Inachukua muda gani kujifunza na kufahamu vizuri mchezo wa karate?

Amanito

JF-Expert Member
Nov 20, 2015
249
1,000
Na pia haikuwa Muay Thai ilikuja kuitwa hivyo baada ya wao kuhitaji mchezo kwa ajili ya mashindano na kuondoa kabisa techniques ambazo zilikuwa kwa ajili ya kuua adui vitani awali ilijulikana kama MUAY BORAN.

Hii wa Thailand waliitumia katika vita kupambana na adui na kwa sasa ni vijijini sana ndo kuna mabaki ya wataalamu wake ambayo huyo Tony Jaa baba yake pia aliwahi kuicheza na kumpa vitu yeye pia.

Ukiifuatilia vizuri kuna techniques humo zinahusu wanyama kama Mamba, Nyani, Tembo, Nyati n.k

Bongo hii mtu akikwambia kaicheza na yupo fiti huyo muongo. Hiyo ni Traditional Martial Art ambayo ili uwe fiti ni lazima ufundwe kule kule na wenyewe kwanza siyo kuangalia you tube tu kuna matambiko yake pia.
Shukrani sana Mkuu.. Umeniongezea kitu ambacho nilikuwa sikifahamu
 

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
315
1,000
Napenda sana na nimefanya sana Kung fu

1. Tambua sababu ya wewe kujifunza mchezo husika. Unataka nini kwenye mchezo huo? Wewe self defense

Binafsi nilitaka kujijengea nidhamu binafsi, kuimarisha afya ya akili na mwili na kujijenga kiroho.

2. Tambua bidii katika kujifunza ndiyo nguzo, usiingie kutaka kujua self defense tu na kutoweka. Kuna makundi ya watu,

Kuna anayejua kucheza kata na anazo technique nyingi ila Hana nguvu ya mwili (ndani na nje) huyu akikutana na mtu mwenye nguvu na imara kimwili hatoboi kabisa. Kuna watu wana mikono mizito yaani wewe kublock tu mkono wake hutakuwa tofauti na mtu aliyepigwa.

Kuna yule mwenye nguvu na uimara wa mwili ila Hana mbinu. Huyu akikutana na mwenye mbinu na yupo imara ni lazima atapigwa.

Binafsi huwa naona ni bora zaidi kuujenga mwili kwa mazoezi imara kisha ndio uanze kujifunza hizo kata na techniques. Ila ukitaka uimara na wakati huo pia wataka master kata, hapa jiandae kwa mazoezi yaliyoshiba ili kuwa vizuri yaani nguvu na techniques.

3. Fanya martial arts yenye manufaa kwako, nidhamu itawale maana ndiyo nguzo kuu katika mchezo wa ngumi.

Mwisho acha kuuliza muda wa kuwa bora kwenye mchezo wa ngumi. Ubora wa karateka haitegemei muda ila ni bidii ya kujifunza. Na hii mchezo jitahidi ukianza usiache yaani endelea kufanya mpaka siku unakufa.

Marial arts ni maisha, hivyo ishi mchezo na uifanye kitu ambacho ni lazima kufanya kila siku ya maisha yako.
Umeeleweka Sana mkubwa
 

Umuzukuru

JF-Expert Member
May 30, 2019
489
500
Kama kweli unania unaweza kujifunza mwenyewe tu cha msingi bidii na nidhamu

Na ni rahisi ukitumia miondoko ya mtaalamu Bruce lee wanaiita jet kan do kama sikosei unachanganya na boxing(masumbwi) amini hakuna muhuni wa kukugusa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom