Imechukua muda gani kutoboa katika biashara yako? Umejifunza nini?

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
806
1,530
Wakuu hebu fungukeni ni miaka mingapi upo kwenye biashara na je, umefanikiwa kutoboa kibiashara? Na, ulifanyaje kufika hapo.

Nina kaduka kangu mwaka wa tano huu sioni dalili ya kutoboa japo sijakata tamaa ila changamoto ni nyingi sana ikiwemo madeni na mtaji kiduchu bado napambana. Je, wewe hali kwako ipoje?
 
Wakuu hebu fungukeni ni miaka mingapi upo kwenye biashara na je umefanikiwa kutoboa kibiashara? Na ulifanyaje kufika hapo.

Nina kaduka kangu mwaka wa tano huu sioni dalili ya kutoboa japo sijakata tamaa ila changamoto ni nyingi sana ikiwemo madeni na mtaji kiduchu bado napambana. Je wewe hali kwako ipoje?
Nilifungua duka baada ya kumaliza chuo. Mwanzo biashara ilianza vizuri lakini baada ya miezi miwili matzo yalishuka sana, huku jirani yangu akipata wateja wengi zaidi. Nikaamua kufunga biashara.
 
Wakuu hebu fungukeni ni miaka mingapi upo kwenye biashara na je umefanikiwa kutoboa kibiashara? Na ulifanyaje kufika hapo.

Nina kaduka kangu mwaka wa tano huu sioni dalili ya kutoboa japo sijakata tamaa ila changamoto ni nyingi sana ikiwemo madeni na mtaji kiduchu bado napambana. Je wewe hali kwako ipoje?
Wanaokutegemea ni wangapi? Katika hiyo miaka mitano kuna plot umenunua au kujenga nyumba?

Biashara ikiwa ndogo unatakiwa uwe bahili kupindukia na usiwe mtu wa kutoa hela hovyo. Wale manabii feki wanaosema toa upate baraka piga chini kwasababu hata Mungu anaona hali yako. Pia usijenge wala kununua plot wakati bado biashara haijaimarika. Yaani kama miaka minne ya mwanzo weka akili na roho yako yote kwenye kukuza biashara.

Mimi sijatoboa ila biashara ya duka la nguo na viatu (boutique) nilianza 2021 nimefanikiwa tu kukuza mauzo hadi kufika wastani wa laki nne kwa siku. Bado napambana. Nikifika laki 5 kwa siku ndo nitafikiria mambo mengine binafsi.
 
Nilianza biashara ya huduma ya maaabara ,2016' 2017,ikafa nikaanza tena 2019 February,octoba ikafa ,2021 nikaanza tena napo ikafa mwaka huohuo ,niliamua kuhama mkoa 2022 mwishoni 2023 mwanzoni nilikopa mkopo kwa ndugu kama 2.5 nikaongezea April nilifungua mkoa niliopo naona kidogo kwa sasa dalili za kuimarika zimeonekana maana hata mkopo nimebakiza kiasi kidogo kumaliza na badhii ya mengi ambayo niliyokwama kwa sasa nayatatua kirahisi .
 
Nilifungua duka baada ya kumaliza chuo. Mwanzo biashara ilianza vizuri lakini baada ya miezi miwili matzo yalishuka sana, huku jirani yangu akipata wateja wengi zaidi. Nikaamua kufunga biashara
Kwanini hukuvumilia huenda ni kipindi tu kingepita ukarudi kwenye ubora wako
 
Wanaokutegemea ni wangapi? Katika hiyo miaka mitano kuna plot umenunua au kujenga nyumba?

Biashara ikiwa ndogo unatakiwa uwe bahili kupindukia na usiwe mtu wa kutoa hela hovyo. Wale manabii feki wanaosema toa upate baraka piga chini kwasababu hata Mungu anaona hali yako. Pia usijenge wala kununua plot wakati bado biashara haijaimarika. Yaani kama miaka minne ya mwanzo weka akili na roho yako yote kwenye kukuza biashara.

Mimi sijatoboa ila biashara ya duka la nguo na viatu (boutique) nilianza 2021 nimefanikiwa tu kukuza mauzo hadi kufika wastani wa laki nne kwa siku. Bado napambana. Nikifika laki 5 kwa siku ndo nitafikiria mambo mengine binafsi.
Wategemezi ni wengi sana mkuu japo nafumba macho najifanya kama siwaoni lakini pia naona hatua ni zilezile nilijaribu kusave lakini bado mwendo hauridhishi naona miaka mingi mbele
 
Nilianza biashara ya huduma ya maaabara ,2016' 2017,ikafa nikaanza tena 2019 February,octoba ikafa ,2021 nikaanza tena napo ikafa mwaka huohuo ,niliamua kuhama mkoa 2022 mwishoni 2023 mwanzoni nilikopa mkopo kwa ndugu kama 2.5 nikaongezea April nilifungua mkoa niliopo naona kidogo kwa sasa dalili za kuimarika zimeonekana maana hata mkopo nimebakiza kiasi kidogo kumaliza na badhii ya mengi ambayo niliyokwama kwa sasa nayatatua kirahisi .
Unapambana sana mkuu haukati tamaa big up
 
Biashara muisikiage tu, Ina utamu kupitiliza lakini pia ina machungu kupitiliza kiasi kufikia mtu anafirisika anakuwa empty kabisa.

nikaona wazi kabisa siwezi biashara ntagonga 50 sina hata kiwanja.

nilivipukuta vumbi vyeti vyangu, kwa mbinde nikaingia rasmi kwenye maisha ya utumishi

uzuri wa kufanya biashara kabla ya ajira ni kwamba kuna uzorfu unao, hii kitu imenisaidia niendelee na game bila nikiwa nayajua mazingira na changamoto zake, huwa naona wenzangu wanachukulia mambo easy sana ma kuiga iga, mwisho wa siku mradi unafeli benki inamkwangua marejesho ambayo hayajazaa matunda
 
Biashara ni changamoto hasa kwa tunaoanza mavumbini kutoboa ni kazi
 
Wakuu hebu fungukeni ni miaka mingapi upo kwenye biashara na je umefanikiwa kutoboa kibiashara? Na ulifanyaje kufika hapo.

Nina kaduka kangu mwaka wa tano huu sioni dalili ya kutoboa japo sijakata tamaa ila changamoto ni nyingi sana ikiwemo madeni na mtaji kiduchu bado napambana. Je wewe hali kwako ipoje?
Achana kwanza na kutoboa, biashara kusimama na kuweza kujiendesha yenyewe huwa ni mziki.

Mwanzo tuliweka mtaji wa kutosha tukijua ndio dawa, lakini ikawa ndivyo sivyo. Siku zinaenda ila biashara ni mwendo wa kobe. For almost 1 year tuna fight biashara isife au isijiendeshe kwa hasara. Kidogo tulipoanza kuona mwanga, tukainduce tena capital ili kuiboost. Sasa hivi walau dalili ni njema. Kinachotusaidia tumekubaliana hakuna mtu kuitolea macho biashara, hivyo kinachopatikana kinarudishwa kwenye mzunguko.

Changamoto ya biashara, usipoifanya kihalali, unakumbana na polisi. Ukiifanya kihalali, unakutana na TRA. Na wote ni wasumbufu kuliko kawaida
 
Back
Top Bottom