In response to the thread maelfu wamiminika DUCE...

kibavu

Senior Member
Oct 15, 2008
136
82
In response to the thread maelfu wamiminika DUCE... https://www.jamiiforums.com/nafasi-za-kazi-na-tenda/365611-maelfu-wamiminika-duce.html Katika thread ile kuna mchangiaji anasema, nanukuu “Sawa viwanda hakuna,na serikali haina mpango wa kujenga viwanda.Vijana wanalalamika kuhusu ajira,Lakini ni lazima serikali iwatafutie vijana wote ajira?.Nini maana ya usomi wenu,kama hamuwezi kuunganisha mitaji midogo na kutengeneza small enterprises,kweli wanaojiita wasomi wa Tanzania ni janga kuu kwa taifa.”
Ni kweli kwamba hili ni tatizo kwa vijana tunaohitimu ngazi mbali mbali za elimu hapa nchini. Nami Hoja yangu itajengwa katika changamoto iliyoletwa na mchangiaji huyu. Binafsi nadhani mfumo wetu wa elimu ni tatizo katika ‘contents (mada za masomo husika), instruction (ufundishaji) na evaluation (upande wa mitihani). Unafundishwa kuambiwa jitegemee kwani siku ya mtihani
Kwa mfano, Unafanya mtihani wa darasa la nne peke yako....unafaulu
Darasa la saba peke yako....unafaulu
Form TWO peke yako....nao unafaulu
Form FOUR peke yako
Form six peke yako...na huu pia unafaulu sana tu.
Na unapofaulu hii mitihani uliyoifanya peke yako pengine unapata zawadi peke yako kwa kuweza kufaulu zaidi ya wenzako. Unakwenda chuo karibu asilimia 80 ya masomo unafanya peke yako ukiacha asilimia kama 20 ambayo mnafanya presentation na group assignment. Bila kujali yaliyomo (contents) kwenye masomo hayo huyu mwanafunzi hata akiwa amesoma Bcom au Business Administration/Management zikibeba kozi kibao za ujasiriamali bado anaweza akashindwa kufanya biashara katika ‘joint venture’ kwakuwa akili yake na elimu yake imemwandaa kuwa mbinafsi zaidi kwan katika sehemu kubwa ya maisha yake kielimu ameandaliwa kuwa ‘mchoyo’ kwan amekua akipimwa na kuheshimiwa anapofanikiwa kufaulu peke yake. Na sifa ya mchoyo ni kutokua tayari kushea na wenzake ili kupata mafanikio ya pamoja, hivyo unakuta wengi wanajiandaa kufanya kazi au biashara peke yao ili kuwaonesha watu ‘what they can achieve/what they have achieved individually.
Pia mfumo huu wa elimu unajenga hali ya watu kuamini wanaweza kufanikiwa kwa kufanya mambo kiupekee na kupenda sifa za binafsi zaidi. Unakuta mtu anashindwa hata kushirikiana na kaka au dada yake katika biashara kisa kila mmoja anajaribu kumuonesha mwenzake kwamba yeye ni zaidi. Lakini ukiangalia historia ya kukua na kufanikiwa kwa ubepari utaona kwamba ni pale ilipofikia hatua ya ukiritimba (monopoly capitalism) ndipo mafanikio yalipokuwa makubwa zaidi i.e. kwa wale mliosoma political economy na history hapa nazungumzia ile transition from competitive capitalism kwenda kwenye monopoly capitalism pamoja na merging of capital. Hii ilisaidia kupunguza ushindani na kuongeza faida kwa wamiliki wa biashara na viwanda. Wakati huku kwetu unakuta ndugu wawili wanamiliki daladala aina ya HIACE kwanini wasiunganishe nguvu wakanunua Coaster? Jibu ni ubinafsi na umimi. Vivyo hivyo kwa wasomi, hawapo tayari kuunganisha mawazo kila mtu anataka kum-surprise mwenzake kwa mafanikio.
Tunahitaji mapinduzi ya kifikra ili tuweze kuondoka hapa tulipo na kusonga mbele ‘we need transformation in order progress’
 
In response to the thread maelfu wamiminika DUCE... https://www.jamiiforums.com/nafasi-za-kazi-na-tenda/365611-maelfu-wamiminika-duce.html Katika thread ile kuna mchangiaji anasema, nanukuu ¡°Sawa viwanda hakuna,na serikali haina mpango wa kujenga viwanda.Vijana wanalalamika kuhusu ajira,Lakini ni lazima serikali iwatafutie vijana wote ajira?.Nini maana ya usomi wenu,kama hamuwezi kuunganisha mitaji midogo na kutengeneza small enterprises,kweli wanaojiita wasomi wa Tanzania ni janga kuu kwa taifa.¡± Ni kweli kwamba hili ni tatizo kwa vijana tunaohitimu ngazi mbali mbali za elimu hapa nchini. Nami Hoja yangu itajengwa katika changamoto iliyoletwa na mchangiaji huyu. Binafsi nadhani mfumo wetu wa elimu ni tatizo katika ¡®contents (mada za masomo husika), instruction (ufundishaji) na evaluation (upande wa mitihani). Unafundishwa kuambiwa jitegemee kwani siku ya mtihaniKwa mfano, Unafanya mtihani wa darasa la nne peke yako....unafauluDarasa la saba peke yako....unafauluForm TWO peke yako....nao unafauluForm FOUR peke yako Form six peke yako...na huu pia unafaulu sana tu. Na unapofaulu hii mitihani uliyoifanya peke yako pengine unapata zawadi peke yako kwa kuweza kufaulu zaidi ya wenzako. Unakwenda chuo karibu asilimia 80 ya masomo unafanya peke yako ukiacha asilimia kama 20 ambayo mnafanya presentation na group assignment. Bila kujali yaliyomo (contents) kwenye masomo hayo huyu mwanafunzi hata akiwa amesoma Bcom au Business Administration/Management zikibeba kozi kibao za ujasiriamali bado anaweza akashindwa kufanya biashara katika ¡®joint venture¡¯ kwakuwa akili yake na elimu yake imemwandaa kuwa mbinafsi zaidi kwan katika sehemu kubwa ya maisha yake kielimu ameandaliwa kuwa ¡®mchoyo¡¯ kwan amekua akipimwa na kuheshimiwa anapofanikiwa kufaulu peke yake. Na sifa ya mchoyo ni kutokua tayari kushea na wenzake ili kupata mafanikio ya pamoja, hivyo unakuta wengi wanajiandaa kufanya kazi au biashara peke yao ili kuwaonesha watu ¡®what they can achieve/what they have achieved individually. Pia mfumo huu wa elimu unajenga hali ya watu kuamini wanaweza kufanikiwa kwa kufanya mambo kiupekee na kupenda sifa za binafsi zaidi. Unakuta mtu anashindwa hata kushirikiana na kaka au dada yake katika biashara kisa kila mmoja anajaribu kumuonesha mwenzake kwamba yeye ni zaidi. Lakini ukiangalia historia ya kukua na kufanikiwa kwa ubepari utaona kwamba ni pale ilipofikia hatua ya ukiritimba (monopoly capitalism) ndipo mafanikio yalipokuwa makubwa zaidi i.e. kwa wale mliosoma political economy na history hapa nazungumzia ile transition from competitive capitalism kwenda kwenye monopoly capitalism pamoja na merging of capital. Hii ilisaidia kupunguza ushindani na kuongeza faida kwa wamiliki wa biashara na viwanda. Wakati huku kwetu unakuta ndugu wawili wanamiliki daladala aina ya HIACE kwanini wasiunganishe nguvu wakanunua Coaster? Jibu ni ubinafsi na umimi. Vivyo hivyo kwa wasomi, hawapo tayari kuunganisha mawazo kila mtu anataka kum-surprise mwenzake kwa mafanikio. Tunahitaji mapinduzi ya kifikra ili tuweze kuondoka hapa tulipo na kusonga mbele ¡®we need transformation in order progress¡¯
Tatizo sio vijana bali ni mfumo mzima wa elimu wanayopata haikidhi haja ya kujiajiri! Hivyo usione ajabu kuona vijana wanahangaika mtaa hadi mtaa kutafuta kazi badala ya kutafuta fedha!
 
Back
Top Bottom