Inabidi Watanzania tumuombe msamaha Rais Magufuli

MWAKITWINO

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
227
121
Nimejaribu muda sasa kuchunguza jinsi kiongozi wetu mkuu wa nchi alivyo na hasira mara zote aongeapo na sisi wanachi wake ni kama kuna kitu kikubwa sana kipo ambacho sisi wa tz tulimkosea maana Najiuliza:

1) Tulipata tetemeko akaongea nasi kwa hasira sana; kwani mimi ndo nilileta tetemeko? Najua wengi mnakumbuka speech ile.

2) Watanzania tuna uwawa msumbiji bado yuko kimya!

3) Juzijuzi tu anasema tukikamatwa huko nje na madawa tunyongwe wewe hebu baba yako anasema ukikamatwa kokote kule unyongwe! Si dariri nzuri kabisa maana yake baba yako kakuchoka

4) Tunapata janga la njaa lakini baba yeye bado yuko tayari tufe eti hakuna kutangaza njaa kutangaza tu??

Jamani list ni ndefu mno! Nauliza tulimkosea nini huyu baba yetu sisi? Hivyo nashauri kama watoto tuulizane kisha tumwombe msamaha labda chuki hii kali dhidi yetu itaisha!
 
Huwezi kuomba msamaha kama hujuwi kosa lako. Baba anaweza kukasilika kama watoto hawana shukrani. Baba kajitolea kuisafisha nchi ili watoto wake tuishi vizuri, lakini hatuna shikrani. Baba yetu aliyeondoka alikuwa hatujali sana, tukipiga kelele, yeye anapiga suit anaenda zake Marekani, akituacha huku tunavaa mitumba. Watoto wake alitubaguwa, akachaguwa wachache akawapa uhuru wa kutumia Mali za wengi.

Hawa wachache, walipeleka watoto wao kusoma kwenye shule za gharama, na kutuacha watoto wake wengi watoto wetu kukaa chini bila madesiki. Akabaguwa watoto wake wachache wakiuguwa anawapeleka Appolo India, akaacha watoto wake wengi kutibiwa hospitali hazina vifaa, AKIWA yeye anapiga safari kila kona ya dunia.

Sasa tumepata baba mwenye kutupenda wote, ikiwa tutavaa mitumba basi tuko pamoja naye, safari haendi tuko pamoja naye, baba anataka haki kwa watoto wake wote sawa, lakini Sasa wake watoto waliokuwa wakipendelewa wamelemaa, hawawezi kuuishi bila ya kuwadhulumu NDUGU zao, tamaa imewashika wanafanya mpaka BIASHARA za uwovu.

Baba huyu ana haki kuwa na hasira kwani watoto hawana shukurani, anafanya wema bado mnataka zaidi na yeye hawezi tufanye kazi, tuache kuuza madawa na wizi baba atatupenda bila ya msamaha.
 
Ana hasira kwamba hakupata kura za kutosha mpaka ikabidi apewe ushindi wa mezani.
Tumuache andelee na hasira zake ili ifikapo 2020 awe anachukiwa zaidi na awe hajafanya lolote la maana zaidi ya kukimbizana na wapinzani.
Duh!Hivi kumbe kuna watu bado wanaamini kuna WAPINZANI Tanzania hii? Hebu nioneshe huyo unayemuona ni mpinzani ili nicheke zaidi.
 
Ndiyo kazi yake analipwa na faida zote anazopata pamoja na familia nzima, bila kusahau ulinzi wa hali ya juu.
Why should we apologize? He knew what he was getting into, huwezi ongoza watu almost 50 million alafu utegemee kila kitu kiende smooth, alifaa ajiandae emotionally kitu ambacho hakiwezi. In short ingekua ni ajira ya kawaida angekua ashafukuzwa kazi. Yapo lakini anayofanya positive na anastahili pongezi kwa kweli. Kazi aliyonayo si ya mchezo ni ngumu balaa.
 
Ana hasira kwamba hakupata kura za kutosha mpaka ikabidi apewe ushindi wa mezani.
Tumuache andelee na hasira zake ili ifikapo 2020 awe anachukiwa zaidi na awe hajafanya lolote la maana zaidi ya kukimbizana na wapinzani.
Ndo Wazo langu la kwanza kabisa...
Jamaa Anajua Wazi Watanzania Hawakumpa Kura...ana stress za kukataliwa! kwahiyo kila akituangalia jamaa huwa anajisemea "hii mijitu ilinipa kura idadi sawa na Kura Za Hashimu Rungwe??...Kweeli??
Sasa ngoja niikomeshe"
Shubaaamit!
 
Huwezi kuomba msamaha kama hujuwi kosa lako. Baba anaweza kukasilika kama watoto hawana shukrani. Baba kajitolea kuisafisha nchi ili watoto wake tuishi vizuri, lakini hatuna shikrani. Baba yetu aliyeondoka alikuwa hatujali sana, tukipiga kelele, yeye anapiga suit anaenda zake Marekani, akituacha huku tunavaa mitumba. Watoto wake alitubaguwa, akachaguwa wachache akawapa uhuru wa kutumia Mali za wengi. Hawa wachache, walipeleka watoto wao kusoma kwenye shule za gharama, na kutuacha watoto wake wengi watoto wetu kukaa chini bila madesiki. Akabaguwa watoto wake wachache wakiuguwa anawapeleka Appolo India, akaacha watoto wake wengi kutibiwa hospitali hazina vifaa, AKIWA yeye anapiga safari kila kona ya dunia. Sasa tumepata baba mwenye kutupenda wote, ikiwa tutavaa mitumba basi tuko pamoja naye, safari haendi tuko pamoja naye, baba anataka haki kwa watoto wake wote sawa, lakini Sasa wake watoto waliokuwa wakipendelewa wamelemaa, hawawezi kuuishi bila ya kuwadhulumu NDUGU zao, tamaa imewashika wanafanya mpaka BIASHARA za uwovu. Baba huyu ana haki kuwa na hasira kwani watoto hawana shukurani, anafanya wema bado mnataka zaidi na yeye hawezi tufanye kazi, tuache kuuza madawa na wizi baba atatupenda bila ya msamaha.
Pro-JPM bhana... maneno meeeeeengi wala hufahamu kwamba hapo amekejeliwa!!!Kuna mwenzako mmoja kaongea sawa na ulivyoongea hapo juu! Kuna maswa;i nikamuuliza ameshindwa kunijibu basi nisaidie wewe hapa:

Kufanya usafi ni pamoja na kuzoa matakataka na kwenda kuyatupa mbali jalalani!!!!

Nisaidie wewe sasa... hadi sasa ni matakataka yapi yameshatupwa jalalani! Au angalau yaliyo kwenye gari tayari kwa kwenda kumwaga jalalani!! Na kama sivyo, basi angalau yaliyo tayari kwenye mapipa yakisubiri gari za taka hili yakatupwe jalalani!!

Nisaidie kwanza hapo....
 
Mtindio w ubongo ni dhahiri kabisa.
Hakuna chama tawala ?
Hakuna vyama vingi ?
Hakuna upinzani ?
Kapimw akili yaweza kuwa wahitaji tiba kidogo Tu
MAJIBU:
-Chama tawala kipo ni CCM
-Vyama vingi vipo mfano CHADEMA, CCM, CUF nk
-Ila kuamini kama kuna vyama vya upinzani inabidi mtu awe na akili kama ZAKO.
 
Fikra mwendo kasi.Mwenzenu ndivyo alivyo yule.Si unajua majani yale kule kwetu ni sigara ya kawaida tyu
 
Back
Top Bottom