Inachukua muda gani kujifunza na kufahamu vizuri mchezo wa karate?

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
315
740
Hapa ni kwa wale wajuzi wa mambo ya MARTRIAL ARTS.

Nimedhamiria kuingia mazoezini kwa mwanangu mmoja hivi kwa ajili ya kupata mbili tatu kuhusiana na mchezo huu wa ngumi.

Swali langu ni je, naweza kuchukua muda Gani kuwa fit katika hili?

Sina maana kwamba sijui niwe na mkanda mweusi, sijui wa njano (NO)

mi nahitaji kujua self-defence tu lakini kwa kiwango kizuri.

Swali la nyongeza.

Ni mchezo gani mzuri zaidi kwa ajili ya self defence?

NAWASILISHA
 
Vyema ukajua aina ya mchezo unaopendelea kujifunza, mbali na kuweka mwili fiti kuna tamaduni ya kila mchezo kulingana na Nchi yenye asili ya mchezo. Mimi niliishia Yellow belt kwenye KARATE, jambo jingine uwe na moyo mgumu mkuu hakuna show-off huko ukifanya mchezo utaacha siku ya pili tu.
Kung Fu- CHINA
Taekwondo- KOREA
Karate-JAPAN
Judo-JAPAN
 
Vyema ukajua aina ya mchezo unaopendelea kujifunza, mbali na kuweka mwili fiti kuna tamaduni ya kila mchezo kulingana na Nchi yenye asili ya mchezo. Mimi niliishia Yellow belt kwenye KARATE, jambo jingine uwe na moyo mgumu mkuu hakuna show-off huko ukifanya mchezo utaacha siku ya pili tu.
Kung Fu- CHINA
Taekwondo- KOREA
Karate-JAPAN
Judo-JAPAN
Showoff una maana gani
 
Ngumi au Self Defense ni umakini wako tu yani ukiwa makini tu bila hata ya Mafunzo yoyote yale unaweza kujilinda vizuri tu, maana kule Hawakufundishi namna ya kuwa makini na adui ila wao wanakufundisha namna ya kurusha ngumi, kurusha teke, namna ya kupangua mashambulizi, jinsi ya kusimama n.k kwahyo wewe kama umezubaa hata kama una black belt unaweza ukagongwa vizuri tu na mhuni wa kitaa anayejiamini! Na asikudanganye mtu likitokea Vagi hautakumbuka chochote kile sijui nirushe ngumi hivi au vile au sijui nisimame hivi yani adui hakupi nafasi ya kuanza kurevise ulichofundishwa kwahyo Self Defense ni Umakini wako wewe mwenyewe mwili wako unatakiwa tu kuwa na utayari, hizo nyingine mbwembwe tu movie zisiwadanganye yale matukio yamepangwa
 
Back
Top Bottom