yake.
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni makubaliano ya watu wawili walioridhiana kuishi kwa pamoja, na ukiishi na mwanamke/mwanamume ndani yamiezi sita mfululizo ni mkeo/mumeo hata kama hamjafunga ndoa (awali ilikuwa miaka miwili) na kama mtafunga ndoa iwe kimila, kiserikali au kidini basi ndiyo kabisa umepigilia msumari. Huyo Mary Kileo alishaolewa mwaka 1999 na muwewe akafariki mwaka 2002 na akafunga ndoa mpya na mume huyu mwaka 2008 kwa mkuu wa Wilaya Kahama. Kwangu hii ni ndoa.

  Wachagga hapa wanalilia mali tu za huyu dada yao kwani alikuwa ni afisa Ugavi(mambo yao si unayajua tena na chenji). Na kwa kuthibitisha hilo ndugu wa marehemu Mary tayari walishakamata gari japo vielelevyo vya gari anavyo mume wa marehemu.

  Hili ni kosa kubwa sana kwa ndugu kutaka kuingilia mali za ndugu marehemu ambaye tayari alishaolewa. Sasa huyo kaka aliko kuzimu sasa amefaidi nini? Kumbuka ukishapokea mahari zinaambatana na mila na kwa wakati mwingine mila huwa ni balaa kuzichezea, makabila mengine mila hizi ni kama mizimu ya kutambikia, sasa wewe unachezea mizimu kisa kijigari, pesa, pengine na mali nyinginezo. Yaani unazembea kujituma kupata mali unasubiri za ndugu akifariki? Sasa basi naamini kuwa kaka yao marehemu alikuwa na mke, basi na waende tena mahakamani wakadai kuwa si mke halali ili wafaidi mali za ndugu zao wawili. Kumbuka kuwa ukifa unaacha mali zote ikiwemo pesa, sijui ni nani alishaomba azikwe na nyumba, pesa, vito vya thamani hata mke/mume na watoto hata kama uliwapenda sana. Ifike mahali tuthamini utu zaidi kuliko mali.

  Kitendo cha jana ni fundisho kwa makabila yote ambayo yanagombania mali za ndugu. Ni fundisho pia kwetu ambao hatuandiki wosia wa mali zetu na utaratibu mzima wa maziko pindi utakapokufa hasa kama umeoa/olewa na kabila tofauti. Haya yakiwekwa wazi huwa yanapunguza kwa kiasi kikubwa mitafaruku mingi.

  Wachagga jana mmetia aibu kubwa mno, mnaonekana ni waroho wa mali na adhabu ikapatikana instantly!!! Sasa leo msiba umehamia wapi? Hata marehemu mwenyewe anahuzunika mnapigania kiwiliwili chake. Je mnafahamu ni kiasi gani ambacho alikuwa anampenda mumewe na leo mnamnyanyasa? Hivi hawa ni wachagga wa eneo lipi? Mwenye kuwafahamu rusha hapa. Shame on You.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mila na desturi hizo!
  mimi nimeona jamaa anaitolea mahari maiti!...ni vitu vidogo sana lakini vina maana kubwa
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Hili ni fundisho tosha kwa wale ndugu wanaopenda kugombea maiti na mali, huyo kijana mali za dada yake zimemtokea puani.
  Vile vile tuwe na utaratibu wa kuandika mirathi na sehemu unayotaka kuzikwa ukifariki.
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Maane nakuunga mkono,haya mambo hatuna budi kuyaacha,mali tunazigombania lakini mwisho wa siku tunaziacha hapa hapa. Mimi ni mfano mzuri sana,nimezaliwa katika familia zenye matatizo hayo.

  Kuna watu walinidhulumu kila kitu kutoka kwa wazazi wangu, lakini leo hii hao ndugu nawasomeshea watoto wao.Wanaona aibu sana na Mungu amewapa uhai waone maisha yangu kuwa hayakuwa yanategemea mali walizoacha wazazi wangu.

