Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

Machalii wa A Town mpo ya kweli hayo?

Tupo kabisa.Kipindi cha kwenda Loliondo tulivuna pesa za watu wa Dar, Mbeya, Iringa na kwingineko. Magari yetu tulikodisha sana ila wengine hatukunywa dawa kwa kutokuwa na imani nayo.
 
Machalii wa A Town mpo ya kweli hayo?

Tupo kaka sisi tulipiga hela ya tours ,mafuta,msosi kwa mashambenga wote bila kujali babu aachwe matapeli wapo makanisani na waganga wamejaa kila kona hata wabunge wanatapeli wananchi ujanja kupata na babu mwacheni ale kuku samunge mlikwenda wenyewe hamkuitwa wajinga ndio waliwao
 
Sawa, ni kweli haya yote yameshatokea, watu wamekunywa dawa na hawajapona, wengine wameshadead mda tu. Swali linakuja Nani wakulaumiwa hapa. Kati ya
(i) Babu,
(ii) Serikali,
(iii) Wananchi waliokuwa na imani juu ya tiba itolewayo na Babu.
Tutafakari!!
 
Ni ishu ya kiimani zaidi, kama imani haba imekula kwako! Ingawa nilisikia huo mmea unasaidia wagonjwa wa kisukari ( sosi huko huko nimri)
 
Watanzania tuna kasoro, tulitakiwa kujua kuwa hii dawa siyo ya kweli tangu mwanzo, lakini watu tunaowategemea kabisa wakiwemo viongozi wa serikali na wasomi ndo walikuwa mstali wa mbele kwenda huko. Nchi hii tunahitaji elimu, big time.
 
Ingekuwa kwa wenzetu serikali nzima ingeachia ngazi. Huwezi kuachia watu watumia dawa then baadae ndio unasema ni utapeli!


Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Watanzania wengi wamekuwa na mila potofu wengine wamekuwa wakitumia dawa za kuongeza umri wamekuwa wengi hasa wa vijijini wamekuwa wanakimbilia kwenye Kikombe cha Babu. Je, Waziri ananihakikishiaje kuwa Dawa ya Babu inatibu Ugonjwa wa UKIMWI moja kwa moja?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 78 SESSION # 3
1646.jpg
Answer From Hon.Mponda, Dr. Hadji Hussein
HEALTH AND SOCIAL WELFARE
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:

Mheshimiwa Spika, Kikombe cha Babu kama kinavyojulikana Babu wa Loliondo, hadi sasa bado tunakifanyia utafiti ili kutoa jibu kwamba kile Kikombe kimoja cha Babu kinatibu magonjwa yale matano ambayo Babu amedai anatibu. Taarifa tulizozitoa mwanzo kwa Watanzania, tulijibu swali la kwamba, dawa ile ni salama kwa matumizi ya afya ya binadamu na haina sumu. Tumewaambia Wananchi kwamba, kwa kile Kikombe cha Babu, anachokitoa ambacho anachemsha kilo tatu za ule mzizi ndani ya maji yali lita 60, bado imedhihirisha ni salama haina madhara.

Hivyo basi, tunaomba Wabunge mpeleke taarifa kwa Wananchi kwamba, wavute subira, tunaendelea na utafiti ambao tunahusisha na wagonjwa pia ambao tayari wamepata Kikombe cha Babu ili tutoe jibu kama kile Kikombe kinatibu yale magonjwa matano. Ninashukuru.

Source: Parliament of Tanzania
 
Babu wa Loliondo lazima afikishwe Mahakamani kujibu shitaka la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu wakiwemo Viongozi wote wa Serikali waliokuwa wakimpigia debe.
 
Wafuatao wamethibitisha kupona kabisa:
1. Mh.Steven Wassira
2. Mh.Nimrod Mkono
3. Mh.Augustine Mrema
4. Mh.JMK wa Magogoni
 
LOL, Watachukua ile Nyumba na Umeme wa Jua toka kwa huyo MZEE? na MAPESA?

Ilionekana tangu mwanzo kabisa kuwa 'babu' huyo ni tapeli.

Kwanza alisema kuwa 'dawa' yake inatibu magonjwa ndani ya wiki moja. Alivyoona mambo hayaendi vizuri, akasema kuwa watu wasiache dawa zao za hospitali. Alivyoona vifo vinazidi kuongezeka kwa waonaotumia 'dawa' yake, akaleta swala la 'imani'.

'Babu' huyu ni tapeli tu, ila viongozi wa serikali walimtumia kama 'political diversion' baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Walitumia swala la 'tiba' ya 'babu' huyo ili kuwahadaa kuwasahaulisha watanzania kuhusu udhalimu uliofanyika kwenye uchaguzi wa mwaka 2010. Viongozi wengi sana wa serikali walienda Loliondo kupata 'tiba' ili waonekane kwenye vyombo vya habari ili wananchi wengi zaidi wapate kuvutwa huko Loliondo.

attachment.php


Na kweli, watu wengi sana walivutwa kwenye 'tiba' hiyo, na kusahau mambo yote ya wizi wa kura kwenye uchaguzi, wakasahau mambo ya kashfa za dowans, n.k.

Sasa, serikali hiyo hiyo inasema nini ?? 'kikombe' sio 'kikombe' tena ??
 

Attachments

  • Lukuvi.JPG
    Lukuvi.JPG
    29.9 KB · Views: 128
Uzuri wa Watanzania hawachelewi kusahau...

Hapo ndipo kwenye kero !! Anazuka tapeli, serikali inamuunga mkono katika utapeli wake...halafu inamgeuka !!!

Angalia wakati huo serikali ilikuwa inasemaje kuhusu 'babu' huyo...

[h=3]Dawa ya Babu haina madhara-Serikali [/h]
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA
MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE - LOLIONDO
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)

Taarifa ziliifikia Serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.
.
.
.
Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.

 
Ni taifa lenye viongozi wasiokwenda na wakati na sayansi na tekinologia kwani mbona niliona mawaziri wengi na wakuu wa mikoa walikunywa ina maana wao bado wanaishi stone age??? Yaani waziri mwenye Phd anakunywa dawa iliyotengwa kwenye kikombe kichafu to that extent. Our leaders are Blind so wote tutatumbukia shimoni. KATAENI BASI!!!!
 
hiii serikali pumbafu kabisa..si alijitokeza Dr .Mwele Malecela akakiri kuwa kikombe kinatibu
 
Back
Top Bottom