Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Mpwimbe,
Kuna maswali mimi sina majibu yake.
Utaalamu wangu uko kwenye historia ya Tanganyika.
Historia hiyo yako potovu we mzee kila kitu kichwani mwako ubongo wote ni Abdul Sykes,sykes×100,
UDINI unao sana tu.
Juzi umekiri mwenyewe sijui madrasa gani ikivunjwa Lumumba.
Umepinda Story na blaah,blaaah zako eti Waislamu hawajatajwa ila wewe umeandika sahihi.
Kuna Historia kila mahali ya Tanganyika.
We unalazimisha yako ndo ukweli
Na huo upupu wa vitabu vyako vya sh 10.
You always undermine Nyerere Baba wa Taifa hili.
 
Zemanda,
Nitawezaje kufuta ushahidi ilhali jina langu lipo Library of Congress, Washington DC, Cambridge Journal of African History, kuna vitabu nilivyoandika, nina blog na You Tube Channel.

Nipo katika maktaba ya radio na tv stations nyingi.
Ningekuwa mimi ni mtu mbaya ningekuwa nishafungiwa huko kote na mialiko isingekuwapo kamwe.

View attachment 3625451
Al Jazeera
View attachment 3625452
Voice of America (VoA) Washington DC
View attachment 3625453
BBC London
View attachment 3625455View attachment 3625456
Library of Congress, Washington DC
Hao waliokualika kote huko nao ni kina said,yusuph,jamal,Muhammed, walewale tu
 
Hao waliokualika kote huko nao ni kina said,yusuph,jamal,Muhammed, walewale tu
Babu,
University of Iowa nilialikwa na Prof. James Giblin na Northwestern University na Prof. Jonathon Glassman.

Zentrum Moderner Orient (ZMO) Berlin na Prof. Kai Kresse.
 
Historia hiyo yako potovu we mzee kila kitu kichwani mwako ubongo wote ni Abdul Sykes,sykes×100,
UDINI unao sana tu.
Juzi umekiri mwenyewe sijui madrasa gani ikivunjwa Lumumba.
Umepinda Story na blaah,blaaah zako eti Waislamu hawajatajwa ila wewe umeandika sahihi.
Kuna Historia kila mahali ya Tanganyika.
We unalazimisha yako ndo ukweli
Na huo upupu wa vitabu vyako vya sh 10.
You always undermine Nyerere Baba wa Taifa hili.
Babu...
Vitabu vyangu naweka bei ya chini kwa nia ya kuwafanyia wepesi wasomaji wamudu kununua.

Toleo la tatu bei ilikuwa 10, 000.00 hii ilikuwa 2014.

Toleo hili la nne bei ni 15, 000.00 na ni kitabu cha kurasa 416 na cha ubora wa kimataifa.
Kiangalie hapo chini:

1783888803751.png
 
Historia hiyo yako potovu we mzee kila kitu kichwani mwako ubongo wote ni Abdul Sykes,sykes×100,
UDINI unao sana tu.
Juzi umekiri mwenyewe sijui madrasa gani ikivunjwa Lumumba.
Umepinda Story na blaah,blaaah zako eti Waislamu hawajatajwa ila wewe umeandika sahihi.
Kuna Historia kila mahali ya Tanganyika.
We unalazimisha yako ndo ukweli
Na huo upupu wa vitabu vyako vya sh 10.
You always undermine Nyerere Baba wa Taifa hili.

View: https://youtu.be/ZrfyEHlxr7I?si=aVjbXaj38JAkzrIl
 
Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.

Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.

Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.

Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.

Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.

Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.

Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.

Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.

Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.

Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.

Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.

Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukristo.

Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Okochi, Ongalo, na Aoko hawa ni wakenya??
 
Ndio nikawa nashangaa inakuwaje mtoto wa kikijini Butiama akamshinda mtoto wa mjini A.Sykes. kumbe kulikuwa na makubaliano/maoni ya namna. Kuna sehemu historia yetu hailezei vizuri haya mambo.
So really you've fallen for this crafted narrative.
 
