saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 5,677
- 7,811
Vyuo vikuuu vya private kasoro Saint Augustin vinatakiwa vifungwe havina sifa ni uhuni, chuo Lecturer anafundisha masomo mpaka Sita tena siyo profession yake anajisomea. Pili, unakuta chuo hakipeleki makato ya pensheni au km kinapeleka kinagawa mshahara mara 2 makato yanafanyika ktk nusu ya mshahara hatimaye unakuta mshahara au pensheni ya anayeitwa mhadhiri wa chuo kikuu ni madogo kuliko mwl wa shule ya msingi. Tatu kodi za serikali hazilipwi kwasababu kinachokatwa kodi ni nusu ya mshahara ambao kwanza ni mdogo sana! ni vyuo vinavyonyanyasa sana watanzania kisa ukosefu wa kazi. Imagine ndugu mtanzania Asisstant Lecturer analipwa mshahra wa Millioni moja tu na anatakiwa atulie km ataleta za kuleta asubiri kufukuzwa bila taarifa unakuta tu hauna mshahara. Unatakiwa ufunishe masomo sita kwa semester ukikataa tegemea kiama chako, vina kiburi hawajui serikali. ajira zenyewe za kikabila, kirafiki, kikanda, chukua mfano wa Chuo Kikuuu Makumira Serikali ikafanye uchunguzi ni uchafu umejaa pale. Unakuta idara au hata faculty ina Mhadhiri moja na kwa mshahara wa Tshs 1M anatakiwa afundishe masomo sita ambayo hajayasomea. Kwanza Lecturer anatakiwa awe na eneo lake la ubobevu (profession), hata sheria huwezi kufundisha masomo yote km ni administrative law au contract law au criminal ndio eneo lako. Nenda hivyo vyuo ujionee halafu hawajui cha serikali, TCU, wala wizara. Waziri mama Ndalihako wasaidie watanzania wenzako tunakuamini!