I'm not happy with my life

I'm not happy with my life

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,363
Reaction score
16,092
Sijui ni lini na mimi ntakuwa na furaha maishani, Furaha yangu ilitoweka pasipo kujua baada ya kumpoteza mama yangu miaka mingi iliyopita nikiwa bado mdogo sana.

Maisha niliyopitia kutoka kwa ndugu, mama wa kambo pamoja na baba asiyejali yananipa hasira sana, sijui hata nimlaumu nani kuzaliwa kwenye hii familia, huu ukoo na huyu mzazi ambaye hakutaka kabisa kusimamia nafasi yake na kutimiza majukumu yake ya malezi ipasavyo kwetu sisi watoto wake.

Natamani kama kungekuwa kuna Dunia nyingine ambayo haitakuwa na binadamu niende nikaishi huko nipotelee nisionekane na mtu yoyote kila mtu asahau kuhusu mimi.

R.I.P mom ulikuwa mpambanaji ukahakikisha kaka amesoma na amemaliza chuo kupitia ujasiriamali wako mdogo mdogo uliokuwa ukifanya, matokeo yake huyu kaka uliyempambania leo hii hakumbuki wadogo zake ametuacha tuteseke peke yetu, hata leo hii simu zake hazipatikani amekuwa addicted na pombe hadi anashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Pengine ungekuwepo mom nisingepita nilikopita ungenifundisha vingi vizuri na imani pia ungenipambania, wala usingeniacha niteseke kama alivyofanya baba. Nasikitika sana kwanini umeondoka nikiwa bado mdogo, bado nakuhitaji mama yangu😭😭

Kwanini Mungu ameruhusu hili litokee kwangu, kuna muda huwa najiuliza hivi Mungu huwa anaona mateso na matatizo yetu tunayopitia sisi wanadamu, huwa namlaumu sana Mungu kuniondolea mama yangu kipenzi nikiwa mdogo, namlaumu pia kuruhusu mateso yawe sehemu ya maisha yangu, kunipa baba asiyejali watoto wake.

Ninahisi kumchukia baba yangu, hata akinipigia simu sifurahii kabisa, hata kwenda kumsalimia hadi anikumbushe au tu hiyo siku nijisikie mwenyewe. Lakini nimemsamehe kwa yote aliyoyafanya maishani mwangu japo moyoni mwangu naumia sana kila nikiyafikiria maisha yangu yaliyopita.

Natamani hata wakati ule mama yangu angebaki ningetanguliaga mimi, najitahidi kuwa na furaha lakini nikikaa mwenyewe furaha yote inatoweka.

Nawezaje kuondokana na haya maumivu yaliombatana na chuki kwa ndugu zangu?
 
Pole sana na changamoto kiss ov love .
Maisha ndivyo yalivyo.
Cha Muhimu ni kuangalia nyuma na kujifunza na sio Kukata tamaa.

Anzia ulipo na upambane kutengeneza Maisha yako ya mbeleni.

Pia Wasamehe Baba Na huyo kaka Yako, Chuki inakuharibu zaidi ww kuliko wao. Kwahiyo haina maana kuipa kipaumbele.

Muombe Mungu wako akupe nguvu ujasiri wa kuendelea na maisha yako (with or without Baba na huyo kaka yako).

Bora ww una kaka na Baba (hata kama hawakujali) ila kuna weng wamelelewa na bibi na babu. Na maisha yakasonga.

Panga maisha yako. Wasamehe ndugu zako na Songa mbele.
 
Dunia imejaa watu weak sana siku hizi.

Huyo kwanza ni dume anajidai KE

hapo ndo shida inapoanzia, ukishajiona mnyonge unaona kulialia ni haki yako.

Unakaa unawalaumu wengine wakati maisha yako ni 100% jukumu lako.

Acha uzwazwa wewe, jikomboe au jinyonge, the choice is yours.
 
