Inabidi Watanzania tumuombe msamaha Rais Magufuli

Alidhani mtu kama wewe utamtia nguvu kwa kumshukuru kwa mema anayotenda kipindi kaanza kurekebisha nchi hadi sasa, kumbe yale ya upande wa pili ndio unashabikia!!!...akachoka akaona aanze kufanya tu kwa moyo Mungu atamlipa maana hafanyi kuifurahisha mishetani.
Tukisema usikojoe hapa!....tunamaanisha hivyo...ukikojoa tukikunyonga usije ukaanza kusema mbona adhabu ni kubwa, swala wewe ukifa hicho kitendo OVU hakitakuwepo na kikijirudia inamaana mtendaji yupo radhi kufa basi
bila katiba mpya, akiondoka tu na mishetani nayo inarudi tena kwa kasi ya ajabu
 
Nimejaribu muda sasa kuchunguza jinsi kiongozi wetu mkuu wa nchi alivyo na hasira mara zote aongeapo na sisi wanachi wake ni kama kuna kitu kikubwa sana kipo ambacho sisi wa tz tulimkosea maana Najiuliza

1)tulipata tetemeko akaongea nasi kwa hasira sana; kwani mimi ndo nilileta tetemeko? Najua wengi mnakumbuka speech ile.

2)Watanzania tuna uwawa msumbiji bado yuko kimya!

3) juzijuzi tu anasema tukikamatwa huko nje na madawa tunyongwe wewe hebu baba yako anasema ukikamatwa kokote kule unyongwe! Si dariri nzuri kabisa maana yake baba yako kakuchoka

4) tunapata janga la njaa lakini baba yeye bado yuko tayari tufe eti hakuna kutangaza njaa kutangaza tu??

Jamani list ni ndefu mno! Nauliza tulimkosea nini huyu baba yetu sisi?? Hivyo nashauri kama watoto tuulizane kisha tumwombe msamaha labda chuki hii kali dhidi yetu itaisha!
Kwa nini unafikiri Magufuli ni baba yako?

Huna baba?
 
PAYE
NSSF
WCF
NHIF
Bila huruma ile 8% badala ya kuongeza ufuatiliaji ilipwe ikapandishwa to 15%
Maisha ya kijana wa kitanzania ni ya taabu sana.
 
Mwenyezimungu pekee ndiye wa kuombwa na kutegemewa magufuli ni kiumbe tu

Mawazo yako ni ya kipuuzi. Kila binadaamu anamutegemea binaadam mwingine kwa mawazo, uongozi na kadharika. Mwenyezi MUNGU ametuumba kutegemeana huku akituongoza. Ni MUNGU ametupa Rais Magufuli atusaidie baada ya kuona nchi inateketea. Amini usiamini, kila kitu ni mipango ya Mwenyezi MUNGU.
 
Sera ya kijamaa uliona wapi ikafanikiwa ndo maana ujamaa uliporomoka, lakini huyo unayemsema alikuwa anavaa suti lakini ww humtendei haki mkuu Wa awamu ya nne! Kaweza kuunganisha barabara nchi nzima, kakujengea hospital ya moyo badala ya kupekeka wagojwa india ss hv ni hapahapa, kakujengea daraja la kigamboni badala ya kupiga mbizi tunasafiri kwa raha zetu ,wananchi wakiendelea na ujenzi nyumba za makazi kila kona ya nchi, katuletea umeme wa gesi na ss hv mgao umeme hakuna japo kuna matatizo madogo madogo ya kiutendaji wa shirika let, kaleta kampuni kubwa ya simenti ya dangote, katujengea hospital kubwa ilonganzila, ameweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma kila mwaka na kumudu kuwalipa wafanyakazi hewa wote nchini na aliweza kuajiri watumishi kila mwaka! Na cha kupongezwa zaidi kama nilivyosema mwanzo keki ya taifa tuliigawana wote na kila mtu alikuwa na hela mfukoni na jioni unapata bia zako mbili unaenda kulala safii, na mwisho katuletea jembe letu magu ila tu azitoe hizo hela benki kuu tunazihitaji mtaani maana kwa sasa mambo hayaendi ushahidi ss hv hakuna anayejenga jengo jipya hivyo maendeleo yamesimama kote nchini, hizo pesa rais wetu azitoe benk kuu abaki na hela yake ya matumizi vinginevyo tutaisoma namba nchi nzima haijalishi ww uko wapi!
 
Mawazo yako ni ya kipuuzi. Kila binadaamu anamutegemea binaadam mwingine kwa mawazo, uongozi na kadharika. Mwenyezi MUNGU ametuumba kutegemeana huku akituongoza. Ni MUNGU ametupa Rais Magufuli atusaidie baada ya kuona nchi inateketea. Amini usiamini, kila kitu ni mipango ya Mwenyezi MUNGU.
Huwezi elewa hayo maneno hadi uwe mpambanuzi wa mambo.hivi magufuli anaweza kuongeza au kupunguza riziki aliyokupangia Muumba? Aweza leta ukame au tetemeko?
 
Ishu hapa c msamaha. Tatizo ni kwamba hatujui maono ya Rais wetu, ndio maana tunapata shida nakuona km ana hasira. Nikweli inawezekana akawa na hasira km mwanadamu ila akasahau ni wapi panapostahili kuziweka hizo hasira. Ila anajua anachokifanya. Shida kukosolewa ndio sumu ya huyu baba, ila kwa upande wa pili hatuna budi kumkubali, hakika kafanya kazi na naamini atafanya kazi ila kwaupande wangu kuwanyamazishawapinzani, ikiwa kweli anahusika ktk hili itakuwa makosa kwakuwa mchangi wa wapinzani hapa nnchini in matikeo ya yanayoendelea SASA. Km c wapinzani tungeendelea kuwapo gizani had I kesho. Kwakweli hakuna haja yakuonba msamaha kwakuwa hakuna mtz alie mkosea labda ajipime mwenyewe km amekosea aombe watanzania msamaha. Km hajakosea aendelee kupiga kazi,
 
Back
Top Bottom