I'm not happy with my life

I'm not happy with my life

iko hivi si kosa lako baba yako kutowajali,wala si kosa lako ndugu zenu kutowajali

Kosa lako ni kuendelea kuuumia kwa mambo ambayo huwezi kuyabadilisha sasa,kosa lako ni kujua kwamba kuna mambo ukiyawaza yanakuumiza lakini bado unaendelea kuyawaza

The moment ukiyajua haya makosa yako na kukubali kwamba unakosea kuendelea kuyakumbatia haya mambo basi itakuwa mwanzo mpya wa ukombozi wa nafsi yako na roho


my dear huzuni hazitakusadia chochote,kulaumu baba yako haitabadilisha chochote,ndio amewakosea lakini you have to move on

All the best
 
Sijui ni lini na mimi ntakuwa na furaha maishani, Furaha yangu ilitoweka pasipo kujua baada ya kumpoteza mama yangu miaka mingi iliyopita nikiwa bado mdogo sana.

Maisha niliyopitia kutoka kwa ndugu, mama wa kambo pamoja na baba asiyejali yananipa hasira sana, sijui hata nimlaumu nani kuzaliwa kwenye hii familia, huu ukoo na huyu mzazi ambaye hakutaka kabisa kusimamia nafasi yake na kutimiza majukumu yake ya malezi ipasavyo kwetu sisi watoto wake.

Natamani kama kungekuwa kuna Dunia nyingine ambayo haitakuwa na binadamu niende nikaishi huko nipotelee nisionekane na mtu yoyote kila mtu asahau kuhusu mimi.

R.I.P mom ulikuwa mpambanaji ukahakikisha kaka amesoma na amemaliza chuo kupitia ujasiriamali wako mdogo mdogo uliokuwa ukifanya, matokeo yake huyu kaka uliyempambania leo hii hakumbuki wadogo zake ametuacha tuteseke peke yetu, hata leo hii simu zake hazipatikani amekuwa addicted na pombe hadi anashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Pengine ungekuwepo mom nisingepita nilikopita ungenifundisha vingi vizuri na imani pia ungenipambania, wala usingeniacha niteseke kama alivyofanya baba. Nasikitika sana kwanini umeondoka nikiwa bado mdogo, bado nakuhitaji mama yangu😭😭

Kwanini Mungu ameruhusu hili litokee kwangu, kuna muda huwa najiuliza hivi Mungu huwa anaona mateso na matatizo yetu tunayopitia sisi wanadamu, huwa namlaumu sana Mungu kuniondolea mama yangu kipenzi nikiwa mdogo, namlaumu pia kuruhusu mateso yawe sehemu ya maisha yangu, kunipa baba asiyejali watoto wake.

Ninahisi kumchukia baba yangu, hata akinipigia simu sifurahii kabisa, hata kwenda kumsalimia hadi anikumbushe au tu hiyo siku nijisikie mwenyewe. Lakini nimemsamehe kwa yote aliyoyafanya maishani mwangu japo moyoni mwangu naumia sana kila nikiyafikiria maisha yangu yaliyopita.

Natamani hata wakati ule mama yangu angebaki ningetanguliaga mimi, najitahidi kuwa na furaha lakini nikikaa mwenyewe furaha yote inatoweka.

Nawezaje kuondokana na haya maumivu yaliombatana na chuki kwa ndugu zangu?
Jipiganie mqenyewe dunia hii hakuna baba, mama, kaka dada, mjombq, shangazi, ndugu, jamaa, rafiki na mwingine yeyote anayefanana nao anayelazimika kukupigania wewe.

Ukishajua kanuni hii utakubali mambo ya walimwengu na kujipigania mwenyewe.

Usipoelewa utabaki mtu wa kulialia daima.
 
Kila kitu wewe unajiweka kando, lawama unawatupia watu wengine.

Jitathmini binti, una mengi yasiyopendeza na unayafisha na bila shaka huna wa kukwambia hili ni baya, huombi ushauri ama lah huna marafiki wazuri.

Nyuzi zako nyingi wewe ni mlalamika usie ma hatia, ulieonewa, hukustahili hayo na vitu kama hivyo.

Tathmini madhaifu yako, hapo ndipo utapata ushupavu wako, acha kulialia kila siku, hamna alieumbwa ili aje ampe kiss ov love furaha, si ajabu hata mama yako nae asingefanya hivyo unavyodhani angefanya.

Jukumu la furaha yako liko mikononi mwako mwenyewe, sio baba, mama, kaka, ndgu wala boyfriend.

Makinika, utapotea, shaurilo, huko kutia huruma kuna wasio na huruma wanawahitaji ninyi watia huruma ili wawalize vizuri.
 
wewe ni mvivu wa kazi unataka kaka yako abebe majukum yako, watu ka wewe nme kutana nao sana wao kufanya kazi ahaha kaka abebe mzigo inafika hattua mtu una kazi nzuri tu lakini hadi mchele kilo moja unakopa kwa mangi kisa mzigo wa ndug fanya kazi wewe ni mvivu mnawaumiza vijana sana mtu anakazi ila ukiyaangalia maisha yake mpaka unamhurumia kumbe ndugu fc wanafanya yao..

fullstop, kwishaaaa
 
wewe ni mvivu wa kazi unataka kaka yako abebe majukum yako, watu ka wewe nme kutana nao sana wao kufanya kazi ahaha kaka abebe mzigo inafika hattua mtu una kazi nzuri tu lakini hadi mchele kilo moja unakopa kwa mangi kisa mzigo wa ndug fanya kazi wewe ni mvivu mnawaumiza vijana sana mtu anakazi ila ukiyaangalia maisha yake mpaka unamhurumia kumbe ndugu fc wanafanya yao..

fullstop, kwishaaaa
Mpaka akili ije kumkaa sawa kua kaka yake nae ana maisha yake na yeye pia ana yake basi inaweza kua kachelewa kisa kuwalaumu wengine ilhali tayari yuko above 20 yrs, bado analalamika fulani hanisaidii, fulani hanijali, fulani hanipi furaha.
 
Bas ni sawaa!!
Kuna wengi wamelelewa na Bibi na babu. Au bibi pekeyake na maisha yakasonga tu.

Ukishapata ufahamu na Ukipewq nguvu basi yaliobaki ni kujipambania.

Kuna msemo unasema
"Hard times create strong men, strong men create good times, good times create weak men, weak men create hard times"
 
Back
Top Bottom