Important Message from the U.S. Embassy in Dar es Salaam

Tegemea KOVA kuja kukanusha Leo kwenye luninga,,,si hujamuona kitambo kwenye runinga yako?????WAIT,,,,,
 
hivi ule utaratibu uliokuwepo wa kila siku jioni mapolisi wanatawanywa jioni mitaani kwa ajili ya doria bado upo?...........maana kule mitaa ya O'bay, Upanga Seaview ndio kabisaa vibaka walikuwa hawagusi kule.......
Patrol wanazozifanya siku hizi ni za kutafuta watu wa kuwatoa mshiko. Si unaona wale jamaa wa 'tigo' wanavyorandaranda kutafutra daladala zinazokatisha njia badala ya kuwatafuta majambazi!
 
AIBU AIBU AIBU kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wiki kama tatu zilizopita jamaa zangu 3 walitoka russian culture centre wakitembea kwa miguu kueleke gymkhana kama saa moja jioni. Walivamiwa na vibaka kama 10 waliojificha vichakani. vibaka hao walifanikiwa
kuwanyang'anya vitu mbali mbali . walipokwenda kituo cha polisi kilicho karibu na tukio , walistaajabu kusikia polisi wakiwadiscribe
baadhi ya wahuni hao kama vile nao walishuhudia tukio hilo. na uchunguzi mdogo tuliofanya ni kwamba vibaka hao baada ya kupora wanawapoza polisi kwa pesa na au simu.
BANDARI SALAMA SI SALAMA TENA
 
[hivi ule utaratibu uliokuwepo wa kila siku jioni mapolisi wanatawanywa jioni mitaani kwa ajili ya doria bado upo?...........maana kule mitaa ya O'bay, Upanga Seaview ndio kabisaa vibaka walikuwa hawagusi kule.......]
sasa hivi wameacha wamekazania ulinzi shirikishi na wanaofanya huo ulinzi wengi ni vibaka wao sijui wanalipwa mshahara kwa kazi gani
navyoelewa mimi ulinzi shirikishi ni pamoja na kutoa taarifa za uhalifu,mhalifu au unapoona mienendo inayotia mashaka kwa polisi na sio kuwatoza pesa wananchi kwa kisingizio cha ulinzi shirikishi mitaa yetu mingi taa za barabarani haziwaki na ukienda kutoa taarifa polisi ya uhalifu itabidi ugharamikie usafiri pamoja na kununua karatasi bado hujaombwa rushwa nchi kila kitu kinafanywa siasa
 
Man mbona nashindwa kukuelewa? wizi ni wizi tu, kama wao hawaruki ukuta na kuiba kama ulivyosema wanakupiga risasi mtaani hausomi habari mbalimbali tafuta murder rate huko uone kuna sehemu nyingine watu wanaopigwa risasi tu hadi kufa ni zaidi ya 40 kwa mwezi, na hata wewe ukibahatika labda kupelekwa New York kikazi mwenyeji wako atakawambia kuna sehemu usiende wanaita no go Areas!

mkuu hapo red ndio asili ya neno Negroes?
 
Vibaka wanawalia mingo sana sana wageni (wazungu) sehemu wanazopendelea . Na ndio maana hakutaja TANDIKA, MBAGALA ,KIGOGO wala SINZA etc...... hata wewe ukienda huko new york kuna sehemu utashauriwa usiende unaweza ukaibiwa , kuuliwa etc. Na pia kuna sehemu utaambiwa usiende kwani unaweza ukaonekana mwizi
 
Aisee Dar siku hizi imekuwa hatari kabisa hata kwa mwananchi.
Magari yakifika kwenye intersection yanapotakiwa kufuata traffic lights hayafuati taa kama inavyopaswa, dereva wa kila upande wanajieendea tu, yaani hatari sana haswa usiku inabidi kuendesha kwa uangalifu sana, defensive driving
 
Kwani ni uongo sasa, na polisi kazi yao kubwa hapa ni kuratibu shughuli za kuzuia mabadiliko
 
Hebu tuletee hizo reports au links zenye kuonyesha watu 40 kwa mwezi wamekufa NY kwa kupigwa risasi !!

Man mbona nashindwa kukuelewa? wizi ni wizi tu, kama wao hawaruki ukuta na kuiba kama ulivyosema wanakupiga risasi mtaani hausomi habari mbalimbali tafuta murder rate huko uone kuna sehemu nyingine watu wanaopigwa risasi tu hadi kufa ni zaidi ya 40 kwa mwezi, na hata wewe ukibahatika labda kupelekwa New York kikazi mwenyeji wako atakawambia kuna sehemu usiende wanaita no go Areas!
 
...Mhhh! Dar tambarare!!!!...polisi magamba wako busy kuwawinda viongozi na wafuasi wa CDM huku ujambazi ukizidi kushamiri!!!!

Mkuu BAK, umenena. Polisi tunao, kazi yao ya msingi ni kulinda raia awe wa local or foreign na mali zao but!!!!!! Wanawezesha wahalifu kutekeleza majukumu ya kihalifu, wanajua kabisa uhalifu waliosema ubalozi na hata ukiwauliza baadhi ya watuhumiwa watakutajia!!!! Wanajua tena siku hizi kuna magari yanajifanya yanabeba abiria vituoni ila wanaenda kuwafanyia uhalifu wa wizi wa mali zao, kubakwa etc but hakuna action, even a press conference/release kukemea maovu haya na kutahadharisha umma!!!! Kumbe hawasemi, pengine niseme wana hisa kwa wahalifu hao!!! Kazi yao kubwa mauaji!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom