Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

Mhafidhina, ujumbe mzito sana huu.

MMKJJ, siku utaandika postings zako kwa kuchambua pande zote mbili nitakuwa miongoni mwa wapenzi wa postings zako.

kwenye ufisadi hakuna pande mbili
Kwenye utawala wa sheria hakuna pande mbili,
kwenye kutaka maendeleo ya kweli na kuwajibika hakuna pande mbili,
Hakuna pande mbili kwenye kutaka sheria ifuatwe no matter what.

Pande mbili ziko kwenye majadiliano na mazungumzo na kubadilishana hoja; kwenye kutaka vitendo ni aidha unatenda au hutendi na ukitenda hakuna pande mbili, na usipotenda hakuna pande mbili kwani zote ni pande moja!
 
MKJJ....!

Nakubaliana na mawazo yako lakini naomba ujaribu kuangalia na upande mwingine wa shilingi....!

Hivi umeshawahi kujiuliza kazi za Raisi ni nini haswa? Naomba usome katiba ya Jamhuri wa Muungano ndo utajua kazi za Rais....! Kazi za Raisi sio za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya Rais ni usimamizi wa serikali pamoja na kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa...!

Aidha, kuongoza nchi sio kama kuongoza kampuni ambapo unaweza ukatoa amri asubuhi na ikatekelezwa hapo hapo...! Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!

Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!

Pia Unapokua raisi changamoto ni nyingi sana na mambo ni mengi sana tena kwa wakati mmoja....! Jaribu kufukiria kwamba unakua Raisi halafu kuna wizara 22 (Mambo ya ndani, maji, mifugo, sheria na katiba, elimu, afaya, fedha, mambo ya nje, miundombinu, sayansi etc) ziko chini yako na kila moja inamatatizo makubwa ya kutolea maamuzi tena maamuzi mzito, usipokua makini, ndio hivyo unaweza ukaishia kuwa dictecta kwa sababu utataka kufanya maamuzi ambayo utataka kuona matokeo yake mara moja...!

Kwa mfano, mimi nilimuelewa sana Kikwete alipozungumzia suala la kiwafukuza kazi wale walihusika kwenye EPA, embu chukulia kama Kikwete angekua na hasira/maamuzi ya haraka haraka akamua kuwafukuza kazi wale wote waliotajwa kule ndani, sio kwamba angwafaidisha kwani wangeenda kufungua kesi kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria?

Mimi naomba uwe unajaribu kujiweka kwenye viatu vya Kikwete na sio ku-mcritisize tu, jaribu kuchuukulia kama wewe ungekua Rais je ungekutwa na changamoto kama anazokumbana nazo wewe ungekua unafanya nini au ugeamuaje? Pia jaribu kuangallia kwamba tanzania ni nchi changa, nilikua nasoma takwimu za taifa jana, nikaona kwamba kati ya watu milioni 38.9 tuliopo tanzania, ni wananchi laki nne tu wenye digree moja...! Hizi takwimu zilikua zinafanya estimate kwamba tokea uhuru watu waliograduate unversity walikua ni watu 7,000 kila mwaka, ukizidisha 7,000X mara miaka 44 ya uhuru utapata jibu kamili...!

Sasa hebu asuume wewe ndio Rais unayeongoza taifa la namna hio, ambalo sehemu kubwa ya wananchi hawana elimu, wewe ungekua unafanyaje?

Tatizo lako ni kwamba unajaribu kulinganisha Tanzania na Marekani au na Uingereza, lakini umejuiliza Marekani au Uingereza inawasomi kiasi gani? au Ilipata lini uhuru? Pia, usilaumu tu ukiwa huko nje ya nchi, njooo huku tanzania uje uijenge nchi yako, usiishie kujenga nchi za watu halafu uishie kulaumu nchi yako na viongozi wako....!

Pia, usisahau kwamba ROME WAS NOT BUILD IN ONE DAY, tusifikiri tutaweza kulala na kuamka tukakuta kesho tanzania imebadilika, kama sisi wananchi wenyewe hatuwezi kubadilika suitegemee hata tungeletewa malaika kutoka mbinguni nchi yetu itabadilika....! Hayo ni maoni yangu mbadala tu....!

Mhafidhina,

Blah blah blah!

I could not even finish to read your post before I started responding to your blah blah blah!

Sisi tulipata uhuru kabla ya Rwanda, Uganda au Kenya.

Sisi tumekuwa na "amani" bila kuwa na vita vya ndani kuuana au kumalizana kama Rwanda, Uganda, Kenya, Msumbiji na Kongo.

Je inakuwaje wenzetu wanaendelea kupeta na kujisahihisha kwa makosa na sisi tunaendelea kung'ang'ania miaka 44 ya Uhuru na ufinyu wa wasomi?

Hivi kuishi kwa uadilifu na Serikali kufanya kazi kwa kuwajibika na uadilifu kunahitaji wasomi wangapi?

Uhuni uliofanywa na Wanasiasa wtu tangu tupate Uhuru mpaka leo ni kwa kuwa Wao si wasomi au wananchi si wasomi na nchi bado changa au ni utashi binafsi?

Kikwete ni Mkuu wa Nchi, ni sawa sawa na CEO na ni sawa na Rais wa Marekani, Waziri Mkuu wa Japan au Rais Kagame wa Rwanda. Iweje yeye awe dhaifu na tuanze kutafuta visingizio kuwa eti ni lazima awe na busara na vikolombwezo vingine na tumpe "mji" atuongoze?

Kama angekuwa na busara, asingechagua walaghai kuwa Mawaziri au Watendaji wa Serikali.

Kama angekuwa na busara, uhuni wa kuihujumu nchi yetu usingepata nguvu na kiburi cha kufanya unachofanya hata kujitukuza na kudharau wananchi.

Kama angekuwa na hekima na upeo wa maono ya mbali, angesitisha mikataba inayoidhulumu Tanzania.

Kwa mtaji wa hekima na upeo wa maono, angelitumikia Taifa na kulinda maslahi ya Taifa na si marafiki au kikundi maalum ndani ya chama au wawekezaji.

Kikwete hawezi kazi, zaidi hajui ni vipi kazi yake ina matokeo mawili tuu, ama kujenga au kubomoa nchi!

Kwa hekima, busara na upeo wa kuona mbali unaompa Kikwete, nakwambia wazi ati huyu hafai, ni mwoga, mvivu, mzururaji na mpiga domo asiye na vitendo.

Hata Mwinyi na upole wake aliheshimiwa na kuogopwa, iweje huyu unayemtukuza hakuna anayemheshimu?

Hivi niambie kila mtu anavuta kamba yake kudai demokrasia kuhusu Muungano, unakumbuka kiliwatokea nini Jumbe, Hamad, Malecela na Kolimba walipocheza makedamakeda na Muungano?

Blah blah blah, unampa tukuzo asiyestahili! Kakiri "mimi Mkwere, kuogoelea sijui'!
 
reverend... wanasema you hit the nail right there; kwa lugha ya JF umemkoma nyani giledi kweli kweli. Lazima ifike mahali tuache kumtafutia rais udhuru.
 
Mchungaji, katika argument yako there's one central theme: the presidency is a very pwoerful office, na inampa almost omnipotent power. in fact checks and balances za Tanzania ni legelege sana. Sasa when someone occupying the most powerful seat in Tanzania anaanza kusingizia eti hana uwezo wa kufanya kitu basi ujue it is a sign of big trouble!! No more excuses for Vasco Da Gama!!!
 
MKJJ

Kwanza naunga mkono juhudi zako ktk unachoendelea kufanya kuhusiana na kijarida cha "cheche" BRAVO!

Nadhani ni hatua muhimu kuwafikia watu wengi zaidi na kuwafanya kutambua walipo na wanapokwenda ktk nchi yao na nafasi yao ktk kufanya mabadiliko yatakayo leta maendeleo.NGuvu unazotumia hapa inabidi kiasi kikubwa uzielekeze kwenye hicho kijarida kitachowafikia watu wengi zaidi pamoja na hapa JF.

Kwa kusema hivyo naona hutakuwa umetoka hapa kwa maana copy ya kijarida cha cheche tutakuwa tunakipata na kwa uchache tutahitaji comments zako.

Nimesoma majibu yako marefu uliyomjibu kijana hapo juu ,yako makini nikasema moyoni hizi fikra kuna watu wengine wanahitaji kuzipata na hawana access ya net, pia wengine wanaamini pia kama huyo aliyekuwa akitetea udhaifu wa mkuu wa kaya.Kwa kweli umesherehesha vema mpaka nikadhani kama ndio ww umesema na kujijibu( no offensive)yaani majibu ni mule mule kitu na box.

Bravo Brother Keeping on doing a good work.
 
Bravo kwa wote wenye uchungu na Tanzania. Bravo kwa Mwanakijiji, Rev Kishoka, ESFM, Kitila na wengine wengi wana JF. Nimekuwa na nyinyi kwa muda sasa, lakini ilipofika mwezi wa tano mwaka huu niliamua niwe naangalia. Nioene jee kutabadilika.

