Illuminati na kifo cha Michael Jackson

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,322
Wanasema ilianzia kwenye video ya wimbo wa ‘BLACK OR WHITE’

Ujumbe wa siri unao patikana kwenye wimbo huo ni kwamba Michael Jackson anawaambia Illuminati wao na yeye sasa ni basi.

Katika wimbo huo Michael Jackson anaonekana akitakaswa na maji matakatifu, sauti ya shetani akiwa amekasirika inasikika, Michael Jackson anazaliwa mara tatu kama alama ya ‘kuzaliwa upya, kuwa mtu mpya na kuachana na mambo ya kale, kisha najipongeza mwenyewe kwa hilo, anapiga magoti mbele ya Mungu na kuwa huru kutoka kwenye mikono ya illuminati.

Kisha kachukua maji matakatifu na kuyamwagia kwenye alama ya ‘ROYAL ARMS’ na ‘Royal’ ikiwa na maana ya ‘Royal Bloodline’ ambazo nazo zipo 13. Mwishowe Michael anabadilika na kuwa ‘panther’. Lakini kabla ya hapo alivunja kioo cha gari kilicho andikwa ‘NIGGER GO HOME’ na na ndani ya maneno hayo nambari ‘666’ ikiwa imefichwa ndani yake.

Akavunja bango la ‘KKK’ ambapo ‘K’ ni herufi 11 kwenye alfabeti,hivyo 11x3=33, lakini pia ‘KKK’ inasimama badala ya jina la Ku Klas Klan, ambalo ni jina la kikundi cha Illuminanti, kilicho undwa na Albert Pike mwana masonia wa daraja la 33, kikundi hichi ni cha kibaguzi na kinahusishwa na kila aina ya uchafu unao fanywa na Illuminanti dhidi ya watoto, wanawake na watu wa matabaka mengine.

Mwishoni Michael Jackson alipogeuka ‘Panther’ ambapo panther inawakilisha, nguvu, uhuru, kuzaliwa upya baada ya mateso, yaani kuwa mtu mpya. Miaka 3 baada ya wimbo huo hadithi ya Michael Jackson kwenye vyombo vya habari ikabadilika.

Miaka 17 iliyo fuata Illuminanti walikuwa kwenye vita kali na Michael Jackson, kwa miaka yote hiyo walifanya kazi kubwa ya kuibomoa taswira yake kwenye vyombo vya habari na kwenye macho ya walimwengu.

Hawakutaka kumuua kipindi hicho kwa sababu hilo lingezindua watu, walimwengu wangeona kuna ambacho hakipo sawa, hivyo ilihitaji mpaka muda maalum, wakati muafaka.

Ingawa Michael Jackson hakung’ara na kupanda chati kwa sababu ya ‘ku-sale his soul to the devil’ lakini kwa sababu ya kipaji chake, lakini hata hivyo Illuminati hawakupoteza malengo yao, walimtumia Michael Jackson kwenye kazi zake kutukuza na kutangaza ushetani.

Wimbo kama ule wa ‘Thriller’ na ‘Beat it’ utakuta kwenye mashairi yake kumebeba vionjo vya kishetani.

Kwa Illuminati ‘mtu mweusi’ ni sawa na mnyama, yaani thamani yake ni ndogo, yaani siyo binaadam kamili, hili linahitaji mtiririko wa post kadhaa iliuweze kuelewa, lakini unapotizama filamu za Hollywood, unapotizama sera za nchi za Ulaya dhidi ya nchi za kiafrika, unapotizama matukio ya ubaguzi kote duniani, hutachelewa kuona kuna tatizo la makusudi la kutengenezwa dhidi ya matabaka na rangi za watu.

Hivyo Michael Jackson naye ‘weusi’ wake ulikuwa ni shida kwenye kipaji chake, ‘baniani mbaya kiatu chake dawa.’

Vipi basi mtu mweusi awe ‘KING OF POP’ na abakie kama kama mtu mweusi, na akumbukwe kama mtu mweusi, hapana hili hata kidogo haliwezekani, hata kidogo haifai mtu mweusi kuwa ‘king of pop’ kazi ya ziada ikafanyika na Michael Jackson akaambukizwa au akatiwa ugonjwa wa ngozi unao fahamika kama ‘VITILIGO.’