Ktk kitu nashukuru, ni kupewa hawa wazazi nilionao, huwa nawaza wasingekua hawa, ingekuaje kwa upande wangu?
Kuna wengi wamelelewa na Bibi na babu. Au bibi pekeyake na maisha yakasonga tu.

Ukishapata ufahamu na Ukipewq nguvu basi yaliobaki ni kujipambania.

Kuna msemo unasema
"Hard times create strong men, strong men create good times, good times create weak men, weak men create hard times"
 
I Cried because I had no Shoes...; Sage words Indeed...

Anyway tafuta hobbie (purpose) na tumia muda na nguvu kufanya hicho / kukidhi hio purpose... vilevile hata kwa sisi ambao sio Watu wa Imani kuna some Wisdom kwenye hizo Imani.... (Peace of Mind)

God grant me the serenity
to accept the things I cannot change;
courage to change the things I can;
and wisdom to know the difference.

Living one day at a time;
enjoying one moment at a time;
accepting hardships as the pathway to peace;
taking, as He did, this sinful world
as it is, not as I would have it;
trusting that He will make all things right
if I surrender to His Will;
that I may be reasonably happy in this life
and supremely happy with Him
forever in the next.
Amen.​
 
Dunia imejaa watu weak sana siku hizi.

Huyo kwanza ni dume anajidai KE

hapo ndo shida inapoanzia, ukishajiona mnyonge unaona kulialia ni haki yako.

Unakaa unawalaumu wengine wakati maisha yako ni 100% jukumu lako.

Acha uzwazwa wewe, jikomboe au jinyonge, the choice is yours.
😂😂😂😂 hapo kwenye kujidai kuna shida
 
Poleee sana Dear!

Ktk kitu nashukuru, ni kupewa hawa wazazi nilionao, huwa nawaza wasingekua hawa, ingekuaje kwa upande wangu?

Pambana dear, iko siku utafurahia kusudi na uwepo wako hapa Duniani.
Uko sahihi, kuna wengine wana wazazi kabisa na bado wana maisha kama hayo hayo tu! Swala ni kumove on na kupambana akiwa busy na kazi au familia hatopata muda wa kuwaza hayo yote!

Maisha saivi ni magumu sana! Kuna muda unakosa ata wa kumlaumu! Ukikuwa unaona kawaida tu na unapambana, ila kama bado anakuwa ataona kama kila mtu anamtenga!mamaanGu mfanya biashara mkubwa tu, lakini mi nakomaa mwenyew na sijasaidiwa na mtu!

Kwahiyo kiss ov love usione kama jua linakuwakia mwenyewe! Jipe muda muda dear utakaa sawa, hatushindani maisha kwamba nani anateseka kuzidi mwenzie lakini jipe muda, Time heals, kila mmoja ana namna anavyochukulia mambo kulingana na mazingira! Pambana kwa moyo wote bila kinyongo usiangalie sijui nani hakukusaidia kipindi unatafuta utaona kawaida na hutokaa ukamlaumu mtu! Anza upya hama ata maeneo ulipo ilimradi tu uweze kuanza moja! Pole sana la mama❤️
 
Punguza kulalamika,nyuzi zako nyingi ni kulalamika tu,
Kulalamika hakuwezi kuibadili hali yako,mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe kwa kubadili fikra zako,

Dunia haina huruma,Dunia ya leo inataka ubishi na ujasiri wa kupambana,
Hizi pole utakazo pewa hapa haziwezi kubadili chochote,

Mama yako aliplay part yake,now it's your turn,
Maisha ni yako,pambana kivyako,life is very short,acha kuishi kinyonge.
 
🤝🤝🤝 thread ifungwe....

Mida ya lunch hii wachangiaji wote na Seran wakale ugali....Evelyn salt na min -me wakale wali
 
Mwisho wa siku lazima maisha yaendelee......

