Imefika wakati wa kuilinda nchi yetu na Katiba yake kwa wivu kabisa

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,194
5,598
Siasa za CCM na CHADEMA, siasa za Vyama zisiwe sababu ya kuinajisi nchi hii. Nchi hii sio ya MBOWE wala ya NDUGAI, nchi hii ni yetu Watanzania. Hapa Tanzania ni kwetu hatuna pengine pakupaita Nyumbani isipokuwa hapa, Tanzania.

Leo Job Ndugai anaongea hadharani bila kupepesa kuwa atainajisi katiba, Watanzania tunafurahi, Job Ndugai ni nani nchi hii Dhidi ya Nchi yetu na utaifa wetu? Haiwezekani.

Ndugai atapita, CCM itapita, CHADEMA itapita, Nchi hii itabaki, itakuwepo kwaajili yetu, watoto wetu na vizazi vyao, tunapaswa kuilinda nchi hii kwa wivu kabisa pamoja na misingi yake ikiwemo katiba

Binafsi nimeumia sana kusikia kauli za Ndugai, nimejiuliza kwa sauti Ndugai ni nani dhidi ya Taifa hili? U- CCM wake, U-CHADEMA wao, hauwezi kuwa sababu ya kunajisi miongozo ya nchi hii.

Kama leo anasimama mtu mmoja, mdogo sana kwa kiburi anajinasibu kuiharifu KATIBA, iliyo msingi wa Taifa letu. Kesho ataibuka mtu, ataamuru wanaume wa Nchi hii waolewe na itakuwa. Tusipopinga mambo madogo yaliyo haki yetu ipo siku hatutakuwa Raia wa Nchi hii kwa Amri ya Kiongozi mmoja wa Siasa.

Nimeumia sana Leo. Ni Muda wa kusimama, nakusema imetosha. Vyama vimenyane wawezavyo, ifikiapo suala la Taifa letu. WAKOME. kuwe na Kiasi.
 
Adui mkuu wa katiba yetu yupo nyuma ya spika.! Nadhani hata hilo jina spika maana yake ndiyo hiyo.
 
Kuna haja waTanzania tubadilike Mambo ya kitaifa tujadili Kama taifa mambo ya uvyama tuachane nayo kwenye Mambo ya kitaifa.

Utawala wa sheria Tanzania umekengeuka. Katiba inasiginwa kwanzia kwa Raisi, mahakama,bunge Tunakoelekea Ni Gizaa.
 
Back
Top Bottom