Ina maana Katiba haijafuatwa?

Ina maana Katiba haijafuatwa?

Hata hivyo waziri mkuu kamshukuru Rais kwa kuendelea kumuacha kwenye hiyo nafasi...
 
Opinion ya TLS ilikua sahihi.

Samia hajavunja katiba ana discretion ya kuendelea na aliowakuta au ateue wapya.

Ila sasa kuna Lacunae kwa maana kwamba hakuna Ibara inayotoa utaratibu wa mazingira ya kinachopaswa kufanyika kama akiopt kuendelea nao, wala hakuna sheria iliyotoa muongozo katika hilo pia.
 
TLS walipotoka, kwa bahati mbaya kabisa wafuasi na chadema wakalibeba Kama ilivyo wakatoa waraka kupitia katibu mkuu kuwa mama Samia anatakiwa kulivunja baraza la mawaziri
Nakumbuka siku ile humu makamanda yalijitoa akili, Ila Sasa hivi yapo kimya hata hayazungumzii tena kuvunjwa Baraza.
TLS imedharaulika Sana kwa hili!! Kiburi hakitawaruhusu kutengeneza kwa kuomba radhi!! Buriani TLS!!
 
TLS walipotoka kisheria. Kimsingi halazamiki kuvunja Cabinet/kuteua PM. Ni discretion yake.
Hii tweak aliyoifanya, nadhani ni kuweka heshima na utii kwa Surbodinates wake.. 'hey im your boss now, i can fire you anytime i wish!'.
Uko sahihi, alifanya makusudi kufanya tu remix, iliwengine waone kumbe she is a Captain of our vessel........then pia siyo mbaya kuwaweka watu kwenye taaluma zao
 
Jipe muda,, unaeza kuta akaapishwa Waziri mkuu mpya siku za usoni
 
Katiba ndio ina mkanganyiko

Ibara ya 51(2), ina mtaka Rais mara baada ya kushika madaraka kumteua PM.

Sasa haijaeleza je kama Rais ameshika Madaraka baada ya Rais aliyepita kufariki.
Inakuwaje.

Katiba ndio ina mkanganyiko.

Wala haina mkanganyiko hapo Mkuu, Raisi kushika madaraka sio automatically right bali ni hadi akiapishwa na Jaji Mkuu. Kwa hiyo kwa hali yoyote itakayosababisha Mtu akashika madaraka ya Uraisi kama raisi basi ataangukia kwenye hiyo kanuni hapo.
 
Mimi ni mtu ninayefuata falsafa ya ‘keep it simple’.

Sikuona sababu yoyote ile ya Rais Samia kulivunja baraza lote la mawaziri na kulisuka upya.

Mabadiliko madogo kama aliyoyafanya ni ya kawaida na niliyategemea.

Lakini tuliambiwa na watu mbalimbali kuwa eti baada ya Rais Magufuli kufariki, basi kwa mujibu wa katiba baraza nalo linavunjika na waziri mkuu anakoma kuwa waziri mkuu.

Nilipovisoma hivyo vifungu vya katiba walivyokuwa wanavitumia hao watu kusema kuwa baraza zima lazima livunjwe, sikushawishika hata kidogo.

Huu ni mwendelezo wa serikali ileile aliyoiacha Rais Magufuli.

Mambo ya kuvunja baraza zima ya nini? Just keep it simple na kazi ziendelee. Tweaks za hapa na pale, hizo ni sawa.

Sasa, mbona waziri mkuu anaendelea tu na nafasi yake? Hajateuliwa upya kama walivyokuwa wanadai hao wataalamu wa sheria. Hajaapa tena. Au ameapa upya?

Je, ina maana Mama Samia kaanza utawala wake kwa kuvunja katiba?
Kwani Waziri Mkuu aliapa kwa Rais au aliapa kwa Magufuli? Na akiapa upya ataapa kwa Rais au ataapa kwa Samia? Na je Magufuli alikuwa Rais halali? Na je Samia ni Rais Halali?
 
Siku zote ni lazima kuwe na ukimya kwanza ili sheria itungwe kutatua tatizo.
Always remember this: Society changes faster than the law.
Mkuu kwanini kuwe na ukimya kwanza?
Bunge la JMT lilianza kufanya kazi mwaka gani?
Kwa miaka yote hiyo lukuki tangu Bunge lianze kufanya kazi, ni kwanini hawakwenda deep na kuona kwamba Kuna haja ya kuweka vizuri vifungu vya Katiba ya JMT katika suala ambalo litahusu nini hatima ya Baraza la Mawaziri endapo rais atafariki akiwa madarakani?
 
Binafsi wamefanya makosa yanayotokana na kukosea katika kudhania (false assumptions). Wao katika kumuacha Rais aendelee na baraza lile la Magufuli wamedhania kuwa Katiba inatofautisha Rais anayeshika madaraka kufuatia uchaguzi na Rais anayeshika madaraka kufuatia kuondoka kwa mtangulizi wake kwa sababu za kikatiba (kujiuzulu, kifo au impeachment). Kwamba, Rais anayeshinda uchaguzi anafuata utaratibu huu akiingia madarakani na anayeingia kufuatia hizo sababu nyingine anafuata utaratibu mwingine. Binafsi siamini huku ni kudhania kwa usahihi. Utaratibu wetu tangu zamani ni kuwa siku Rais mpya anapoapa tu Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika. Siku WAziri Mkuu akijiuzulu au Rais akimtengua na Baraza linaondoka (kama ilivyotokea kwa Lowassa).

Ni kosa pia limetokana na kuwa hatujawahi kupitia njia hii; ya Rais kufa akiwa madarakani.

Kwani watunga sheria wetu hawakuona au kufikiria kuwa ipo possibility ya rais kufa akiwa madarakani?
Daima kifo kipo!
 
Opinion ya TLS ilikua sahihi.

Samia hajavunja katiba ana discretion ya kuendelea na aliowakuta au ateue wapya.

Ila sasa kuna Lacunae kwa maana kwamba hakuna Ibara inayotoa utaratibu wa mazingira ya kinachopaswa kufanyika kama akiopt kuendelea nao, wala hakuna sheria iliyotoa muongozo katika hilo pia.
Hata ulichoongeaa unakijua kweli?
TLS walitoa waraka wakitaka raisi avunje Baraza kwa kujibu wa katiba inavyosema, raisi hajavunja baraza, ndio mleta uzi akasema kutokana na baraza kutovunjwa je Samia kavunja katiba?
 
Binafsi wamefanya makosa yanayotokana na kukosea katika kudhania (false assumptions). Wao katika kumuacha Rais aendelee na baraza lile la Magufuli wamedhania kuwa Katiba inatofautisha Rais anayeshika madaraka kufuatia uchaguzi na Rais anayeshika madaraka kufuatia kuondoka kwa mtangulizi wake kwa sababu za kikatiba (kujiuzulu, kifo au impeachment). Kwamba, Rais anayeshinda uchaguzi anafuata utaratibu huu akiingia madarakani na anayeingia kufuatia hizo sababu nyingine anafuata utaratibu mwingine. Binafsi siamini huku ni kudhania kwa usahihi. Utaratibu wetu tangu zamani ni kuwa siku Rais mpya anapoapa tu Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika. Siku WAziri Mkuu akijiuzulu au Rais akimtengua na Baraza linaondoka (kama ilivyotokea kwa Lowassa).

Ni kosa pia limetokana na kuwa hatujawahi kupitia njia hii; ya Rais kufa akiwa madarakani.
Mkuu uko sahihi Sana...kosa limetendeka na mbaya zaidi Ag ndo anaendeleza kumdanganya rais
 
Haogopi wala hatoogopa. Keshawaambia hao wanaoota 2025 wanyamaze ila kakosea kidogo kwenye umakamu, wote 2 wachumi. Angalau angeteua waziri aliyebobea katika mambo ya mazingira maana ni muhimu sana. Kuna hili suala la mabadiliko ya climate change ni very important kwa maendeleo ya Taifa lolote duniani. Tabia nchi isipodhibitiwa inasababisha madhara kama ukame, mafuriko, joto kali n.k
Anapiga beat Yaani anauma na kupuliza
 
Hata ulichoongeaa unakijua kweli?
TLS walitoa waraka wakitaka raisi avunje Baraza kwa kujibu wa katiba inavyosema, raisi hajavunja baraza, ndio mleta uzi akasema kutokana na baraza kutovunjwa je Samia kavunja katiba?
Wewe una elimu ya sheria??