Kusema kweli nimeshindwa kusikiliza speech ya Jakaya, machozi yamenitoka, na nimeshindwa kumalizia kusoma what Mwanakijiji alichokuwa akisema. Nadhani nimepandwa na jazba, au ni uchungu wa kuibiwa na kunyanyaswa, uchungu wa kudhalilishwa, na kuteswa, ni uchungu wa wadhalim kama JK na wenzie.

Nadhani imani yangu na Tanzania iko kwenye kingo, siamini tena kama Tanzania ni for all Tanzanian. Nadhani Tanzania ni for few elites on top, Tanzania ni kwa kina JK mpaka kina Mkapa. Ni nchi ya wachache na wengi tulibakia ni vibarua.

Raisi anapopindisha sheria, na kuanzisha sheria yake ya kuwapa watu siku za kufanya malipo kama vile imeruhusiwa kikatiba. Ni sawa na raisi aliyetuvua nguo sote, akatuacha wazi mbele ya wake zetu na watoto zetu. Ni raisi msaliti ambae hastaili kuishi na sisi, bali anastaili kutengwa na kuishi visiwa vya mbali au porini.

JK ametudhulumu watanzania, na Kisheria ya dini yangu na JK ni kwamba dhambi ya dhuluma ni dhambi kubwa sana. Na ni dhambi itakayo msaka mpaka siku ya qiyama.

Nimeona ni towe dukuduku langu.... Poleni Watanzania, nchi imeuzwa na aliyeinunua ni Rostam.
 
bila kanzisha redio na television hakuna atakaye kusikia , vijijini hakuna magezeti , REDIO UKOMBOZI tuianzishe, unaona mkuu kasikia nchi zima, tanganyika sasa irudi kumbe ni nchi kama zanzibar
 
MKJJ mkuu wetu wa kaya tumempa nafasi kibao za kujipanga na kufanya shambulio zito lakini yeye mwenyewe anashindwa kwa hiyo hapa tunamashaka na kura zetu tulizo mpa zilikuwa kwaajili yake na watu flani flani anao wajua yeye.
HApo naweza nikasema JK katika urais wake ameingia ubia na watu flani flani anao wajua yeye na kusimama kidete kuwatetea kinamna namna.Aangalie muda utakapo fika atakaa pembeni ataanza kuhukumiwa na watakao chukua kiti chake.Kama anawalinda ili na yeye wamlinde hapo baadae anajidanganya sana kwani watu sasa wanatambua wapi wananyonywa na wapi wanapigwa bla blah ingekuwa enzi hizo hotuba kama hiyo watu wangeanza kumsifia sana mitaani na kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Mnao mshauri JK mnampotosha kwa masirahi yenu binafsi mlio karibu naye mmshauri ajiunge na JF hapa aje apewe nondo huko anako elekea si sahihi kabisa watu tunakosa imani naye sasa....
 
Mimi si member wa siku nyingi JF ila Mwanakijiji amekuwa mstari wa mbele katika posts na unchangiaji wa mada muhimu kwa taifa letu. Ninakuomba sana, tena sana gawa tu muda wako ili japo upate muda kidogo kwa mchango JF hasa pale ambapo kuna a big issue for discussion. Kweli, priority ipe hiyo Newsletter but, chonde tuwe wote. tupigane wote na mwisho tutashinda tu. Nakupongeza kwa kijarida hicho, ibua issues na kifikie wengi. Naomba ikiwezekana tafuta ufadhili uweze kutoa both English and Swahili Versions kufaidisha lugha zote kuu mbili kwa TZ. Samahani sijakisoma hivyo sijui kama unakitoa kwa Lugha ipi. Bravo MKJJ.
 
Goodmonring people of Tanzania...its another day na jua nalo halina hiyana limechomoza kama kawa...giving us hope and the possibility that its not the end, but the begining. Yesterday is just that yesterday. MKJJ and all others in JF you are the reason some of use who were guests for a while decided to become members in JF, ilikuwa part of what can bring changes in our country, kupata/kutoa maoni (however few), kwa kupeana moyo na zaidi ni kupata ufahamu jinsi mambo yanavyokwenda nchini kwetu and not just go with the flow. For the 1st time jana i listened to JK's speech (just shows how young in all this i am!)...am speechless and wondering what was the whole point!
Am not saying MKJJ and those who think they should take leave should not, hiyo ni haki yenu na you have all the rights to decided what to do with your time, but as you are thinking of that keep in mind, JF members value your views, your knowledge na siasa ya nchi yetu (i personally learned a whole lot of things right here in JF). However as you take other step on fighting for changes, msiache JF, i have seen Cheche jarida, and big up for it MKJJ, i see you even have a section kutoa ya wanaJF, we can work together kuisambaza na kuhakikisha it spreads around, hata humu mjini kuna watu hawaijui JF wala why we are facinated with it...but through the jarida they will be enlightened.
Muhimu ni kuacha kulumbana wenyewe kwa wenyewe for issues zisizo na maana but on facts and things that will change our thinking for the better, and make us believe together we can make things happen!
JF for changes...
 
