Mkuu, yawezekana kabisa ..hata kule kijijini wengine tulikulia migongoni mwa akina mama zetu wakati wakihangaika na mapishi au kuuza pombe (komoni, Kindi, chimpu na Kangara). Hakika wazazi waliweza kutupa pombe wakati huo. Ila kwa dhana ya malezi, kumpa mtoto ulevi kwa maana yeyote ile ni kumwaribu huyo mtoto. Hii ni sawa na kumwacha mtoto kuanza mapenzi mapema kabla ya umri, japo tendo husika ni "tamu" na pengine halina madhara ya moja kwa moja, lakini kwa ubongo wa mtoto haitamchukua muda kabla hajaharibikiwa. Waweza kulinganisha hata na baadhi ya watu wazima wenyewe wanavyoharibikiwa kutokana na kutumia vileo.Ngoshwe,
Usisikitike sana. Watoto wangu walipokuwa wadogo walikuwa wakipenda kuonja Heineken yangu. Niliwaachia kwa sababu bia pia ina protein.
Lakini ukubwani wote hawajageuka kuwa walevi. Wananiangalia tu nikibighua bia zangu na mwingine ananiuliza " Dad why do you like beer so much?
Ngoshwe,

Tunawafundisha nini watoto wetu Bandugu?. Ni mzazi wa Kitanzania, anatundika picha ya mwanae hewani hivi ili walimwengu waone jinsi aleavyo mwanae.
Huyu mtoto hajui afanyalo na akikua kwa maadili haya, mzazi atakuwa na haki ya kumkea mtoto kama huyu?.Hivi ile Sheria ya Watoto (The Children Act, 2009 http://www.africa.gnrc.net/mm/file/positionpapergnrc.pdf) ina maana yeyote kwa Watanzania kama ilivyo kwa wenzetu Ulaya na Marekani ? Tokea imetingwa mwaka Jana 2009, sijapata kusikia makali yake hata kidogo japo ilisemekana itazuia mambo kama haya ikiwemo kupiga vita tabia za wazazi kuwatuma watoto baa au kuingia nao Baa na kumbi za starehe .