Yalitokea ukiwa mdogo,sasa ushakua mkubwa simama kwa miguu yako songa mbele, hata ukikaa kuwalaumu watu haisaidii kitu
Sure, hakuna namna ni lazima kuishi na kuishi ni lazima kupambana kwa kusimama na miguu yako mwenyewe.

Na tunakoendea maisha yatazidi kuwa tough sana, yaani haturudi nyuma, life linazidi kuwa tough...
 
Pole sana. Huku kuna watu wema tu. Endelea kupokea comments kuna watu wema watajitokeza kukusaidia. Ushauri wangu, wasamehe wote waliokukosea na wewe mwenyewe ujisamehe na anza kumtafuta Mungu akuonyeshe njia. Mungu ajakuacha. Nenda kwenye nyumba za Ibada watakupa maneno ya Mungu ya faraja.
 
Sijui ni lini na mimi ntakuwa na furaha maishani, Furaha yangu ilitoweka pasipo kujua baada ya kumpoteza mama yangu miaka mingi iliyopita nikiwa bado mdogo sana.

Maisha niliyopitia kutoka kwa ndugu, mama wa kambo pamoja na baba asiyejali yananipa hasira sana, sijui hata nimlaumu nani kuzaliwa kwenye hii familia, huu ukoo na huyu mzazi ambaye hakutaka kabisa kusimamia nafasi yake na kutimiza majukumu yake ya malezi ipasavyo kwetu sisi watoto wake.

Natamani kama kungekuwa kuna Dunia nyingine ambayo haitakuwa na binadamu niende nikaishi huko nipotelee nisionekane na mtu yoyote kila mtu asahau kuhusu mimi.

R.I.P mom ulikuwa mpambanaji ukahakikisha kaka amesoma na amemaliza chuo kupitia ujasiriamali wako mdogo mdogo uliokuwa ukifanya, matokeo yake huyu kaka uliyempambania leo hii hakumbuki wadogo zake ametuacha tuteseke peke yetu, hata leo hii simu zake hazipatikani amekuwa addicted na pombe hadi anashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Pengine ungekuwepo mom nisingepita nilikopita ungenifundisha vingi vizuri na imani pia ungenipambania, wala usingeniacha niteseke kama alivyofanya baba. Nasikitika sana kwanini umeondoka nikiwa bado mdogo, bado nakuhitaji mama yangu😭😭

Kwanini Mungu ameruhusu hili litokee kwangu, kuna muda huwa najiuliza hivi Mungu huwa anaona mateso na matatizo yetu tunayopitia sisi wanadamu, huwa namlaumu sana Mungu kuniondolea mama yangu kipenzi nikiwa mdogo, namlaumu pia kuruhusu mateso yawe sehemu ya maisha yangu, kunipa baba asiyejali watoto wake.

Ninahisi kumchukia baba yangu, hata akinipigia simu sifurahii kabisa, hata kwenda kumsalimia hadi anikumbushe au tu hiyo siku nijisikie mwenyewe. Lakini nimemsamehe kwa yote aliyoyafanya maishani mwangu japo moyoni mwangu naumia sana kila nikiyafikiria maisha yangu yaliyopita.

Natamani hata wakati ule mama yangu angebaki ningetanguliaga mimi, najitahidi kuwa na furaha lakini nikikaa mwenyewe furaha yote inatoweka.

Nawezaje kuondokana na haya maumivu yaliombatana na chuki kwa ndugu zangu?
Pole sana, pitia hapa https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/w20010201/Unaweza-Kukabiliana-na-Kivunja-Moyo/
 
Sure, hakuna namna ni lazima kuishi na kuishi ni lazima kupambana kwa kusimama na miguu yako mwenyewe.

Na tunakoendea maisha yatazidi kuwa tough sana, yaani haturudi nyuma, life linazidi kuwa tough...
Unantisha mzee mwenzangu kwahiyo hapa mnyoosho bado 😂😂😂

The Icebreaker kwani huko mshahara wa beki tatu kiasi gani 😢
 
Back
Top Bottom