  Huyu jamaa aliyekufa ni fundisho kwa watu wote wanaopenda kugombea mali. Huyu mke wa huyu marehemu mpya namuonea huruma sana,maana hii familia kimeo.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi watu kwa nini wasitafute kwa jasho mpaka wasubiri marehemu afe ndo waanze kutoa macho kwenye mali zake
  Inakera sana
   
 8. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  1stlady hawa watu wanapokea mali lakini wanataka kuendelea kuwa na haki na ndugu yao. Sheria ziko wazi kabisa,mtu akioa au kuolewa mali zake ni haki ya mwenzie na watoto wake unless atoe mwenyewe kwa mtu mwingine akiwa hai.
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mkuu Geoff, mahari ni hatari sana. Ndiyo maana ikiwa unataka kumtolea mwanake mahari ni lazima uwe kweli umeamua kuoa, si mchezo. Na kwa mila nyingine mwanamke akishatolewa mahari yaani ni kifungo, ni lazima pia uwe umeridhia mahari hiyo. Na kwa makabila mengine ukishatolewa mahari na kama ndoa haikufungwa basi huwa mahari haitolewi mara mbili, mwiko!!! That is huwezi kufanya the same mila/matambiko kwa mtu mmoja zaidi ya mara moja. Ukitaka kufanya hivyo ni lazima ufanye tena mila kubwa za kupooza ile ya awali ambayo it is expensive to do that.

  Kama ulivyosema, kwa mfano ulishaishi na mwanamke na kwa bahati mbaya akafariki kabla hujatoa mahari au kukamilisha mahari basi ni shurtu ukamilishe mahari ndipo upewe kibali cha kuzika, of course inakua ni kiasi tu cha mfano angalao uonekane umetenda. Unafahamu kuwa wanaamini kuwa ile mahari inashikirikisha pia mababu na mabibi ambao walishafariki, eti kuwa siku ya mila baadhi ya vyakula kwa baadhi ya makabila, hasa pombe na vitu kama damu huwa vinamwaga chini kuwapa wazee, this is dangerous.

  Yule ndugu Sukari jana alilia kwa masikitiko na kutaja mahari yake ambayo hata marehemu wa jana alihusika kupokea, kilichofuata mlikiona. Na wakicheza watapoteza roho wengi pale. Wamwache mume azike mke wake. Tena na kichanga cha miezi 8 na wiki 2, je wachagga nacho mnataka mzike!!?? Mnataka kujimaliza nyie, kama kuna mtu anawafahamu wapeni hii niliyoandika hapa itawasaidia. Kwa kiasi mila naheshimu japo sijishughulishi nazo kwa kiasi kikubwa. Na huwa zinasumbua ndiyo maana watoto wangu sikutaka kuwahusisha na kuwafanyia mila zile hatari maana ni kifungo ni lazima wao wafanye pia. Too bad.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yaani jamaa amekufa mahakamani kwa fraha kushinda kesi ya maiti kwa nini haswa watu wanagombea mtu aliye kufa? Wanataka kutambika?
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa bold umenikuna penyewe. Na nitapenda sana Mungu awaweke hai wale woe wanaodhulumu yatima au mjane na kuona maendeleo ya wale watoto. Mungu mwenyewe alisema "Mimi ni mume wa wajane na baba wa yatima". Maneno haya ya Mungu huwa naya heshimu sana. Hebu tuzinduke, jiweke ndani ya viatu vya yatima na wajane/wagani tunaonyanyasa.

  Tena ni vema tukawa na upendo sana na wale shemeji zetu wanaoolewa na kaka zetu na pia kuwapenda wale wa upande wa dada zetu. Ndugu zangu wakileta za kuleta kwa wake zao nawatoa upepo kabisa, yaani kesi ikiletwa kwangu sina ndugu, bali nina shemeji tu na huwa wananiogopa kama pilipili. Sitaki upumbavu kabisa katika kunyanyasa mke. Na ndugu akifariki shemeji mali ni zake na watoto wake, ila akiamua kuolewa ni shurti aziache zile mali ambazo ziliandikiwa watoto na zile alizoandikiwa na mumewe ana uhuru nazo na kwa busara aachie watoto akitaka ila si lazima. Na hiyo iko wazi katika vikao na utaratibu wa familia na ukoo mzima.
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani ubinadamu uko wapi tena, kwann watu tunathimini pesa kuliko utu? inabidi tuwe na aibu kidogo tumwogope Mungu ndugu zangu. sasa hawa ndugu watamzika yupi kwanza? Real shame on you!
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kuna mchangiaji mmoja wa TBC Taifa amesema kuwa ndugu hawapendi kumuuguza mgonjwa kwa sababu ni mzigo na hasara ila wanagombania maiti kwa sababu ni dili. Nadhani kuna ukweli fulani katika hili....???:confused:
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hehehehe dah alafu ndugu wangekuwa wanagombania mgonjwa kuuguza mbona wagonjwa wangekuwa wanapona kwa faraja. Lakini utashangaa wkt anaumwa hao jamaa walikuwa mbaali kafa basi wote hao wanagombania ndo maana mm naamini wanagombania kwa ajili ya mambo ya kishirikina zaidi.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hilo la ushirikana sina uhakika nalo ila kwa nchi inayokaribia Nigeria kwa mambo ya uchawi na utabiri siwezi kushangaa.

