Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Aug 28, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]  [​IMG]
  Stori: Makongoro Oging'

  SERIKALI imethibitisha kuwa kitendo alichokuwa akifanya babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile, cha kutoa dawa ya kutibu magonjwa, ukiwemo Ukimwi aliyokuwa amedai kuwa ameoteshwa na Mungu ni cha kitapeli.


  Utafiti umebaini kwamba dawa hiyo ya babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.


  Kwa mujibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (pichani), utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa Ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa, umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.


  Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.


  “Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.


  Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.


  Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.


  Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.


  Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko.


  Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.


  “Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John.


  Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya, ameitupia serikali lawama kwa kuipigia debe dawa ya Babu na kuwafanya wagonjwa kutoroka hospitali huku wengi wao wakiacha kuendelea na dawa wakiamini wangepona baada ya kunywa kikombe kimoja .


  “Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa kumfungulia kesi.


  Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi.


  Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba, amesema babu huyo siyo mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi.


  Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  LOL, Watachukua ile Nyumba na Umeme wa Jua toka kwa huyo MZEE? na MAPESA?
   
 3. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,782
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu wa MCHUNGAJI kitanzini!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,968
  Likes Received: 891
  Trophy Points: 280
  teh teh teh...no comment!
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,189
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280
  Babu yake PakaJimmy, kwi! Kwi! Kwi!...teh teh teh...ha haa haaa...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mchungaji aliwatahadharisha wananchi kuwa wasiache kutumia madawa yao ya hospitali. Kwa uzembe wa Serikali na wakapuuza ushauri wake wa katazo wakaenda kwa kasi kubwa. Leo wasimulaumu kwa kuwa alitoa tahadhali sisi watu makini hatukwenda, lakini pia bei ya dawa yenyewe ilitia mashaka. Wamuache babu wasimuletee shida, maana hata Prof. Maji Marefu baada ya kutapeli watu sasa hivi ni Mbunge mbona hamjapiga kelele. Serikali DHAIFU.
   
 7. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ni kali. Mchungaji ana kinga, naweza hata kuwa wakili wake. Kwanza aliweka wazi kuwa jambo hili ni la kiimani zaidi. kama waliokwenda kwake hawakuwa na imani, ni wazi wasingeweza kupona. Mchungaji hawezi kuhusika kwa watu waliojipeleka kwake bila imani. Haiwezekani kulaumiwa kwa hilo.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,189
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280
  Machalii wa A Town mpo ya kweli hayo?
   
 9. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,724
  Likes Received: 1,232
  Trophy Points: 280
  alisema"TIBA YAKE INAKWENDA NA IMAN YA MTU"...hapo ndio atakapowapigia bao wanaotaka kumshita.....yes_no imani...hakuna kupona...lo!
   
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kweli hapa Serikali Hatuna. Yaani kama ingekuwa ni sumu mpaka leo ndio serikali inastuka, je wangekuwa watu wangapi wamepoteza maisha?
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,189
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona ueleweki kwa hiyo Babu wa Loliondo ni Chadema...unapinga kuwa sio tapeli?
   
 12. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mmmhhh wanaotaka kuchukua hatua wenyewe, na hao wanaosemasema ni waoga kichizi, tena babu kasema sasa atadili nao, shauri zenu mimi simo
   
 13. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,747
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Mchungaji Ambilikile Masapile "TAPELI", kuna haja ya serikali kuwamulika na wachungaji na so called "Manabii" maana wanajifanya kutibu watu kwa jina kwa jina la bwana kumbe wizi mtupu.

  Wakati mponda akikemea hili, baadhi ya viongozi wa dini wa kikristo walimjia juu wakidai ule ni ufunuo, kumbe ni ufunuo wa shetani.

  Kweli wajinga ndio waliwao!!!!!
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,189
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280
  Mkuu Babu wa Loliondo ni Tapeli hakuna mtu aliyepona.
   
 15. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli kabisa
   
 16. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,876
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Muulize William Lukuvi, Dr. Magufuli na Omar Mahita walikwenda kwa babu kufanya nini
   
 17. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  wakimpeleka mahakamani mimi nitajitolea kumtetea, huyu babu ni mzalendo hata bei yake ilikuwa ya kizalendo tsh 500 tu! aneyelalamika katapeliwa 500 aje nimrudishie: mh lyatonga mrema alitoa ushuhuda jinsi babu alivyomsaidia:

  wizara ya afya ndio ishitakiwe kwa kuingiza vipimo feki vya HIV na madawa feki ya malaria ambayo hayatibu!
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa kwa wenzetu serikali nzima ingeachia ngazi. Huwezi kuachia watu watumia dawa then baadae ndio unasema ni utapeli!
   
 19. r

  radica Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo mmechemka, mlikua wapi siku zote. Acheni kumdhulumu babu wa watu, mwacheni akae na michango yake. By the way nani ambae sio tapeli awe wa kwanza kunyoosha mkono?
   
 20. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Kekundu kekundu!
   
Loading...