In Memoriam: Siku Saba za Maombolezo ya Mzee R. M. Kawawa

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Jk ametangaza rasmi siku saba za maombolezo ya kitaifa kutokana na kifo cha Mzee kawawa, na bendera nchi nzima zitapepea nusu mlingoti
 
Kama hii ni kweli, basi ni jambo jema na la busara sana.

Mkuu, tumebadilisha title ya topic yako na kuwa Rais badala ya JK. Natumaini unakubaliana na uongozi wa JF kubadilisha title hiyo!
 
Bwana ametoa na bwana Ametwaa.
Mungu amlaze pema peponi. amen.
Kawawa atakumbukwa Daima kwa mchango wake katika ujenzi wa taifa hili. ana historia yake hapa Tanzania
 
Kama hii ni kweli, basi ni jambo jema na la busara sana.

Mkuu, tumebadilisha title ya topic yako na kuwa Rais badala ya JK. Natumaini unakubaliana na uongozi wa JF kubadilisha title hiyo!

poa hamna noma, kurekebishana ni muhimu
 
Kweli huyu alikuwa simba wa Vita, nakumbuka sana enzi za utoto wangu kulikuwa na story za kuchekesha sana kuhusu HUYU kamanda wa VITA, nakumbuka siku moja tukiwa safarini na Baba yangu, gari lilikwama kwenye matope, ilikuwa ni landlover 109, mara nikamsikia Dingi anasema ngoja niweke KAWAWA, litatoka sasa hivi, pale kwenye gia kuna gia ndefu na kale kafupi, kale kafupi ndo kakiitwa KAWAWA na kweli alipoweka kale, gari ilikuwa very powerful na ikachomoka pale kwenye MATOPE, so Kawawa Tutamkumbuka sana tena sana kwa mengi tu, Mungu ailaze roho yake Mahala pema peponi
 
siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things
 
ni vema ametumia busara sana na kama taifa tunatakiwa kuombeleza kweli kifo cha mzee wetu
 
siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things
mkuu maombolezo sidhani kama hakuna kufanya kazi!! kazi itaendelea but mabo kama bendera kupepea nusu mlingoti no siku saba!!!

anastahili hiyo heshma mzee K!! R.I.P
 
Acha wafu wazike wafu wao. Si tutakufa njaa tukiomboleza siku zote hizi au kuna kipunga nchi nzima?
 
leo nimeamini kama kweli watz ni wavivu na hawapendi kazi, jamani siku 7 zote, na hakuna anayelalamika, na nchi yetu masikini ya mwisho
 
mkuu maombolezo sidhani kama hakuna kufanya kazi!! kazi itaendelea but mabo kama bendera kupepea nusu mlingoti no siku saba!!!

anastahili hiyo heshma mzee K!! R.I.P

Mwenye maelezo zaidi ya uhakika ofisi/kazi zitaendelea kama kawaida au itakuwaje? Sijaelewa
 
Kweli huyu alikuwa simba wa Vita, nakumbuka sana enzi za utoto wangu kulikuwa na story za kuchekesha sana kuhusu HUYU kamanda wa VITA, nakumbuka siku moja tukiwa safarini na Baba yangu, gari lilikwama kwenye matope, ilikuwa ni landlover 109, mara nikamsikia Dingi anasema ngoja niweke KAWAWA, litatoka sasa hivi, pale kwenye gia kuna gia ndefu na kale kafupi, kale kafupi ndo kakiitwa KAWAWA na kweli alipoweka kale, gari ilikuwa very powerful na ikachomoka pale kwenye MATOPE, so Kawawa Tutamkumbuka sana tena sana kwa mengi tu, Mungu ailaze roho yake Mahala pema peponi

Mkuu umenikumbusha hii story, zipo nyingi tu zinazowahusu hawa wawili Nyerere na Kawawa, kifupi sisi wakati huo tukiwa watoto wazazi wetu walituambia story nyingi mno tena za kuchekesha ila zilionyesha Upendo wa hawa viongozi wetu yaani mfano ile ya Mwalimu na Kawawa walivyosafiri pamoja wakati wa kwenda kuhutubia Umoja wa Mataifa.... hata nyimbo pia kama huu - nyerere yupoo nyerere yupoo ukiona kundi la siasa ......kawawa yupooo etc...hapa nilikuwa darasa la kwanza

Au ule wa jenga jenga taifa lakoo usinione napiga domo NAJENGAA nalijenga taifa langu najengaa...

Nchi yoyote duniani lazima itangulize utaifa kwanza, na lazima watoto wafundiswe kikamilifu kulipena taifa lao, tunaandika haya sababu tunakumbuka ingawa tulikuwa watoto wa miaka 7 tu.
 
Jk ametangaza rasmi siku saba za maombolezo ya kitaifa kutokana na kifo cha Mzee kawawa, na bendera nchi nzima zitapepea nusu mlingoti

siku saba??? nyingi sana, atleast wangefanya siku 3, nchi tajiri na zilizoendelea they dont do these things

mkuu maombolezo sidhani kama hakuna kufanya kazi!! kazi itaendelea but mabo kama bendera kupepea nusu mlingoti no siku saba!!!

anastahili hiyo heshma mzee K!! R.I.P
Waliosikia na kuelewa, watuweke sawa ktk hili, kuna kazi au hakuna kazi??!!
 
leo nimeamini kama kweli watz ni wavivu na hawapendi kazi, jamani siku 7 zote, na hakuna anayelalamika, na nchi yetu masikini ya mwisho

Kazi kweli kweli, hapa hata sijui unaanzia wapi kuelimisha...
 
Siku ya maziko yake inatakiwa tukae nyumbani ili tuomboleze kuondokewa na mzee wetu. Kama Nyerere alivyokuwa huyu mzee alikuwa muadilifu kweli kweli. Hana chembe ya ufisadi wala tamaa ya madaraka. Kama mwenzake alikaa kijijini Madale au Kiluvya akijishughulisha na kilimo.

Tunaomba Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu mzee RMK mahali pema peponi Amin.

RIP mzee RMK
 
Maombolezi siku saba, haina maana kwamba hakuna kazi siku saba. Twendeni kuchapa kazi na tumuenzi RMK kwa vitendo.
 
Kazi kweli kweli, hapa hata sijui unaanzia wapi kuelimisha...
jamani hata baba wa taifa alipofariki siku kadhaa zilitengwa kwa maombolezo lakini hatukukaa nyumbani, kama nakumbuka sku ya mazishi no hapakuwa na shughuli zozote (shule au kazi)

mtazamo wangu hatutafanya kazi siku ya mazishi BUT wacha tusikilizie taarifa rasmi!!!
 
Back
Top Bottom