Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,119
- 136,866
Mimi ni mtu ninayefuata falsafa ya ‘keep it simple’.
Sikuona sababu yoyote ile ya Rais Samia kulivunja baraza lote la mawaziri na kulisuka upya.
Mabadiliko madogo kama aliyoyafanya ni ya kawaida na niliyategemea.
Lakini tuliambiwa na watu mbalimbali kuwa eti baada ya Rais Magufuli kufariki, basi kwa mujibu wa katiba baraza nalo linavunjika na waziri mkuu anakoma kuwa waziri mkuu.
Nilipovisoma hivyo vifungu vya katiba walivyokuwa wanavitumia hao watu kusema kuwa baraza zima lazima livunjwe, sikushawishika hata kidogo.
Huu ni mwendelezo wa serikali ileile aliyoiacha Rais Magufuli.
Mambo ya kuvunja baraza zima ya nini? Just keep it simple na kazi ziendelee. Tweaks za hapa na pale, hizo ni sawa.
Sasa, mbona waziri mkuu anaendelea tu na nafasi yake? Hajateuliwa upya kama walivyokuwa wanadai hao wataalamu wa sheria. Hajaapa tena. Au ameapa upya?
Je, ina maana Mama Samia kaanza utawala wake kwa kuvunja katiba?