tatizo hatuna mbadala!!! atarudi kwa kishindo tu. naumia sana sana
 
ndugu yangu Mwanakijiji hebu niambie ugomvi wako na hotuba ya jana ya Jakaya ni nini hasa? kuzungumzia barabara?umeme?shule?nishati?inflation?michezo?umuhimu wa kuwatendea watu haki?,muungano?muafaka? nini hasa kimeku put off mpaka unaamua kuzila JF? Ulitaka atangaze kuweka watu ndani au kuua kabisa?
 
ndugu yangu Mwanakijiji hebu niambie ugomvi wako na hotuba ya jana ya Jakaya ni nini hasa? kuzungumzia barabara?umeme?shule?nishati?inflation?michezo?umuhimu wa kuwatendea watu haki?,muungano?muafaka? nini hasa kimeku put off mpaka unaamua kuzila JF? Ulitaka atangaze kuweka watu ndani au kuua kabisa?

You are not serious!
As a speech from the leader ingekuwa na final directives and decisions...and not creating more questions and dissapointments.
 
ndugu yangu Mwanakijiji hebu niambie ugomvi wako na hotuba ya jana ya Jakaya ni nini hasa? kuzungumzia barabara?umeme?shule?nishati?inflation?michezo?umuhimu wa kuwatendea watu haki?,muungano?muafaka? nini hasa kimeku put off mpaka unaamua kuzila JF? Ulitaka atangaze kuweka watu ndani au kuua kabisa?

Come on Bishanga,
So you are happy kwamba kasema wezi wa EPA amewapa muda wa siku 72 walipe mambo yaishe???? Yaani una mbembeleza mwizi tena unamfichia siri???

Speech gani hiyo isiyo na maamuzi? isiyo na meno zaidi ya bla blah na uswahili wa kukata mzizi wa fitina? mzizi gani kaukata kwenye spichi yake? kuwalinda wahujumu uchumi? grrrrrrrrrrrrrr!!!!

Nani kamwambia shida yetu watz ni kuwa na wabunge wanawake wengi bungeni?? shida yetu ni ukali na ugumu wa maisha uliosababishwa na wahujumu uchumi ( a.k.a fisadi) yeye anakuja na cheap sentences kukwepa analotakiwa kulifanya!
 
Binafsi jana nilitoka kazini nikijua muheshimiwa si wa kumsikilizia ofisini na sikupenda niadithiwe,kwa hakika nilijilaumu kwa kile nilichofanya.Binafsi kikwete nilikuwa simuamini kabla hata hajapata urais wenyewe,ila alinipa moyo na ile hotuba yake ya kwanza pale bungeni.Jana ilifikia wakati nikawa najiuliza pale bungeni alikuwa ameenda kufanya nini,nafikiri kama ana akili atagundua yale maneno ya spika yalikuwa yana maana gani.Ndo kwanza mwaka wapili na nusu na bado atataka miaka mingine mitano 2010.WE HAVE A LONG WAY TO GO.
 
I missed this speech. Seems dude Rocks!! Kafanya nini hadi mmenuna?
beavis_and_butthead_headbanging.gif
 
MKJJ

mawazo yako yapo sahihi kabisa ila watanzania hatuna utamaduni wa kusoma. Nina idea tofauti. Kwanin tusianjishe redio ikawa na nguvu kama RFA ilivyo na nguvu na sisi tukaisimamia kwa udi na uvumba? Mkuu sioni sababu ya kupeleka sadaka kanisani wakati sidhani kama inafaida at all. Ni kwanini nisitoe fungu langu la kumi kwa mtu ambaye atakuwa hodari kwenda kuwaambia wananchi nini maana ya siasa na root cause ya haya matatizo? kuwapa shule waelewe, inchi itanyooka tu.

Naomba kuwakilisha.

Naunga mkono mawazo yako..JF inawanachawa wengi sana hivyo tukitoa fungu la kumi..tutaweza kabisa kumiliki Radio Station
 
We expected alot but he delivered nothing!I

Poleni sana wajemeni, I understand your feelings about our president. But then, I will not stop asking this because you always force me to, why did you expect "a lot" from this guy? What made you have such huge expectations in the first place?

Huyu mtu amekuwa kiongozi serikalini maisha yake yote na hajawahi kufanya chochote cha kushikika. Iweje leo nyie ndiyo mlitegemea afanye makubwa katika urais? Au mlidhani ukiwa Rais basi unavishwa uwezo, akili, uchungu,n.k.?
 
Back
Top Bottom