Imetosha kusoma tu: Jiunge, Changia, Shiriki..

Imetosha kusoma tu: Jiunge, Changia, Shiriki..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,239
Reaction score
44,476
Tunayakosa maoni yenu na mawazo yenu; nikiangalia maoni yanayotolewa mara kwa mara na wale ambao tumo humu siku nyingi ni wazi kuwa sehemu kubwa ya watumiaji hawajajiunga na ni watazamaji tu.

Kwa maneno mengine, yawezekana wanawakilisha kundi kubwa la Watanzania ambao wamechagua kuangalia toka mbali tu kile kinachofanyika; watu ambao wanaweza kuwa wanalalamika sana pembeni lakini wakipewa nafasi ya kutoa maoni huchagua ukimya kuliko kutoa maoni yao ambayo yanaweza kukosolewa, kupingwa, au kuungwa mkono au hata kusababisha malumbano.

Kwenye wanachama zaidi ya elfu 16, yawezekana siyo zaidi ya watu 100 wanaotoa maoni yao mara kwa mara na labda ni kikundi cha watu 50 tu kinachotoa mwelekeo wa maoni hapa. Hili siyo jambo zuri.

Najua kwa kutoa maoni yenu au kujiunga moja kwa moja wengine mnahatarisha hadhi na majina yenu na hata nafasi zenu. Na hasa labda wakati mwingine mnakwazika kwani baadhi yetu humu hatuchelewi kuwashambulia mara moja bila kuwapa nafasi ya kujizoesha au hofu ya kuwa unaweza kusema kitu kika kugive away.

Ushauri wangu ni kuwa yawapa mkivuke hicho kizingiti cha hofu (threshold of fear) na hatimaye nanyi mtoa mawazo yenu kuchangia. Binafsi nitakaa pembeni na mimi kuwa msomaji wiki hii (isipokuwa kama kuna ulazima kweli wa kuvunja ukimya huo) ili kuwapisha wanachama wapya nao watoe michango yao.

So.. inatosha kusoma.. jiunge... changia!!!
 
Lakini kuna wengi ni members, huamua tu kusoma kama guests, na wakiona kinachowagusa huingia na kujibu au kuchangia mawazo!
Suala la kuchangia(fedha) ni nyeti, hata kwa members wa siku nyingi hapa ndani,.../.... jamani, MKONO MTUPU HAURAMBWI!

Kuhusu uoga au kuhatarisha kazi, mi naona sio kigezo cha kumtisha mtu, maana hatutumii majina yetu, unless mtu akiamua kwa udi na uvumba kumfuatilia mtu.

Mkjj, unaanza kuishiwa hoja nini, kwanini uende likizo ya wiki?...au na wewe ni mmoja wa wanaokumbwa na kizingiti cha woga?
 
hahaha.. hivi chemchemi huishiwa maji kwa vile watu hawachoti.. nipo hapa namalizia hadithi yangu ya kwanza in almost three years!! finally nimekivuka kile kiitwacho Writer's Block..
 
Nashukuru sana kwa maoni muafaka, naomba unieleze namna ya kuchangia kutoka Dar es Salaam, kwa kutumia Shilingi ya Tanzania. Nitachangia vipi mtandao wetu maridhawa? Maelekezo naomba yatumwe kwenye e-mail hii:
simbamwene@hotmail.com
 
hahaha.. hivi chemchemi huishiwa maji kwa vile watu hawachoti.. nipo hapa namalizia hadithi yangu ya kwanza in almost three years!! finally nimekivuka kile kiitwacho Writer's Block..

Unamalizia kutunga/kuandika au kusoma?
Kama ni kitabu, tutakipata?...Hongera kwa kuvuka hicho kigingi!
 
Nashukuru sana kwa maoni muafaka, naomba unieleze namna ya kuchangia kutoka Dar es Salaam, kwa kutumia Shilingi ya Tanzania. Nitachangia vipi mtandao wetu maridhawa? Maelekezo naomba yatumwe kwenye e-mail hii:
simbamwene@hotmail.com

Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

1. Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Paypal users:

Send via email - macdemelo@gmail.com moja kwa moja itafika na utaarifiwa ndani ya dakika 60 kuwa mchango wako umepokelewa.

2. Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo Mubyazi wa Dar es Salaam.

3. Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

4. Njia ya nne:

Unaweza kutuma recharge vouchers za tiGO, Zain, VodaCom au Zantel kwenda kwa Maxence - 0713444649 naye atakufahamisha kuwa kazipokea.

=================================

Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.

Tunayakosa maoni yenu na mawazo yenu; nikiangalia maoni yanayotolewa mara kwa mara na wale ambao tumo humu siku nyingi ni wazi kuwa sehemu kubwa ya watumiaji hawajajiunga na ni watazamaji tu.

