umenikumbusha,mwaka 2011 niko chuo mwaka wa kwanza,asa si unajua tena ile wenge ya bumu,mara paa nikakutana na binti mmoja kwa wakati huo alikua form six pale loyola,ebana mtoto alikua mkali yule,nikamtongoza na kweli mtoto nae akawa kanielewa sana,asa nikawa nashangaa mtoto ananibania kunipa papuchi while anasema ananipenda sana,na kilichokua kinanistaajabisha nilikua nikimwomba mchezo anakosa raha au anakua kama analia flani hivi,at first nilidhani labda ni kalelewa katika maadili flani hivi but i was wrong...so siku moja nikaamua kumpeleleza nimjue kiundani akanambia wazazi wake walishafariki wote na kwa wakati ule alikua analelewa na mama ake mdogo,kilichonifanya nianze kuchezwa na machale aliniambia vifo vya wazazi wake vilipishana mwaka mmoja tu,halafu ugonjwa uliowaua eti ni malaria,alarm ikagonga kichwani kuwa huenda wazazi walikufa kwa ngoma..anyway sikutilia maanani kivile,asa kuna siku tukawa tumepanga tena kukutana mahali ili nimtafune,ila cha ajabu binti akaja kavaa uniform za shule,yani alitumia hiyo technique ili nisiweze kumwingiza lodge coz wananchi wangeniijia juu kuwa natembea na mwanafunzi,ebana siku hiyo nilikasirika hatari,tukaagana usiku katika chatting na yeye akawa analia anasema nimsamehe tu yeye hawezi kufanya hicho kitendo ingawa ananipenda saana na anajiskia vibaya kunibania ila kuna siku ntaelewa kwa nini anakataa kufanya hivo..mara nikashangaa tena demu kaanza kusali makanisa ya walokole wakati alikua mlutheran mwenzangu..mwisho wa siku demu akaanza kuumwa hatari...kumbe alizaliwa na ukimwi bwana na alifariki 2013,i was next to her wakati anakata roho...na siku chache kabla ya kufa tuliongea nae ndo akanambia she real loved me ndo maana hakutaka kuniua...since then nimejifunza,huwa sifanyi ngono zembe kabisa maana niliishasalimika kifo..yule demu ingawa kafa lakini huwa namshukuru mpaka leo na upendo wake kwangu nauona kama ulikua wenye thamani kubwa sana...sidhani kama kuna mwanamke ashawahi kunipenda kama yule binti asee.