  Hii tabia ni ya kawaida sana mkoani Tanga. Mgonjwa anatelekezwa na kutunzwa na hospitali pale Bombo, ila akifariki tu na maiti kupelekwa mortuary wanajitokeza ndugu hadi ukoo mzima kiasi ambacho huwezi kuamini.

  Halafu nasikia huwezi kuzika binti wa Kibondei. Wanakupa mtoto wao unatunza na kutesa naye ila akifariki warudishie maiti ikazikwe Bonde. Nadhani yapo mengi kwenye hii issue. Ngoja tuwasikilize watu wengine, labda tutapata updates toka Usukumani, kwa Wagogo, Wanyalu n.k.
   
 16. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ukigundua kuwa mali ni vitu vya kupita na sisi binadamu hatuwezi kudumu milele,hutaweza kufanya mambo waliyofanya watani wetu wachaga. Jamaa wanaheshimu sana pesa kuliko utu wa mtu.

  Mahari ya jamaa wa watru walichukua leo hii wanafanya umafia kumpora mwili wa marehemu mkewe. Hii siyo haki hata kidogo. Haya mambo yana mwisho wake,kama jamaa angekubali mambo yaiushe mapema bila mikwaruzanio wala asingepata presha zozote,kajiletea presha mwenyewe.
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Jamaa ana cheti kabisa cha ndoa, halafu ndugu wa Marehemu wanapigania akazikwe kwao , mimi nadhani ukoo wote ule ukapimwe AKILI, nadhani wanamatatizo fulani. Kwa nnini walipokuwa wanaishi ndugu hawakwenda pale na kusema wewe mwanaume hatukutambui? mimi ningekuwa na mamlaka ningemrudisha yule kaka aliyekufa awe hai halafu achapwe viboko kama 30 hivi halafu afe tena. na mahakama imekuwaje iruhusu ndugu zake wakamzike?? badala ya mumewe??
   
 18. E

  Edith.Lyimo New Member

  #18
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli watu tumezidi kupenda mali kuliko utu. Hata hatumwogopi Mwenyezi Mungu?
  Kwa nini tunajitetea kwa kutumia uongo mwingi sana ili tupate mali?. Jamani hili ni fundisho. Kila mtu ajitafiti amedhulumu wangapi kwa uongo alioutumia? Tumwogope Mungu! Mali zote tutaziacha hapa hapa. Hata kama huyo mume wa pili hakutoa mahari lakini ukweli kwamba alikuwa anaishi na huyo dada mpaka alipofariki mimi naona ana haki kabisa ya kumzika (Lakini inaonesha kuwa haki tuliyonayo sisi si haki ya mahakama maana tayari imekuwa tofauti).
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Makabila mangapi hasa yanapenda kugombea maiti? kama yanajulikana anayetoka kabila hilo aseme kuna siri gani kupelekana mahakamani?

  Kuna jamaa kutoka mwanza pia mkwe wake alivyokufa tu, ndugu upande wa kile walifika wakachukua hadi kandambili - jamaa mstaarabu akawaachia wakataka kwenda mbali eti wachukue na mwili ya marehemu mkewe akawaambia IMESHOSHA - niacheni nimzike mpenzi wangu - wakakubali ila kwa shida sana.

  Hili kabila ni hatari sana hasa ukiolea huko lazima uwe makini - wana matatizo. tunaomba mwana JF anayetoka huko atupe siri ya urembo kupigania kuzika kuna nini hasa - MATAMBIKO.
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hili limekuwa ni tatizo kubwa! Na hii yote inatokana na watu kutopenda kutafuta mali zao wenyewe, na matokeo yake wanakuwa wanapiga mahesabu ya mali za ndugu zao!
   
Loading...