I'm gonna say it anyway! ...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Polisi 10 kizimbani kwa wizi

Habari Zinazoshabihiana
• Polisi kupambana na wanaoibia ATM 04.08.2007 [Soma]
• Meneja adaiwa kuiibia Celtel milioni 700/- 17.04.2007 [Soma]
• Wahasibu Mahakama Kisutu kizimbani wizi wa m.400/- 18.06.2008 [Soma]

Na George John, Musoma

ASKARI Polisi 10 mkoani Mara, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa na kusomewa mashitaka 12 ya uzembe, kula njama, uvunjaji na kuiba mali mbalimbali zinazomilikiwa na mgodi wa dhahabu wa MEREMETA na Buhemba Gold Mine (BGM).

Askari hao ambao juzi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. Liberatus Barlow, alitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini hapa za kufukuzwa kwao kazi, walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Bibi Janneth Musaloche.

Akisoma mashitaka yanayowakabili watuhumiwa hao jana, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Msaidizi Geofrey Mungujuna, aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa G1011 Konstebo Daud (21), G1012 Konstebo Deogratius, Mei 24 mwaka huu katika muda usiojulikana, walikula njama na kuvunja kontena na kuiba mali ya BGM.

Mwendesha Mashitaka huyo alidai kuwa washitakiwa hao hao kwa pamoja katika muda na mahali hapo hapo, walivunja kontena mbili zenye thamani ya milioni moja mali ya MEREMETA.

Alisema washitakiwa hao hao walifanya uzembe mahali hapo hapo wakijua kuwa kilichokuwa kikifanyika ni wizi walishindwa kuchukua hatua madhubuti za kukizuia.

Pia mshitakiwa wa tatu F7468 Konstebo Haji Nossoro(24) alidai kuwa Mei 25 mwaka huu mchana katika maeneo ya mgodi wa Buhemba, alikula njama na mtu aliyetajwa kwa jina la Sospeter Yohana na kuiba, na mshitakiwa huyo huyo Mei 6 mwaka huu katika eneo hilo aliiba CPU yenye thamani ya sh. 600,000 mali ya BGM.

Nao Washitakiwa G72 Konstebo John (23) na G909 Konstebo Said (22) kwa pamoja Mei 6 mwaka huu wakijua Kuwa Yohana alikuwa ameiba CPU inadaiwa walishindwa kuchukua hatua za kumkamata.

Naye mshitakiwa E5331 Konstebo Majaliwa anadaiwa kuwa Mei 15 mwaka huu muda usiojulikana, aliiba betri ya gari aina ya N200 yenye thamani ya sh. 400,000 mali ya BGM.

Katika mashitaka mengine askari namba E704 Konstebo Kiza (26) na G1012 Konstebo Deogratius wanadaiwa kwa pamoja walikula njama katika muda usiojulikana katika eneo la Buhemba waliiba.

Makonstebo Kiza na Deogratius wanadaiwa pia kuiba Rolapaneli mbili zenye thamani ya sh. 500,000 mali ya BGM.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kushindwa kuchukua hatua, huku makonstebo E 585 Raphael (44), F 4333 Prosper (28) na G 993 Peter kwa pamoja wakidaiwa kuwa Mei 7 mwaka huu saa 3 usiku walikula njama na kuvunja ofisi za MEREMETA/BGM na kuiba CPU sita na 5AC vyenye thamani ya sh. milioni 7.2.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao watatu huku wakijua kulikuwa na mpango wa kuvunja na kuiba lakini walishindwa kuzuia kufanyika kwa kosa hilo.

Washitakiwa wote walikana mashitaka dhidi yao na walitimiza masharti ya dhamana na wako nje hadi Agosti 20 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.


My Take:
Ukikuta kitu hakina mwenyewe, na ukauliza uliza mwenyewe ni nani hakuna anayejitokeza, basi ukikichukua hutakuwa umeiba, nyumbani wanasema "umeokota". Yes I said it; waachieni hawakuiba!! Unless watuambie wamemuibia nani; kama kitu kimechukuliwa kutoka meza iliyokutwa barabarani, basi mwenye meza ajitokeze na kusema meza ni yake na hicho kitu kilichokutwa juu ya meza ni yake. Kama hakuna mwenye mali basi hata meza inaweza kuchukuliwa vile vile!
 
Ukikuta kitu hakina mwenyewe, na ukauliza uliza mwenyewe ni nani hakuna anayejitokeza, basi ukikichukua hutakuwa umeiba

Concept yako inafanya kazi only kama hicho kitu kitakuwa kiko abandoned na aliyekuwa anakimiliki.

Lakini kama kitu hicho kitakuwa kimepotezwa (lost) na mmiliki, then ukikichukua utakuwa umefanya kosa linaloshabihiana na wizi.

Kwa hiyo, hata kama ukiuliza uliza kwa watu na hakuna atakayejitokeza kama mmiliki, bado utakuwa na ulazima wa kujua kama hicho kitu kiko "lost" au "abandoned" kabla huja kiweka kwapani na kuambaa nacho.
 
There are opinions and the law of the land.

What does the law of the land and the police code of ethics, if we have one, say?
 
Hakuna mmiliki wa Meremeta anayejulikana; na hakuna aliiyetayari kujitokeza kuwa ndiye mmiliki. Kama hapa Michigan, nikikuta burungutu la hela nikalisalimisha polisi, wanazo siku thelathini kwa mwenye nazo kuzidai, baada ya hapo; wananiita na kunipatia na ninakuwa "nimeokota".

Sasa sijui inakuwaje kwenye kampuni kubwa kama Meremeta isiyo na mwenyewe.
 
Hakuna mmiliki wa Meremeta anayejulikana; na hakuna aliiyetayari kujitokeza kuwa ndiye mmiliki. Kama hapa Michigan, nikikuta burungutu la hela nikalisalimisha polisi, wanazo siku thelathini kwa mwenye nazo kuzidai, baada ya hapo; wananiita na kunipatia na ninakuwa "nimeokota".

Sasa sijui inakuwaje kwenye kampuni kubwa kama Meremeta isiyo na mwenyewe.

Huyo huyo alikuwa kwenye registration paperwork za Meremeta ndiye "presumed" mmiliki.
 
kama Meremeta ni legally registered company basi hizo mali ni za mtu na huyo mtu jina lake ni "Meremeta"; na inatambulika kama mtu na inayo haki zake ambazo zinatofautina na haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom