Imetimia mwezi mmoja sasa tokea nimeanza kukaa na Mwanamke, natamani nimtimue

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Dah wazee, kutokuoa ni Bora kuliko kuoa, nimekaa Miaka mingi ya u-bachelor mpaka age ilipoanza kusonga hivi, maisha yangu yote yalikuwa ya furaha isiyo na kifani, sina stress za hovyo hovyo naweza kujiamulia kwenda sehemu yoyote bila stress, mipango yangu Ilikuwa inaenda sawa kidogo nachokipata najibana nikajikita kununua mashamba, kiufupi maisha yalikuwa mazuri though nilikuwa na mchumba mmoja wa muda mrefu kidogo, nikasema nivute niiweke sawa nikatoe mahali baadae kidogo.

Ni mwezi mmoja tu lakini stress nilizonazo ni kama nimekaa Miaka 70 kwenye ndoa, ogopa Mwanamke mjuaji, kiburi Cha chini chini asiefata maelekezo, kichwa changu kinawaka moto vibaya mno. Sina furaha tena nimemtimua aondoke amegoma naona hapa mimi ndio nitimke kimya kimya, nimuachie vitu nisepe.

Ninapokaa hapa nina miaka 5 sina mazoea na watu kabisa, sipendi kuzoeana na siruhusu mtu anizoee zaidi ya salamu (haswa Majirani) wananiona mkorofi sana kwa sababu ya kutopenda mazoea. Alipofika hapa nilimwambia principle yangu huwa sipendi mazoea na watu zaidi ya salamu na vitu vingine vidogo vya ku-socialize Lakini mazoea lazima yawe na mipaka. Ooh ndani ya mwezi ameshajuana na watu mbalimbali, majirani woote wanamfahamu.

Ndani ya Mwezi mmoja tu majirani wote wanajua identity yake tokea alipozaliwa na mikoa aliyoishi Hapo kabla, kiukweli Sielewi but moyo wangu una hasira sana. Kiukweli sipendi kufungua password ya maisha yangu kabisa tena kwa stranger Lakini huyu yeye akitekenywa tu anafunguka vibaya mno japo tokea amekuja nimeshamwambia zaidi ya mara 1000 never trust anybody. Kila unaemuona mbele yako muone kama threat kwenye maisha yako, Lakini haelewi.

Kwa sehemu mbalimbali nilipopita kwa nature ya mabinti kama huyu nilienae Ilikuwa rahisi sana kusex nae bila hata ya kumtongoza kwa sababu unachokifanya ni kutengeneza mazoea tu na trust kwa sababu wamejengwa kuamini watu mapema huwa wanaliwa kizembe tu.

Mmewezaje kukaa na Mwanamke mjuaji? Unalomwambia hafanyi? Wala maelekezo hafati?

Nimeona kwamba katika Maisha watu tupo na character tofauti tofauti, tumezaliwa katika mazingira tofauti tunapokutana ukubwani kimbembe Cha kubadilishana tabia ndio kinaanza unakuwa mwana saikolojia, sosholojia na filosofia bila kupenda.

Suala jingine namuona kabisa ana chembe chembe za ubinafsi na uchoyo, niliwaza nifungue biashara yeye awe msimamizi lakini nimerudi nyuma na kuhairisha kabisa, unajua uaminifu wa vitu vikubwa huanza na vitu vidogo, kuna siku tulikuwa tunataniana nae akasema "ndio maana chakula kikitetengwa unakaaga mpaka Mwisho" ilo jambo lilinifikirisha sana.

Navyoona huko mbeleni kama naenda kupiga mtu vibaya mno.
 
Dah wazee, kutokuoa ni Bora kuliko kuoa, nimekaa Miaka mingi ya u-bachelor mpaka age ilipoanza kusonga hivi, maisha yangu yote yalikua ya furaha isiyo na kifani, Sina stress za hovyo hovyo naweza kujiamulia kwenda sehemu yoyote bila stress, mipango yangu Ilikua inaenda sawa kidogo nachokipata najibana nikajikita kununua mashamba, kiufupi maisha yalikua mazuri though nilikua na mchumba mmoja wa muda mrefu kidogo, nikasema nivute niiweke sawa nikatoe mahali baadae kidogo.

Ni mwezi mmoja tu Lakini stress nilizonazo ni kama nimekaa Miaka 70 kwenye ndoa, ogopa Mwanamke mjuaji , kiburi Cha chini chini asiefata maelekezo kichwa changu kinawaka moto vibaya mno Sina furaha tena nimemtimua aondoke amegoma naona hapa Mimi ndio nitimke kimya kimya nimuachie vitu nisepe.

Ninapokaa hapa Nina miaka 5 Sina mazoea na watu kabisa sipendi kuzoeana na siruhusu mtu anizoee zaidi ya salamu (haswa Majirani) Wananiona mkorofi sana kwa sababu ya kutopenda mazoea, alipofika hapa nilimwambia principle yangu huwa sipendi mazoea na watu zaidi ya salamu na vitu vingine vidogo vya ku-socialize Lakini mazoea lazima yawe na mipaka. Ooh ndani ya mwezi ameshajuana na watu mbalimbali Majirani woote wanamfahamu.

Ndani ya Mwezi mmoja tu Majirani wote wanajua identity yake tokea alipozaliwa na mikoa aliyoishi Hapo kabla, kiukweli Sielewi but moyo wangu una hasira sana. Kiukweli sipendi kufungua password ya maisha yangu kabisa tena kwa stranger Lakini huyu yeye akitekenywa tu anafunguka vibaya mno japo tokea amekuja nimeshamwambia Zaidi ya mara 1000 never trust anybody Kila unaemuona mbele yako muone kama threat kwenye maisha yako, Lakini aelewi.

Kwa sehemu mbalimbali nilipopita Kwa nature ya mabinti kama huyu nilienae Ilikua rahisi sana kusex nae bila hata ya kumtongoza kwa sababu unachokifanya ni kutengeneza mazoea tu na trust kwa sababu wamejengwa kuamini watu mapema huwa wanaliwa kizembe tu.
Mmewezaje kukaa na Mwanamke mjuaji? Unalomwambia hafanyi? Wala maelekezo hafati?

Nimeona kwamba katika Maisha watu tupo na character tofauti tofauti, tumezaliwa katika mazingira tofauti tunapokutana ukubwani kimbembe Cha kubadilishana tabia ndio kinaanza unakua mwana saikolojia, sosholojia na filosofia bila kupenda.

Navyoona huko mbeleni kama naenda kupiga mtu vibaya mno.
Sijakuelewa bado, hupendi watu wa kuzoee kwa kifupi upo kivyakovyako salaam imeisha hiyo.

Sasa haya Maneno ya umbea kuhusu mchumba wako umeyapata wapi? Hebu niweke sawa kwanza hapo halafu ndio tuendelee.
 
Bila shaka mwanamke ni mswahili....
 
Mkuu Prakatatumba abaabaabaa mbona unataka kumchoka mwenzio bado mapema hivyo?

Kuna watu inawachukua muda hata miezi 6 kuweza kujifunza na kuelewa mambo.

Nadhani umpe muda na ujifunze kumvumilia ukijua mwenzio sio Malaika bali ni Binadamu kama wewe.

Mungu awaongoze kwenye mahusiano yenu, muishi hadi muone Wajukuu zenu.
Jamaa ameshakula sasa amemkinai mapema hapa anatafuta tu sababu ya kuingia mitini.

Ila nawatahadhalisha tu mtindo wa kuchezea mabinti za watu na kuwakimbia mkumbuke kuna kurogwa, ni vitu nimeshuhudia kwa macho yangu si kuhadithiwa.
 
Hata mimi sipendi sehemu nimekaa nimeji brand kwa namna ninayotaka mimi nionekane halafu aje mtu aharibu.

Kuna sehemu nilikuwa naishi (nilihama baada ya hili tukio). Nikawa nina uhitaji wa msichana wa kazi ila akawa hajapatikana. Basi kuna cousin wangu akaja kunisaidia kidogo before aende chuo.

Aisee ndani ya siku kadhaa ameshaanika kila kitu kuhusu mimi nakwambia. Anafunguka hadi ambavyo hatakiwi kufunguka.

Na watu wanavyopenda umbea na kujua ya watu basi walimpenda kinoma yaani.

Yaani mimi naishi zangu mjini nime jibraaaaand hata kama nilikuwa nafake ila ilinipa heshima halafu kaja mtu siku mbili anafunguka kila kitu.

Nilimaimd sana alivyoondoka nikahama.

Mkuu mimi nipo upande wako kama hajirekebishi timua. Mtu wa kujitangaza tangaza kwa watu wasiomsaidia chochote hana maana.
 
Sijakuelewa bado, hupendi watu wa kuzowee kwa kifupi upo kivyakovyako salaam imeisha hiyo.

Sasa haya Maneno ya umbea kuhusu mchumba wako umeyapata wapi? hebu niweke sawa kwanza hapo halafu ndio tuendelee.
Nikitoka job namkuta yupo na Majirani huko nje, story zake tukiwa tunaongea. Pia weekend huwa nashinda ndani asubuhi mpaka jioni akitoka nje akiwa anafanya shughuli zake, utamsikia Mimi Dodoma hivi na vile....eeeh Nina ndugu yangu pale....nimekaa sana pale.....nimesoma Hapo.....hata Mama yangu alishaugua huo ugonjwa.....chuma hayo majani yanatibu UTI. Nadhani umenielewa kaka, Sasa hiyo situation ya kuongea ongea sana sijisikii vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom