Asante kwa Kuchangia baba mtu, tarehe 31 october usisahau kumpigia Kura ya Ndio Dr. Wilbroad Slaa"Kila kitu kimefanywa na wewe. Wee ndiye ulokutana na huyo rafiki yako. Wee ndiye unaotueleza kile alichosema rafiki. Baada ya kutueleza hivyo, ni juu yetu sie kuamini au kutoamini hayo ulotueleza. Huna haja ya kumlazisha mtu aamini kile ulichokisema wee pamoja na huyo rafiki yako. Na pia huna haja ya kumtukana mtu. Umetumia kipimo cha aina gani hata ukagundua kiwango cha akili alonacho malaria sugu????"
Wakuu juzi nilisikia kati ya ahadi zake kule Mlandizi ni kuwa amefanya mazungumzo na waisraeli kuja kulima nyanya kwenye bonde la mto RUVU.
1. Je hii inawezekana au ni ghiliba tu za mkulu ili apate kura?
2. Je anafahamu kuwa huo mto ni chanzo cha maji yanayotumika Bagamoyo, Dar na Kibaha na kwamba uwekezaji wowote mkubwa katika secta ya kilimo ungeathiri maisha ya watu wengi wanotegemea mto huo?
3. Je anafahamu madhar ya kimazingira yanayoambatana na matumizi ya viatilifu katika kilimo (kemikali)?
4. Je at what point of the river hicho kilimo kitafanyika?
5. Je kwa nini NAFCO walishindwa kuendesha mashamba yale ya zamani?
6. Je Kikwete anatumia ujinga wa ndugu zake kuwadanganya ili apate kura wakati akijua fika kuwa anawadanganya?
7. Je kwa style hii ya ngonjera za ahadi za kikwete tutafika?
Mungu ibariki Tanzania
Nafikiri hili siyo jambo geni!asilimia kubwa ya watanzania wanalifahami hili,hata wenzetu walio CCM wanalifahamu hili!Wakati umefika tufanye mabadiliko!
Muda mwingi aliutumia kwa safari za nje zisizo na tija na kusahau kazi yake ya msingi.Ulimwengu wa sasa wa mawasiliano ya kisasa kama video conference nakadhalika yangemrahisishia kazi na kupunguza gharama,bado ana mabalozi,na waziri wa mambo ya nje.Sijui kama Raisi wetu amejifunza kitu toka kwa wananchi anaongoza,Wananchi hawadanganywi kama mtoto mdogo na peremende,wanataka Raisi afanye kazi ya Uraisi sio kazi ya vipeperushi.Ni bahati mbaya atakumbukwa kama Raisi aliyetoa ahadi nyingi nakushindwa kuzitekeleza kifasaha.kuna washauli wake wanamhalibia jamani mi naona kama siyo akili yake vile! na usisahau Reli toka tegeta mpaka posta, barabara za juu ameludia tena. WATAKAO MCHAGUA VILAZA SANA HAO BORA YA YEYE!
Juzi nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye anafanya kazi usalama wa taifa! tulikuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu, dakika za mwisho kabla ya kuachana nilifurahi nilipoona jamaa kakiri mbele yangu kwamba " Anatambua ya kuwa watu wengi wamepoteza matumaini na serikali iliyoko madarakani" na huo ndo ukweli!
Halafu wakishamtoa JK nani aongoze nchi?Mbowe/Slaa,Zitto, Mnyika au Mdee?kwa akili yenu JK ndo kasababisha mfumuko wa bei?ili umsaidie nini?tafuteni suluhisho sahihi la matatizo si kulaumu mtu binafsi kwenye suala kama hili.Imeshakuwa wimbo sasa kila kitu JK?Kumuondoa Jk si suluhisho.