Immigration, hebu ingieni Kampala international university

Puma yetu

Senior Member
Sep 23, 2016
111
125
Kile chuo kuna wanigeria wamejaa kama njugu, tunasikia kua wanaombwa kuja kufundisha wanafunzi wa diploma masomo ya Afya lakini wanafundisha wanafunzi wa shahada.Wengine wanaenda kwa mafunzo ya vitendo lakini wanazamia kazini moja kwa moja.

Sijui kiutaratibu serikali inaruhusu vyuo vyetu kuajiri wafanyakazi wa kigeni kiasi gani lakini pale wageni wamejaa utafikiri ni Nigeria hasa kwa kozi za sayansi.Labda kama ni chuo cha wageni nao wanaendesha kama vile wako kwao, lakini nijuavyo mimi wale ni wawekezaji kwahiyo kwa namna yeyote ile watanzania wanatakiwa kunufaika kwa ajira za uwekezaji huo.Yaani pesa walipe watanzania, halafu zikaliwe nje! Why?

Kuna vijana wangu ambao niliwapeleka chuoni hapo mwaka juzi, kila mara wamekua wakilalamika juu ya taratibu za ufundishaji wa walimu hao kutokana na uwezo mdogo wa kujibu hata maswali pindi wanapoulizwa darasani. Nafikiri ndio hiyo sababu ya kuja kwa gia ya kufundisha stashahada lakini hupangiwa kufundisha shahada.

Kujazana kwa raia hao wa kigeni sijui ni taratibu gani za kisheria zimezingatiwa hasa kwa kipindi hiki ambacho kuna vijana wengi wa kitanzania wanamaliza vyuo vikuu hawana ajira, wengine hatujui huenda tushafungulia soko huria na nchi hiyo.


UHAMIAJI kama mmekuta madadu mengi kuasi hicho kwa makampuni ya Manji nina imani pale Kampala mtachoka kabisa kama hamkushiriki kwa namna yeyote kuruhusu hao watu kujazana kiasi hicho tena kwa kazi ya ualimu tu.
 
Povu lote la nini???.....au nawewe ni miongoni mwa wale waliofukuzwa chuo kwa makosa ya udanganyifu wa mitihani.....
 
Wana Nigeria siyo watu wa Kuaminika kwa sasa hata mwenye degree ya History atajifanya MD
 
Unashangaa ya KIU, St. Joseph Luguluni wahindi wanatoka Gujarat kuna kusalimia waume zao na kugeuka wahadhili!
 
Ni jambo jema chuo kuwa na mchanganyiko wa lecturers wa kimataifa yaani kutoka nje na wa ndani maana inasaidia kuinua sifa si za wanafunzi tu kimataifa bali hata kitaaluma na kujiamini.
 
Ni jambo jema chuo kuwa na mchanganyiko wa lecturers wa kimataifa yaani kutoka nje na wa ndani maana inasaidia kuinua sifa si za wanafunzi tu kimataifa bali hata kitaaluma na kujiamini.
Hatupingi Uwepo wao swali ni kuwa je wapo kihalali mana tusijekaribisha maadui kwa mgongo wa wahadhili(lecturers) taratibu za mtu kuwa nchini kama mgeni zinajulikana wanapaswa kuwa na work permit ndio wawe legally kufany kazi sio mtu anakuja kusalimia then anabaki mazima kufundishi sio hapo tu waende pia sehemu kama zanzibar na Arusha kwenye mahotel uone wakenya walivyojaa bila vibali
 
Back
Top Bottom