Kwa maneno mengine, yawezekana wanawakilisha kundi kubwa la Watanzania ambao wamechagua kuangalia toka mbali tu kile kinachofanyika; watu ambao wanaweza kuwa wanalalamika sana pembeni lakini wakipewa nafasi ya kutoa maoni huchagua ukimya kuliko kutoa maoni yao ambayo yanaweza kukosolewa, kupingwa, au kuungwa mkono au hata kusababisha malumbano.

Kwenye wanachama zaidi ya elfu 16, yawezekana siyo zaidi ya watu 100 wanaotoa maoni yao mara kwa mara na labda ni kikundi cha watu 50 tu kinachotoa mwelekeo wa maoni hapa. Hili siyo jambo zuri.

Najua kwa kutoa maoni yenu au kujiunga moja kwa moja wengine mnahatarisha hadhi na majina yenu na hata nafasi zenu. Na hasa labda wakati mwingine mnakwazika kwani baadhi yetu humu hatuchelewi kuwashambulia mara moja bila kuwapa nafasi ya kujizoesha au hofu ya kuwa unaweza kusema kitu kika kugive away.

Ushauri wangu ni kuwa yawapa mkivuke hicho kizingiti cha hofu (threshold of fear) na hatimaye nanyi mtoa mawazo yenu kuchangia. Binafsi nitakaa pembeni na mimi kuwa msomaji wiki hii (isipokuwa kama kuna ulazima kweli wa kuvunja ukimya huo) ili kuwapisha wanachama wapya nao watoe michango yao.

So.. inatosha kusoma.. jiunge... changia!!!
unakaa pembeni ili wanachama wapya watoe michango yao KWENYE JUKWAA GANI?...(i hope sio siasa)..........
sasa kama hawana ''KA-NZI''...............
na kama hawana ''mitandao''............
na kama hawapo ''kwenye system''..........

NB:KARIBU KWENYE JUKWAA LA MAMBO YA KIKUBWA..........mimi na maria roza tutakaa pembeni wiki hii ili na wewe uchangie.
 
Mkuu Mwanakijiji
Naamini kwamba uzalendo utakuongoza japo kuandika line mbili tatu maana ukisema unajiweka pembeni ni sawa na kuamua kuwakimbia wanafunzi.

Lakini nakuunga mkono kwamba wengi wanachota humu bila hata ya kuchangia kitu. Shime wanajukwaa mlio silent msiwe kama wabunge wa bunge la tanzania ambao wengi ni kujaza namba tu wala hawajui ABC za uwakilishi wao bungeni
 
Kwenye wanachama zaidi ya elfu 16, yawezekana siyo zaidi ya watu 100 wanaotoa maoni yao mara kwa mara na labda ni kikundi cha watu 50 tu kinachotoa mwelekeo wa maoni hapa. Hili siyo jambo zuri.

Mwanakijiji, ni kweli kabisa hayo uliyoyasema... lakini mfumo wetu na tamaduni yetu ndivyo ilivyo... ni wachache sana huweza kusema wazi, na pia ujue kwamba si wote wachangiaji humu tunajua risks associated with our comments nadhani itakua vizuri tuendeleze "status-quo". Kila memba mpa atavutika kwa namna yake na kuingia kama siye tulivyoingiza vichwa humu,

Hilo la kuchangia nadhani ni la mbolea sana na tunahitaji kuvuka mipaka ya members kupata financial support

DN
 
kuna watu humu wao wamelalia mlengo mmoja tu hasa wanapoona mwanachama mpya katoa mchango wake basi wao moja kwa moja watajaribu kuondoa maana ya kitu ambacho mchangiaji amekileta kichangiwe au watajifanya ni wajuaji sana kiasi cha ku-paralyse mada yenyewe na kuishia kuharibu kabisa maana ya kitu ambacho kingekuwa na manufaa makubwa kwa jamii.
pili unaweza kukuta hoja imetolewa na member wa siku nyinig hata kama itakuwa ya ki-puuzi utakuta inapewa postive response bila kujali dhima yake. hii inamfanya mchangiaji mpya kuona hakuna maana ya kuingia kwenye exposure ambayo inaweza kum-affect psychologically
 
hahaha.. hivi chemchemi huishiwa maji kwa vile watu hawachoti.. nipo hapa namalizia hadithi yangu ya kwanza in almost three years!! finally nimekivuka kile kiitwacho Writer's Block..

Hongera kwa kuivuka hii kitu mzee.Ni ngumu kama nini, kwani waweza kuandika hata kurasa mia lakini huku kusita kunaweza kukufanya ukaacha kabisa kuandika.
 
Mbali na mchango wa mali, lakini kama sikumuelewa vibaya mzee mwanakijiji alikuwa akimaanisha kuchangia hoja kwenye thread mbali mbali au pia kuanzisha hoja moto moto mpya.

Plz watu msifungwe kwa sababu mmeombwa kuchangia jukwaa pesa. Lakini mawazo yenu ni muhimu kwa taifa hili ninalolipenda na hupenda kuliita Danganyika.
 
Back
Top Bottom