Inachefua sana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inachefua sana!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lekanjobe Kubinika, May 5, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mambo ya ndani na mwenza wako hayafai kuyasema kijiweni au nje. Udhaifu wa mwenzako unatakiwa kumsaidia muumalize ndani kwa ndani, kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu. Wewe unapowaambia wenzako mkeo habadilishi nguo ya ndani wiki nzima unataka wenzako wakuonee huruma gani? Kwa nini usimfunze kwa kuichukuwa ukamfulie halafu uone reaction yake? Au, umemnunulia nguo za ndani na ukaona bado habadilishi? Naye akikusema kwa wenzake kwamba unalala doro mtalimbo wako sekunde moja tu unadhani watakuonaje watu unapopita mtaani? Kumwambia nyumba ndogo kwamba mkeo "kama gogo" unamkosea mkeo sana na utalipia ufidhuli huo mpaka ukome, maana wakijua udhaifu wako watakuchomoa mpaka ushindwe kununua kanda mbili.

  Kuna mambo ambayo mtu mzima hatarajiwi kuambiwa afanye, yeye mwenyewe kama anayo akili sawasawa anatarajiwa kupima na kuamua afanye nini. Kama mwenzako ni mdhaifu na ameshindwa kutatua udhaifu wake maana yake na wewe ni mdhaifu vivyo. Kama wewe ungekuwa zaidi ungemnasua aondokane na udhaifu wake. Kama mke anavyojisikia vizuri kusifiwa na mumewe, kadhalika mume anajisikia vizuri akisifiwa na mkewe.

  Uking'ang'anizi wa mkao mmoja miaka nenda miaka rudi nyumbani kwenu ndio unaofanya vyumba vyenu vichuje kwa kasi na hata mkaanza kutazamana kama mazezeta. Kabla hamjaungana mlikuwa mko hyper hyper kila mtu kwa mwenziwe, sasa hamjiulizi inakuwaje chumvi haijakolea siku hizi ila kwa jirani tamu sana "chai" yake?

  Dunia imebadilika sasa na mdudu anawakodolea watu awameze kila kukicha. Kila mtu akae kwenye nafasi yake na ndoa zetu zitakuwa tamu kila leo. Mkate wa kuiba ni mtamu lakini madhara yake ni makubwa.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa mkuu nakubaliana na wewe mmeshakuwa mwili mmoja, sasa ukimsema mwenzako ni sawa na umejisema mwenyewe
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja 100%
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  [​IMG]

  ..."udhaifu" umegawanyika katika makundi mawili.
  • Udhaifu wa ndani,
  • Udhaifu wa nje.
  Malezi yanachangia kwa kiwango kikubwa kujenga/kupunguza udhaifu wa mtu LAKINI,
  mapungufu kwenye malezi yako yasiwe kisingizio cha mtu kutojifunza na kubadilika kadri
  maisha yanavyoendelea.

  ...mkuu huu ni uchafu bana. Hii tabia haikubaliki kama alivyo mzinifu, mlevi, mwizi nk
  Mtu asiyebadili chupi wiki nzima, ana akili timamu huyo? Tusisingizie hakuna mkamilifu kwenye tabia mbaya.

  ...naunga mkono hoja. Huu ni udhalilishaji.

  ...chukulia statement yako huyo mvaaji wa chupi chupi wiki nzima bila kuifua!

  ...mkuu, 'some words are easily said than done!' pamoja na uzito wa dhambi na matokeo ya uzinifu, Sababu za kutoka nje ya ndoa ni nyingi kulikoni hiyo ya kujitosheleza mahitaji ndani ya kuta nne.
   
 5. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160

  Nakuongezea sio kijiweni tu anakwenda kumwambia nyumba ndogo yake oohh mke wangu yuko hivi yuko vile na kanyumba ndogo ndo kanatake advantage hapo kanaendeleza kuona huruma kumbe wizi mtupu tu umejaa ujinga sana huu sijui mkoje nyie wavaa suruali sio wote lakini msinipige mawe.Inachefua sana haifai kabisa pambafu
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe kwa asilimia 100%
   
 7. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Well said mkuu!!
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180  :amen: Really hope everyone atazingatia...
   
 9. W

  Wakuchakachua JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmh yani mpaka hofu hizi ndoa hizi mungu saidia iwe salama loh loh
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sawa Wakuchakachua, Mungu atasaidia ikiwa utamshirikisha aingilie kati kusaidia. Amekwishakueleza kwamba "Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo magumu, makubwa usiyoyajua...... (Yer 33:3). Kama unatumia njia za mkato unavunjika guu lako wewe mwenyewe na wala usimlaumu Mungu kwa nini kakuachia hadi unaumia naye anakuona. Omba nawe utapewa, bisha hodi nawe utafunguliwa. Binadamu ameumbwa kwa sura ya Mungu mwenyewe na hivyo Mungu hafurahii binadamu anayekufa na dhambi. ndiyo maana watakatifu na wacha Mungu vifo vyao ni vya amani mara nyingi isipokuwa kama Mungu ameruhusu vinginevyo kwa utukufu wake. Ayubu si unakumbuka? Alikuwa kwenye mtihani na alipofaulu alizawadiwa. Yona alipokimbia maagizo Mungu aliamua hadi kieleweke, hata siku tatu akakaa ndani ya tumbo la samaki, sayansi wala haiwezi kuelezea hapo kuashiria kwamba sayansi si kitu juu ya mambo ya Mungu.

  Je, ni kweli ndoa zetu zinamshirikisha Mungu? Je, ahadi tunazotoa kwenye kufunga ndoa zetu tunazifanyia kazi wote? Katika mema na mabaya, umasikini na utajiri, magonjwa na afya, kutojishirikisha na wengine ila huyo tu, .....sasa nyumba ndogo inapoingia inakuwaje? Bora mwizi mwenye akili atatunza heshima ya mmiliki wake. Wewe unapomweleza housegirl mambo ya 6x6 na mkeo kwa sababu tu naye anakuhudumu una akili kweli wewe? Kuna mtu alifikia hata kumtaliki mke ili abaki na house girl ati amegundua house girl ana hazina kubwa kumzidi mkewe,...PAMBAF! Limbukeni huyo hana siri. hata panya anang'ata na kupuliza, paka anajisaidia kwenye unga na kufukia kinyesi chake humo tena anahakikisha hata harufu haitoki. Kwa hiyo uozo wako unauanika nje wewe mwenyewe kwa kumsema hovyo mwenzio, maana nyani haoni nanihii lake.
   
 11. A

  Aine JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mke/mume ni rafiki, mpenzi laazizi wako na majina yote mazuri unayoyajua, sasa ukiona kitu kibaya kwake unapomuambia mtu mwingine ndio umemsaidia nini? Meme/mke mzuri ni yule anayeongea na mwenzi wake na kumuambia akipendacho na akichukiacho, na mume/mke mzuri ni yule ambaye anajitahidi kukwepa yale mwenzi wake asiyoyapenda na kujitahidi kufanya yale ambayo mwenzi wake anayoyapenda ambayo si kinyume na mafundisho ya neno la Mungu. Ukisema nje ina maana umejisema mwenyewe na aibu inakuwa kwako, utanyooshewa vidole hadi basi na lazima ukikutana na yule uliyemuhadithia utasikia aibu tu, ila mwenzako kwa vile hajui uliyoyasema yeye hana aibu hata chembe!!
   
Loading...