Kwenye mahojiano ya mwaka 1993, Michael akasema kuwa ‘Baba aliniambia kuwa ugonjwa wa ngozi wa Vitiligo upo kwenye damu ya familia yetu”

Lakini ajabu ugonjwa ulimpata Michael Jackson peke yake ambaye ametokea kuwa ni King of Pop.

Kabla ya ‘Thriller’ MTV, walikataa kuonesha kwa watazamaji wake wimbo wowote wa Michael Jackson.

Kwanini?

Michael Jackson ni MWEUSI.

Rais w CBS Records Walter Yetnikoff aliwatishia MTV na kuwaambia “Sitawaletea tena video na ninakwenda hadharani na **** kuwambia watu kwamba hamtaki kuonesha video za watu weusi"

Nafasi ya Walter iliwafanya MTV waanze kurusha vidio ya ‘Billie Jean’ na ‘Beat it’.

Bahati mbaya ni kuwa Thriller ilikuwa ni kama barabara ya kumfanya Michael kuwa kikaragosi cha Illuminati, kuanza kumtumia Michael na kipawa chake kuingiza maono ya kishetani kwa umma. Safari hiyo ilikuwa ni muhimu kufanyika kabla hawajamfanya Michael kuwa ‘White Man’ yaani kabla hawajampatia ugonjwa wa vitiligo ulio badilisha ngozi yake.

Dada yake na Michael, Latoya Jackson alikuwa na haya ya kusema kuhusu kifo cha kaka yake.

"I believe Michael was murdered," she said. "I felt that from the start. Not just one person was involved, rather it was a conspiracy of people. He was surrounded by a bad circle. Michael was a very meek, quiet, loving person. People took advantage of that. People fought to be close to him, people who weren’t always on his side."

"He had needle marks on his neck and on his arms and more about those will emerge in the next few weeks," she said. " I cannot discuss that any further as I may jeopardize the investigation. I can, however, say that I have not changed my mind about my feeling that Michael was murdered."

"I am going to get down to the bottom of this," she said. "I am not going to stop until I find out who is responsible. Why did they keep the family away? It’s not about money. I want justice for Michael. I won’t rest until I find out what and who killed my brother."

Yaani kwa kiswahili.....

"Namini Michael aliuwawa, nilihisi hilo tokea mwanzo, sio mtu mmoja tu alihusika pasi na shaka ni kikundi cha watu, alizungukwa na kundi baya, Michael alikua mkimya na mpole na mwenye upendo,kwaio walitumia nafas hio vibaya kwake,,watu walipigana kua karibu nae,sio kila mara watu walikua upande wake. Alikua na majeraha ya sindano kwenye shingo na kwenye mikono,japo siwezi kuzungumzia hilo kwa kina nitaharibu upelelezi, lakini siwezi kamwe kubadili msimamo wangu na ninachoamini kwamba Michael walimuua. Sitapumzika hadi nihakikishe nani alihusika, kwanini wameitenga familia, sina shida ya pesa,nataka haki itendeke kwa Michael, sitapumzika.hadi nijue nani alimuua kaka.yangu".

Michael Jackson alifahamu kuwa Illuminati wanataka kumuua. Mwili wake ulipatikana na majeraha kadha ikiwemo shingoni na magotini, pia inaonesha kuwa alidondoka sakafuni kabla ya kifo chake, yaani alikuwa akipambana dhidi ya muuaji kuokoa uhai wake.

Latoya alipoulizwa ni nani aliyemuuwa Michael alijibu ....

“Doctor unaye muona, anaye tajwa kama msababishi wa kifo, ni kinga, yupo nyuma yake watu waliotaka Michael Jackson afe.”

Wakati wa shitaka la mara ya pili la Michael lililomalizika Juni 13 2005, wazazi wa Michael walimuita rafiki yake na Michael Dick Gregory, ambaye alikuwa ni rafiki mzuri wa Michael, walimuomba amtembelee Michael maana hayupo vizuri hata kidogo.

Baada ya siku chache Gregory alirudi na Michael kwenye jumba lake la Neverland. Michael alimkumbatia na kumuambia tafadhali usiniache wanataka kuniuwa.

