IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

ukiwauliza wanakwambia uchumu unakuwa kwa 7% .........nimeshasema mwakani mwezi wa pili tutakuwa hatuna pesa....
 
ni kweli hapa, kuwa na sera nzuri za uchumi ni kitu kimoja lakini utekelezaji wake ni kitu kingine ambavyo inabidi viende hand in hand. Kuna gap kubwa kati ya wataalamu (watengeneza sera/wachumi) na wanasiasa (watekelezaji) hapa TZ ambao ndio wanasimamia hizo pande mbili na ndio maana resources zote zikiwa supported na amani iliyopo havionyeshi mafanikio yoyote ya maana.
Lakini kitu kikubwa kabisa kilichosahaulika ni kuwa uchumi wa kweli unajengwa na mtu mmoja mmoja ambapo linakuja suala la mass education (universal education) ili kumwezesha mtu binafsi atakapokuwa kuwajibika strategically kuleta mabadiliko. Sasa hapa serikali inawa mislead wananchi wake kwa kuwaambia kuwa itawafanyia kila kitu na kutowaeleza ukweli wa mambo pale mambo yanapohalibika. Kwa sasa hivi hakuna kabisa uwajibikaji wa binafsi hapa Tanzania na hasa kwenye taasisi za umma ambazo ndizo zinasimamia uchumi kwa vile hiyo spirit imeanzia uongozi wa juu. Tatizo kuu likiwa lilelile kuwa kwa kutowas sensitize kama individuals!
Hizi 'variables' (wataalamu+wanasiasa+wananchi=maendeleo) endapo zitakuwa katika mpango huo zinaleta maendeleo lakini ukizieuza "kichwa chini miguu juu" inakuwa equivalent na UMASIKINI kama tulivyo sasa!
wasomi wa tanzania-wachumi hawana nafasi, maamuzi yote ni ya kisiasa tu bila kupata ushauri wa kuaalamu
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!
Declaration of bankruptcy is always a shame especially at the amidst of ample resources!! and rampant corruption like TZ led by Msanii.
 
Wachumi wetu mko wapi?mbona mambo yanazidi kuwa magumu kwa walalahoi.Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania ?

Mkuu, kama Serikali ingelianzisha kitu kinachoitwa "Dawati la JF" kwa maana ya kutumia michango mbalimbali inayotolewa na wanaJF na kuifuatilia na hatimaye kuitekeleza, nadhani swali hili usingeliuliza. Wana JF ina watu wa makundi tofauti, kuna vilaza, kuna waropokaji lakini kuna great thinker wa ukweli ambao wameshaishauri Serikali hii kwa namna ya kipekee tena bure kabisa, ni suala la kuchambua na kutekeleza, lakini wapi wao wanajua ku-hire ma-consultants ambao hawana lolote zaidi ya kuja na li-document kuubwa lisiloweza kusomwa na viongozi wetu vilaza hawa, na likisomwa halifanyiwi kazi.
Kwa uchache tu,
JF
1.ilijadili mfumo mpya wa kuingiza magari wa TRA na athari zake
2. imejadili misamaha ya kodi na athari zake na nini serikali ifanye
3. ilijadili madhara ya kupanga mipango kwa mazoea
4. Ilijadili athari za mgao wa umeme na mapendekezo yake
5. ilijadili mfumo rafiki wa uwekaji wa viongozi wa kisiasa na athari zake
6. ilijadili ukubwa wa sserikali kwa maana ya mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, manaibu katibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na madhara yatakayosababishwa na "Diminishing return"
7. ilijadili mfumo mbovu wa uchaguzi wa biashara ya kura badala ya uhalisia wa sera
8. ilijadili madhara ya gharama kubwa za uchaguzi kwa maana ya machapisho ya fulana, kofia, khanga, suruali, magamba, magwanda, chai simple, mikopo ya kina mama lishe isiyozingatia ushindani wa kimikopo, kumbuka pesa zote hizi zina-loose track ya kuwa monitored na mfumo wa mzunguko wa fedha,
9.ilijadili madhara ya tume ya uchaguzi kuwalea viongozi wabovu na kudharau matokeo halali ya wapiga kura,
10. ilijadili madhara ya chama tawala kutozingatia ushauri wa kitaalamu katika maamuzi ya kitaifa
11. ilijadili ubaya wa safari za kwenda nje zinazokuwa-spearheaded na mkuu wa nchi
12. ilijadili madhara ya kutochukua hatua kwa wahujumu wa mali za umma kuwa impact yake ni kila mmoja kuwa mhujumu wa mali za umma
13. ilijadili madhara ya kutokuwa na Reli ya Kati, Kusini, Arusha na madhara yake kwa uchumi kuwa kuleta mahitaji makubwa ya magari makubwa "trucks" kwa ajili ya kusafirisha miziggo na hatimaye kuwa na demand kubwa ya mafuta ya diesel na petrol(madhara yake yapo wazi)
14. imejadili madhara ya kutokuwa na shirika la ndege kuwa kuua hub ya nchi hivyo kuudhoofisha utalii na mengineyo
15. imejadili mishahara midogo ya walimu hivyo kupelekea walimu kutokuwa na moral ya kazi na kuhama fani hivyo kuwa na graduate wabovu
16. imejadili ......kila kitu
17. ilijadili madhara ya wabunge wa kuteuliwa kuwa hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kula stahili na kupiga meza kupitisha hoja dhaifu na dhalili za serikali
18. ilijadili matumizi ya serikali katika kununua magari ya GX V8 kwa ajili ya kuchukua wakurugenzi kutoka mbezi beach hadi posta na kuwarudisha
19. ilijadili hata wizi wa vifaa pale bandarini kuwa utafukuza watumiaji wa bandari yetu toka Congo, Zambia, burundi, Uganda, Rwanda
20. ilijadili madhara ya familia za viongozi na watendaji wa serikali nao kuwa viongozi na watendaji wa serikali kwa maana ya matumizi resources za serikali
21...
Orodha ni ndefu mkuu, cha msingi waambie kuwa wachumi wapo, ma-injia wapo, wahasibu wapo, wanasheria wapo lakini nao wako bize kwenye kufisidi mali za umma kama viongozi wao wanavyofanya.
 
Hakuna kitu kinakula hela ya serkali kama magari - haya ma-STK. Bili ya mafuta ni noma, hasa wakati huu wa joto ambapo hayazimwi hata yakipaki ili kibosile akute AC imepooza. Usiseme kuhusu service. Service ya kumwaga mafuta ya STK inaweza kupitiliza hata Shillingi Millioni moja.
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!
Mkuu FF, sidhani kama kukopa ni tatizo, ni utaratibu wa kawaida tu. tatizo letu hapa ni kuwa (kulingana na taarifa nilizoziona hapa) tunatumia zaidi kuliko tunavyokusanya. Hii inamaanisha kuwa tunalazimika kukopa ili kufidia pale tunaposhindwa kukusanya. isingekuwa vibaya kama tungekuwa tunakopa kwa ajili ya midari ya maendeleo kwa sababu ingekuja kulipa hayo madeni baadaye. hatari ni kuwa tunakopa kwa ajili ya kughramia recurrent expenditure. Ukiona hali kama iyo, basi ujue kuwa tunaelekea kule kwa Greece
 
Mficha ugonjwa kifo humuumbua.! Na masharti mapya ya kukopa ndio hayoo kama yalivyotolewa na Uingereza, serikali inaongozwa na ma poyoyo .! Kutegemea kodi ya sigara na pombe
 
Brother kila siku nawaambia watu wa humu JF kuwa achaneni na wehu wa humu, wamo wengi tu. Unapoteza nguvu nyingi kumfafanulia jambo la msingi asiyestahili. Kumbukeni kila soko lina mwehu wake!
 

Kwani mishahara siyo matumizi ya kawaida?
 
Serikali ya Ugiriki imeanguka jana tu kwa mambo ya hivihivi, matumizi makubwa kuliko mapato. Na huko ni Ulaya. Mimi kwakweli naogopa.
 
hapa nakukubali mkuu maana Mzee Mwnakijiji alitoa hapa (bureeeeeeeeeeee) draft ya katiba. Pia alitoa structure ya Bodi ya Mikopo ambapo ilikuwa wazi tu! Lakini kaulize kiasi ambacho Werema na Celine Kombani wamespend katika kupindisha sheria ya katiba. Angalia wanafunzi masikini ambao wangeliweza kuliondoa taifa hili hapa lilipo walivyokosa nafasi za kusoma vyuo!
 
Yea, this is impressive, but the way we are doing now, by obtaining loans to foot recurent expenditure, we are going to erode our impressive reswerves soon, and that is not health for our economy
 
Hapo panaopoonekana aid as total % of budget kuwa inashuka haina maana kuwa wanakopa less,bali ni kwamba mapato ya ndani yameongezeka lakini bila kuchukua hatu yoyote ya kupunguza aid money.

Ama kweli, onyesha na kabla ya kuchukuwa nchi Kikwete ilikuaje? hiyo ulioonesha tu haina haja ya kuelezewa inakusuta

JF Premium Member



Join Date : 2nd November 2007
Posts : 8,553
Rep Power : 83


[h=2]
Re: IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa![/h] [TABLE="class: cms_table_cms_table"]
[TR]
[TD]Period[/TD]
[TD]Domestic Revenue (Tsh)[/TD]
[TD]Foreign Aid (Tsh)[/TD]
[TD]Overall Budget (Tsh)[/TD]
[TD]AID (Ushoga) as % of total budget[/TD]
[TD]Domestic Revenue as % of total budget[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2007 – 2008[/TD]
[TD]3.5 trillion[/TD]
[TD]2.5 trillion[/TD]
[TD]6.1 trillion[/TD]
[TD]41 %[/TD]
[TD]57 %[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2008 – 2009[/TD]
[TD]4.8 trillion[/TD]
[TD]2.4 trillion[/TD]
[TD]7.2 trillion[/TD]
[TD]33 %[/TD]
[TD]66 %[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2009 – 2010[/TD]
[TD]6.3 trillion[/TD]
[TD]3.1 trillion[/TD]
[TD]9.5 trillion[/TD]
[TD]33 %[/TD]
[TD]66 %[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2010 – 2011[/TD]
[TD]8.3 trillion[/TD]
[TD]3.2 trillion[/TD]
[TD]11.6trillion[/TD]
[TD]28 %[/TD]
[TD]72 %[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2011 - 2012[/TD]
[TD]6.7 trillion[/TD]
[TD]3.9 trillion[/TD]
[TD]13.5 trillion[/TD]
[TD]28 %[/TD]
[TD]49 %[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Marekani wanakopa na pesa nyingi zinaishia kwenye vita visivyo na tija..Afghanistan, Iraq na Libya.
 
Nilikuja na hii hapa mmeshindwa kuijibu mpaka sasa:

Ili kuwasaidia, nikaweka data hizi hapa ambazo zinafuta swali la 14 hapo chini (Akiba ya nje (foreign reserve), nawapa fursa tena tuendelee na mengine 13 yakiyobaki, msilete hadithi ndefu zisizokuwa na "data", leteni hoja yakinifu sio ubunifu:



  1. Weka idadi ya barabara za lami kabla ya Kikwete
  2. Weka idadi ya Shule kabla ya Kikwete
  3. Weka idadi ya Waalimu kabla ya Kikwete
  4. Weka idadi ya Zahanati kabla ya Kikwete
  5. Weka idadi ya Viwanda kabla ya Kikwete
  6. Weka idadi ya Utalii kabla ya Kikwete
  7. Weka idadi ya Umeme kabla ya Kikwete
  8. Weka idadi ya Maji kabla ya Kikwete
  9. Weka idadi ya kazi kabla ya Kikwete
  10. Weka idadi ya biashara kabla ya Kikwete
  11. Weka idadi ya umaskini kabla ya Kikwete
  12. Weka idadi ya kilimo kabla ya Kikwete
  13. Weka idadi ya bidhaa zinazopita bandari zetu kabla ya Kikwete
  14. Weka akiba ya fedha tulokuwa nayo kabla ya Kikwete
 


Msilumbane waungwana, mnachozungumza ni kimoja. tofauti yenu, wakati gmosha matumizi ya stionary, fuel, ukarabati nk umeyaweka kwenye posho na mishahara na kubaki na takribani 20% kwa miradi ya maendeleo; mwenzio hizo other charges kazijumuisha kuwa ziko kwenye maendeleo na hivyo kukamilisha takriban 40% ya total bdget.

My note. Pesa for other charges, zinaweza kupunguzwa kuondoa misafara ya viongozi inayotumia magari mengi, kupunguza/kuondoa matumiz ya magari ya kifahari yanayokunywa mafuta mengi, wakachukua gari simple ndo zikawa kwa matumizi ya office. na kuepuka kila mkuu wa idara kuwa na gari lake na bajeti yake, zikatafutwa costa/isuzu za kuwafuata wafanyakazi na kuwarudisha nyumbani,
 

Tunaongelea hali ya sasa ya kiuchumi na muelekeo wake, Wakuu wamejaribu kuchambua bila ya kuingiza siasa ndani wacha tubakie kwenye mkondo huo tafadhali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…