IN Tanzania thamani ya kifo ni 8 MILLION

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Kila kifo Gongo la Mboto fidia Sh.8.5m

Na Muhibu Said
3rd March 2011

Kila aliyekufa kutokana na milipuko ya mabomu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Serikali italipa fidia ya Sh. milioni 8.5.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, ambaye ilizitaka familia 29 zilizofiwa na ndugu kutokana na mabomu hayo kuteua msimamizi wa mirathi ya marehemu, kwani iko tayari sasa kuilipa kila familia Sh. milioni 8.5 kama kifuta machozi.

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, alipozungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupokelea misaada kwa waathirika cha Kamati ya Maafa ya Mkoa jana.

Alisema kwa sasa kinachotakiwa kufanywa na familia za marehemu, ni kufungua mirathi mahakamani ili kumteua haraka msimamizi wa mirathi, ambaye ndiye atakayelipwa fedha hizo kwa niaba ya warithi.

Sadiki alisema utaratibu huo ndio unaostahili kufuatwa, kwani utasaidia kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza ndani ya familia iwapo fedha hizo zitatolewa kiholela.

Alisema hadi kufikia jana, watu waliothibitika kufariki dunia kutokana tukio hilo, ni 29 akiwamo aliyefia nyumbani Kinyerezi wiki iliyopita na mwingine aliyefia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) juzi.

source: :: IPPMEDIA
 
Ambayo ni sawa na 348 mil.

Kwa hiyo serikali haitatumia zaidi ya Bil 1 kulipa fidia ya vifo na mali.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, ambaye ilizitaka familia 29 zilizofiwa na ndugu kutokana na mabomu hayo kuteua msimamizi wa mirathi ya marehemu, kwani iko tayari sasa kuilipa kila familia Sh. milioni 8.5 kama kifuta machozi.

Mi sijaelewa!

Yaani familia ina watu 6, wamekufa watu wa5 so nae atalipwa mil 8.5 au?

Halafu hilo neno KIFUTA MACHOZI naona kama matusi kwa wafiwa. Taifa Stars walivyofungwa Kombe la Mto Nile kule Egypt walipewa kifuta machozi, waliokufa nao kifuta machozi? Hivi kumpa mtu aliyepoteza mke na watoto wawili Mil 8.5 ndo umemfuta machozi???
 
Ambayo ni sawa na 348 mil.

Kwa hiyo serikali haitatumia zaidi ya Bil 1 kulipa fidia ya vifo na mali.

Mungu ibariki Tanzania.

Kuna Michango mingi sana iliitishwa, wewe binafsi ulichangia kiasi gani? na unataka Serikali ilipe kiasi gani? Tuache kulalamikia kila kitu kinachofanywa na serikali
 
Ambayo ni sawa na 348 mil.

Kwa hiyo serikali haitatumia zaidi ya Bil 1 kulipa fidia ya vifo na mali.

Mungu ibariki Tanzania.

Mi sijaelewa!
Yaani familia ina watu 6, wamekufa watu wa5 so nae atalipwa mil 8.5 au??
Halafu hilo neno KIFUTA MACHOZI naona kama matusi kwa wafiwa. Taifa Stars walivyofungwa Kombe la Mto Nile kule Egypt walipewa kifuta machozi, waliokufa nao kifuta machozi? Hivi kumpa mtu aliyepoteza mke na watoto wawili Mil 8.5 ndo umemfuta machozi???

nimesikia na JKT watajenga nyumba, kwa hiyo hakuna fidia ya pesa kwa mali zingine kama TV, nguo, mafriji majiko nk zilizoteketea na mabomu!

yaani nchi yetu hii, basi tena. inauma sana,
 
Ambayo ni sawa na 348 mil.

Kwa hiyo serikali haitatumia zaidi ya Bil 1 kulipa fidia ya vifo na mali.

Mungu ibariki Tanzania.

Halafu zingatia kwamba kuna wabunge takriban 380 wanapewa mikopo ya milion 90 kila mmoja kununua mashangingi, ambapo serikali inalipia nusu ya huo mkopo. Yaani milioni 45 mara 380 ni bilioni 17!

Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Eti Waliokufa gongo la mboto watapewa milion 8. Walikufa 25. Mawaziri wapo 49 milion 12 wanapokea kila mwezi, milion 8 kama ni baba wa familia itawafanyia nini watoto wake? Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Kidumu chama
 
Nataka kujua walikadiria vipi kupata Mil 8.5 na sio chini au zaidi?
 
Jamani naomba msiniaribie siku kwa mi'bad news ya nchi hii.
kila kukicha ni uozo tuu.
aah! mi nshachoka bana.
 
Hivi hawa wakina Zitto na wenzao walioko humu jamvini mbona mada hizi hawachangiagi? au haziwagusi moja kwa moja nini? Haya ni matusi kwa wafiwa, dhihaka kabisa. Au ndo yale ya waache wafu wawazike wafu wao, jamani hiki ni nini mbona mi sielewi, uwiiii............... nyie wanasiasa, mbona hamtii neno humu??
Halafu zingatia kwamba kuna wabunge takriban 380 wanapewa mikopo ya milion 90 kila mmoja kununua mashangingi, ambapo serikali inalipia nusu ya huo mkopo. Yaani milioni 45 mara 380 ni bilioni 17!

Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Halafu zingatia kwamba kuna wabunge takriban 380 wanapewa mikopo ya milion 90 kila mmoja kununua mashangingi, ambapo serikali inalipia nusu ya huo mkopo. Yaani milioni 45 mara 380 ni bilioni 17!

Kidumu chama cha mapinduzi.

na ndio mana nampenda Godbless Lema amezikataa hizo pesa zao
 
Mi sijaelewa!

Yaani familia ina watu 6, wamekufa watu wa5 so nae atalipwa mil 8.5 au?

Halafu hilo neno KIFUTA MACHOZI naona kama matusi kwa wafiwa. Taifa Stars walivyofungwa Kombe la Mto Nile kule Egypt walipewa kifuta machozi, waliokufa nao kifuta machozi? Hivi kumpa mtu aliyepoteza mke na watoto wawili Mil 8.5 ndo umemfuta machozi???

hakuna samani halili ya uhai wa mwanadamu hivyo serikali hutoa kiasi cha fedha kulingana na uwezo wake. uhai ungekuwa na thamani basi wangelipwa kwa thamani hiyo. labda mtusaidie kukokotoa thamani ya uhai ili uwe mwongozo kwa serikali kuwalipa wahanga mbalimbali hapa nchini na kwingineko duniani
 
Kifo is not worth thamani yeyote ya pesa.

Ifike wakati tutumie njia nyingine kuwafariji wafiwa.
 
Hiyo ni rambi rambi ya serikali. Lazma tutambue kifo cha mtu hakilipwi ila tunawezatoa rambi rambi tu. Naipongeza serikali kwa uamuzi huo kwani hata ingetoa bilioni moja kwa kila familia isingetosha kuondo majonzi kwa wafiwa.
 
Ambayo ni sawa na 348 mil.

Kwa hiyo serikali haitatumia zaidi ya Bil 1 kulipa fidia ya vifo na mali.

Mungu ibariki Tanzania.
Kwa Fisadi hiyo kwake ni sahihi ili ajilinde yeye na familia yake wakapate matibabu nchi za nje, watoto wao wasome shule nzuri za Ulaya....saa ngapi awaze kumlipa mfu ambae anaonekana kama mleta kiwingu kwenye system yao. Mungu Bariki Tanzania na Watanzania wote.
 
Nataka kujua walikadiria vipi kupata Mil 8.5 na sio chini au zaidi?

Uozo, Uchakachuaji,kila kitu dili bongo. Wananchi wapigwe mabomu na wanjeshi hadi kuuawa ishakuwa dili.
Tegemea vifo hewa, nyumba hewa kadhaa.
Kifuta machozi..... Good Lord!
 
KUFUTA MACHOZI HICHO HAKITOSHELEZI KUYAFUTA MACHOZI YA WAFIWA.
hebu mfano amekufa baba na ameacha mama asie na kazi wala hajajiajiri na ana watoto wadogo kama wa3,atawasomesha vp atawalea vp kwa hiyo mil8.hata akifanya biashara still bado haitafanikisha lolote mbele.
 
Back
Top Bottom