Pole kwa yaliyo kukuta. Ninajua utakuwa na hasira kwani tukio zima linachukiza. Ila ndugu yangu suluhisho unalolifikiria nalo nitatizo kubwa zaidi. Hivi unajua sheria ya ndoa inasemaje kuhusu kuishi na mwanamke kinyumba kwa zaidi ya mwaka au miwili? Huyo house girl/muhudumu/mwajiriwa atakuwa automatically ni mke wako. Mkataba wenu utakapo ishia ndipo sheria itakapo anzia. Na kwa kuwa umeamua kufanya kazi kwa bidii ina maana utakuwa na mafanikio makubwa ambayo mtagawana tena na bi dada pindi mkataba wake ukiisha. Baada yapo utaajiri mwingine?
Tafakari kabla ya kuchukua hatua. Hapo ndipo huwa anahitajika Maombi kwa mwenyezi Mungu akujalie upate mke mwema. Bila shaka itakubidi nawewe uwe Mume mwenye akili ili maeisha yaende. Kila la kheri.