In Memoriam: Siku Saba za Maombolezo ya Mzee R. M. Kawawa

Jamani sio kwamba hamna kufanya kazi, kazi zitaendelea kama kawaida. Maombolezo ya siku 7 ni recognition kwamba kama taifa tukumbwa na msiba mzito e.g. bendera nusu mlingoti n.k.
 
Kuna kutoeleweka vizuri kuhusu hizo siku saba. Kama hakuna kazi tuambiane mapema tukatoe hela za kutosha ATM tusije tukafa njaa. Nakumbuka wakati wa msiba wa Mwalimu JKN, sherehe zote zilipigwa marufuku katika siku za maombolezo, sasa sijui hatima ya harusi ya mpwa wangu weekend hii. Kama na sasa sherehe zimesimamishwa, tuelezane basi nikavunje kamati ya sherehe, ingawa ndoa itakuwepo.
 
Tunamsubiri mtabiri wetu yahaya atueleze kama hii nayo ni kafara nyingine au kafara ni kafiri tu.
 
Kazi kama dawa na siku saba za maombolezo haina maana hakuna kufanya kazi bali bendera katika ofisi zote za chama na serikali zitakuwa nusu mlingoti kwa siku hizo saba
 
nimesikia kazi hakuna kwa siku saba

Maombolezi siku saba, haina maana kwamba hakuna kazi siku saba. Twendeni kuchapa kazi na tumuenzi RMK kwa vitendo.

Kazi kama dawa na siku saba za maombolezo haina maana hakuna kufanya kazi bali bendera katika ofisi zote za chama na serikali zitakuwa nusu mlingoti kwa siku hizo saba
MImi napendekeza tukae nyumbani, tutawezaje kuomboleza tuko kazini bwana???
 
Jamani Mourning period kazi ni kama ada.... ni kutoa heshima tu lakini sio MAPUMZIKO... Siku saba kwa mzee kawawa sawasawa ... Mzee wetu huyu ni katika viongozi waadilifu na wafuasi wa kweli wa itikadi ya stahili ya heshima ya kila binadamu kama ilivyoa inishwa katika katiba ya nchi.... Kama Mwalimu, Mzee Kawawa hakuwa mlafi... yule pale amekufa anakula pension tu bila "vijisenti". RIP simba wa Vita....
 
Muda na wakati wake ulifika kwa mzee wetu na pia historia imejiandika kwake na tena yeye kama shujaa wa taifa letu Tanzania ni lazima watu wote tuone kuwa ni mchango mkubwa sana
 
siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things

Nadhani wewe unafananisha na "Public holidays".Maombolezo sio kwamba hautakwenda kazini.Kazi kama kawaida!Ni sahihi kabisa na sidhani kuna haja ya kufananisha na nchi tajiri kwenye hili suala.Kawawa ni mmoja and will remain the only Kawawa(RIP mzee).Kama alivyokuwa Nyerere!
 
Rais kasema bendera itapepea nusu mlingoti katika siku zote saba za maombolezo. Hii haina maana watu watapumzika majumbani.
 
siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things

Tovuti,
Acha mambo yako na nchi zako tajiri bana, kumbuka Tanganyika ni nchi tajiri pi, utajiri wetu ni kuwa na hazina ya watu mahiri kama mzee wetu Simba wa Vita. Kwa hiyo siku 7 ni sahihi kabisaa.
AMANI NA HEPI NEW YEAR
IDUMU JF.
 
Mimi nadhani hakuna jipya hapa.Hili suala la kuomboleza siku 7 na bendera nusu mlingoti ni jmabo la kawaida kwa viongozi wetu hapa nchini.Why are we discussing this issue?
 
RIP mzee kawawa, naombeni kuuliza hivi ni sahihi kupiga king'ora cha polisi Hospitalini jamni????????????????
 
Kwa wale wenye uwezo wa kuona tbc ,imeanza kuonyesha historia ya mzee wetu kawawa na bday zak alizokuwa akifurahia na wajukuu na wanawe,...kwa kweli mungu amlaze mahali pema,kuna sehemu amenigusa amabayo hata nyerere akuwahi kusema hilo
alipoamua kuomba radhi kwa watanzania wote aliowafanyia vibaya bila kujua ama kwa sababu ya mazingira ya kazi,...
Eemola mlaze pema peponi ,leo hii wakuu wa nchi wa cchache wanakufa wakijua uchafu waliotutendea bila hata kuomba samahani,....nawatakia pole wafiwa jf n familly tuko nyuma yenu

bwana ametoa bwana ametwaa
 
Ila katika maombolezo ya Mwl Nyerere redio nyingi zilitumia muda mwingi kutumbuiza nyimbo za maombolezo; maana yake baadhi kama siyo zote ziliathirika kimapato kwa kutorusha matangazo mengi ya biashara kama kawaida. Hizi siku saba itakuwa vivyo hivyo? Na waliopo kwenye contracts za burudani kuanzia leo (mkesha) hawataathirika na maombolezo. Mwenye kujua hili tafadhali.
 
Back
Top Bottom