Gregory akamuuliza Michael lini ilikuwa mara yake ya mwisho kula maana anaonekana kudhoofu, Michael akamjibu, “ wanataka kuniuwa kwa sumu”, akamuuliza ni lini mara ya mwisho amekunywa maji, Michael akamjibu, “Wanataka kuniua”

Gregory akamchukua Michael na kwenda naye kwenye hospitali ya karibu lakini mbali na Neverland bila kumuarifu mtu yeyote kwamba anakuja hapo na Michael Jackson, na akatundikiwa dripi kutoka 11:30 jioni mpaka 11:30 asubuhi na siku iliyofuata kwa masaa 24 akawa kwenye drip bila kupumzika, Dr. Aliyekuwa akimuhudumia akasema lau asingefika kwa wakati basi masaa mengine 12 angelikufa.

Utaona hapo kuwa Juni 2005, illuminati walikuwa wakifanya jaribio la kumuuwa Michael tena, lakini lilishindikana, lakini Juni 2009 walifanikiwa kutekeleza azma yao baada ya kumtumia mtu ambaye Michael alimuamini zaidi, Daktari wake, Conrad Murray.

Michael alikuwa na nguvu za kutosha, dokumentari kadhaa zimetolewa zikimuonesha wiki kabla ya kifo chake, alionekana yuko safi, na akifanya maandalizi ya ‘tour’ yake ya London aliyoipatia jina la ‘THIS IS IT’, Tetesi ni kuwa kwenye Tour hiyo Michael kati ya mengi aliyo kuwa nayo ilikuwa ni kuufumbua macho ulimwengu kuhusiana na madhila na ubaya wa Illuminati, lakini jamaa nao walishaiona hatari hiyo na hawakuwa na muda wa kupoteza, ndipo daktari ambaye pia ni Freemason alipochukua jukumu hilo zito la kumuangusha King of Pop.
 
Kuna vitu vingine vinafurahisha sana,tunaambiwa mwanadamu anaongozwa kwa dhamira mbili ambazo humsababisha atende mema au mabaya,akitenda mema basi hiyo ni dhamira ya mungu na akitenda mabaya hiyo ni dhamira ya shetani ndio imemutuma.lakini neno hilo hilo linasema Mungu ndio muumba wa vitu vyote hata shetani aliumbwa na Mungu ndio tusema Mungu alimuwekea shetani ndani yake dhamira ya uovu-kwa maana nyingine Uovu unatoka kwa Mungu mwenyewe,sasa ni kwa nini ahukumu binadamu kwa nnn uovu alio uumba mwenyewe??? Uamuvi wa binadamu kuwa upande a au b ni uamuzi ulio ndani ya nafsi yake ambao umetoka kwa Muumba wake!
Kama kweli!Mungu atawahukumu binadamu eti kwa kuwa hawakutenda mema basi ni dhahiri anajihukumu mwenyewe
 
Story hi niliwahi pia kuisikia kama ilivyo somewhere; the question is, kwanini weusi tunachukiwa hivi!? Kuna viongozi kadhaa ambao nao ni members wa hilo kundi na ni weusi, hivi hua wanajisikiaje wanapodharauliwa na members wenzao weupe!?
Hii stori niliisoma kwenye Los Angeles Times mwezi ule e aliofariki MJ
 
Kama mimi ...one of my best. hua anankumbusha old memories when i listen to his songs hasa zile za kitambo
Mi nina documentary yake yani ni anaonesha maisha ake halisi...

Jamaa alikuwa na roho nzuri sana..

Kama kuna viumbe vilivyopendwa duniani basi MJ was the best, kuna siku alienda German kuuza nguo zake kwenye Auction ili kusaidia watu wenye Kansa, hiyo nyomi barabarani ilikuwa ni nomaa

Kuna videmu vilitenguliwa hadi viuno na virungu vya Polisi eti " I wanna hug Michael"
 
Mi nina documentary yake yani ni anaonesha maisha ake halisi...

Jamaa alikuwa na roho nzuri sana..

Kama kuna viumbe vilivyopendwa duniani basi MJ was the best, kuna siku alienda German kuuza nguo zake kwenye Auction ili kusaidia watu wenye Kansa, hiyo nyomi barabarani ilikuwa ni nomaa

Kuna videmu vilitenguliwa hadi viuno na virungu vya Polisi eti " I wanna hug Michael"
Alikua ana nyota kali sana sana
kuna baadh ya show zake yan anaanza kuimba tu wadada wanazimia wengine wanalia kabisa ...aiseeee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom