Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,651
Mediaman baada ya kunukuu mistari mingi ya biblia na kuona haimuungi mkono, sasa amegeukia viongozi wa kisiasa hata kufikia kumtaja Obama amsaidie. Naona wale wapinzani wa babu wamekamatwa pabaya, ni kama kusema pamoja na kufunga na kumuomba mungu wao amdhuru babu hakuwasikiliza. Hii ni kusema kwamba mungu wa babu huenda ndie Mungu wa kweli maana amelifunga anga lote na miungu minginehaifurukuti, mfano wa alivyofanya Eliya hapo walipowakusanya wana wa Esraeli mlimani.
Watu mnaojiita wa kiroho mnatupa nafasi sisi watazamaji kwamba mungu wenu huenda amesafiri ama amelala na toka mnampigia kelele juu ya babu hasikii. Jitahidini huenda akawasikia atakapozinduka usingizini.
Mungu wa Israel, mungu wa manabii watakatifu, tunaemwabudu kwa jina la Yesu, amezungumza katika kitabu cha zaburi ya 103 kusema, yeye ndie anaetusamehe maovu yetu na kutuponya magonjwa yetu yote. Sasa hakuna mnalowezafanya kwa yule aliyemsamehe na kumponya, maana hakufanya hivyo kwa sheria bali kwa neema yake.
Mtataka kuupiga mchuguu teke hata lini?
.
Ewe shabiki wa babu uliyejawa upofu. Tutaendelea kupaza sauti hetu hata Yesu Kristo atakapojitwalia utukufu.
1. Hayuko hata mmoja anayeomba Mungu amdhuru babu. Bali twaomba neema ya Mungu iwashukie wali mliopotea kwa kufuata mkumbo, mkidhani Mungu wa kweli anafuata idadi ya watu. Hakuna andiko hata moja linaloelekeana na tiba za asili za babu.
2. Unaposema Mungu wa babu huenda ndiye Mungu, inaonyesha kiwango cha imani yako. Ina maana hata yule uliyedhani unamwabudu kabla ya loliondo hukumjua vema bado. Ndio maana umesombwa na mafuriko ya loliondo. Sasa umeamua kujaribu Mungu wa loliondo. Kumbuka Mungu huruhusu mambo kama haya yatokee ili iwe kipimo cha imani. Hapa ndipo utawajua wale wamwabuduo kwa kinywa tu lakini mioyo yao iko mawindoni ikitafuta miungu mingine kama babu wa loliondo.
3. Katika zama za nabii Eliya Mungu alitenda kazi zake kupitia vinywa vya manabii. Lakini tangu Kristo alipoleta neema na uzima wa bure, neno lake limeandikwa mioyoni mwetu. Hivyo tuna uhuru wa kuchagua kumfuata ama kutomfuata. Ukisoma zaburi ya 73 utaona jinsi anguko la watu wenye dhihaka, kiburi, majivuno, kujiinua juu, ambao wameweka kinywa mbinguni wakati ulimi ukitangatanga duniani. Mungu huwaweka kwenye utelezi wakaanguka hata mahali palipoharibika. Huiondosha sanamu yao ghafla. Hivyo kama babu wamuona ndio Eliya wenu, unapotea. Eliya alifanya ishara iliyopelekea watu kubadili mioyo yao na kumwabudu Mungu wa kweli, siyo kushangilia muujiza tu. Muujiza wa Eliya uliamsha hofu kuu kwa Mungu aliye juu. Muujiza wa babu je?
4. Unasema Mungu wa manabii watakatifu ndiye mnayemwabudu ninyi, kwa jina la Yesu. Mbona mnamwabudu kwa vinywa tu wakati matendo yenu yakiwa mbali naye? Mbona huyo babu hamtaji Yesu? Baadhi ya mashabiki wa loliondo wanadai eti hamtaji babu ili kuepuka kuwagawa mashabiki wake, kwa vile Mungu anaabudiwa na wote na si Yesu. Sasa wewe huyo Yesu huko loliondo ulimtoa wapi tena? Tena hiyo aya ya zaburi umeisoma vizuri ukaielewa? "Anatusamehe maovu yetu" halafu sasa baada ya msamaha "anatuponya magonjwa yetu yote." Hivyo msamaha kwanza. Je ulipokwenda loliondo ulianza kwa kumwomba Yesu msamaha? Au ulikimbia kuwahi foleni ya babu tu? Maana Yakobo anasema tukiziungama dhambi zetu Yeye ni mwaminifu hata atusamehe..... Hebu tafakari hapo.
5. Ni kweli Yesu ametuletea neema. Lakini hilo lisiwe chaka la kujificha katika maovu. Warumi 6:1 "Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?." Wewe ndio amua sasa. Hivyo neema sio substitute ya kuendelea katika dhambi. Ndio maana woooooote mliotoka kwa babu tunategemea tuone matunda mema, mkiishi katika neema ya Kristo.
"Bila imani haiwezekani kamwe kumpendeza [Mungu] vema, kwa maana yule anayemkaribia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na kwamba yeye huwa mthawabishaji wa wale wanaomtafuta kwa bidii." (Waebrania 11:6)
Mungu akubariki sana.