Maana nisiwe napoteza muda kujadiliana mambo ya kitaaluma na layman.
 
Mkuu kwanini kuwe na ukimya kwanza?
Bunge la JMT lilianza kufanya kazi mwaka gani?
Kwa miaka yote hiyo lukuki tangu Bunge lianze kufanya kazi, ni kwanini hawakwenda deep na kuona kwamba Kuna haja ya kuweka vizuri vifungu vya Katiba ya JMT katika suala ambalo litahusu nini hatima ya Baraza la Mawaziri endapo rais atafariki akiwa madarakani?
Mkuu kitu ambacho lazima tukifahamu ni kwamba jamii siku zote huwa inbadilika kwa haraka kuliko sheria. Sheria kazi yake ni kuja kusaidia kurekebisha matatizo ya kijamii ambayo tayari yameshatokea. Hivyo baada ya hili tatizo tutegemee kuona miongozo na kanuni mbalimbali zikitengenezwa ili kulikabili vizuri endapo litatokea tena. Hii ndiyo mara ya kwanza JMT imekutana na kifo cha Raisi aliyeko madarakani.

Japo, naomba kukubaliana na wewe kabisa kwamba waandishi wetu wa katiba na sheria hawakuumiza kichwa sana kujaribu kufikiria na kusema dhahiri nini utakuwa mustakabali wa Baraza la Mawaziri endapo, Raisi atafariki. Maana ikumbukwe nchini Tanzania mawaziri hufanya kazi kwa matakwa ya Raisi (At the pleasure of the President), pia hula kiapo cha Utii kwa Raisi (An oath of allegiance to the President) na kwa Jamhuri (An oath of allegiance to the Republic). Hivyo hili lazima liangaliwe vizuri...

Ukimya huu uko hata ndani ya Kanuni za kudumu za bunge (Standing Orders), ambapo hakuna utaratibu unaelezea jinsi ya kumpitisha makamu wa Raisi mpya, endapo nafasi ya makamu wa Raisi iko wazi kwasababu za kifo au makamu wa Raisi kuwa Raisi. Juzi nilitazama bunge na spika akakiri dhahiri kwamba hawana utaratibu hivyo watatumia uzoefu uliofanyika na Bunge baada ya kifo cha Dr Omar Ali Juma. Lakini kanuni za Bunge ziko kimya kuhusu hilo.

Ni mifano iko mingi sanaaaa...........
 
Binafsi wamefanya makosa yanayotokana na kukosea katika kudhania (false assumptions). Wao katika kumuacha Rais aendelee na baraza lile la Magufuli wamedhania kuwa Katiba inatofautisha Rais anayeshika madaraka kufuatia uchaguzi na Rais anayeshika madaraka kufuatia kuondoka kwa mtangulizi wake kwa sababu za kikatiba (kujiuzulu, kifo au impeachment). Kwamba, Rais anayeshinda uchaguzi anafuata utaratibu huu akiingia madarakani na anayeingia kufuatia hizo sababu nyingine anafuata utaratibu mwingine. Binafsi siamini huku ni kudhania kwa usahihi. Utaratibu wetu tangu zamani ni kuwa siku Rais mpya anapoapa tu Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika. Siku WAziri Mkuu akijiuzulu au Rais akimtengua na Baraza linaondoka (kama ilivyotokea kwa Lowassa).

Ni kosa pia limetokana na kuwa hatujawahi kupitia njia hii; ya Rais kufa akiwa madarakani.

..naamini uko sahihi.

..lakini bado tuko ktk "tanzania ya magufuli" ambako tunaangalia ushauri unatoka kwa nani, kabla ya kuukubali, au kuukataa.

..ushauri huu haukuzingatiwa kwasababu ulitolewa na chombo ambacho watawala hawakipendi.
 
Back
Top Bottom