Mzee mimi sio mjinga halafu mimi nimezaliwa katika jamii ambayo haina udini. Mtu kama wewe na hoja zako ni rahisi sana kubaini dhamira yako.

Lengo lako ni dhahiri sio kuelimishana ila unatumia huu mwanya kutengeneza narrative ya kibaguzi ili waislam wahisi kudhurumika na kunyanyasika.

Huu ni upandikizaji wa chuki ya wazi wazi. Kwa hili sitakuachia na nitakutangaza kwa huu uovu. Wewe na wale interahamwe wa RWANDA MASSACRE hauna tofauti.

Nimeshakopi hizi nyuzi zako na kuscreenshot vichwa vya hizi nyuzi kama ushahidi incase ukitaka kubadilika kuficha ushahidi.

Wewe sio mtu mzuri unataka kuwachonganisha raia kwa kuwapa sababu na hoja za kibaguzi ili waanze kutazamana kwa macho ya kubaguana. Wewe sio mtu mzuri kwa taifa.

Watu kama wewe ndio Nyerere alikuwa anawaweka kifungo cha ndani kwasababu mnapenda kuanzisha mijadala ya kibaguzi mkijifanya mnatafuta haki.

Wewe sio mtu mzuri narudia tena, wewe MZEEE NI MFITINISHAJI NA UNA ROHO MBAYA SANA YA UBAGUZI.
Bravo bro, 👏 👏 👏 👏.
 
Bravo bro, 👏 👏 👏 👏.
Nakuwekea hayo hapo chini na nitashukuru sana kupata mawazo yako:

Nakuwekea hayo hapo chini na nitashukuru sana kupata mawazo yako:

Nashukuru umetaka maoni yangu.
-Nyerere asingetaifisha shule zilizokuwa zinamilikiwa na taasisi za kidini(mostly makanisa ya Catholics) gap la elimu ya Christians na Muslims kwenye elimu lingekuwa ni kubwa mno.
-Nyerere asinge-politicize vyama vya ushirika vilivyochangia kusomesha vijana enzi hizo(mostly wakulima wa kahawa ndiyo walisomesha sana kwa makato ya mauzo ya kahawa no wonder Kagera(the then West Lake), Kilimanjaro na Mbeya ndiyo walisomesha zaidi vijana wao basi maeneo mengi yangeachwa nyuma sana kielimu.
-Nyerere alilazimisha kuweka balance ili kuwe na uwiano lakini ikawa inaua quality ya elimu.
 
Monster,
Nilitaka uone udini uliokuwapo.
 
Monster,
Nilitaka uone udini uliokuwapo.
Udini ulikuwa ni kunyang'anya institutions za dini mbalimbali kuzigeuza kuwa za umma whilst nyingi zilikuwa zikipokea waumini wa dini zote na wapagani pia, the terribly painful and dangerous thing ni nyie mnaoukoleza udini kwa ajenda(agenda) zenu binafsi.
 
Waislamu hawakunufaika na utaifishaji wa shule za Kanisa.

Soma tena hotuba ya Kitwana Kondo kaweka takwimu.

Wizara ya Elimu haikuwa na majibu.
 
Ni kweli lugha za staha zinahitajika
Ndomana toka mwanzo nlikuambia hao wakina Sykes walikuwa mbele ya muda
Tofauti yao na nyerere ni falsafa tu wakina Sykes nyerere aliona kama wako kipebari zaidi huku JKN akiamini ujamaa na kujitegemea

Ova
Huyu Mzee mwenyewe anapenda misaada kuliko kula.

Ubepari na misaada wapi na wapi?
 
Monster,
Waislamu hawakunufaika na utaifishaji wa shule za Kanisa.

Soma tena hotuba ya Kitwana Kondo kaweka takwimu.

Wizara ya Elimu haikuwa na majibu.
Kwamba Wizara ya Elimu inataliwa kutoka kujibu tuhuma za msikitini?

Hao Kikwete wamesoma shule za Kanisa?

Nyie ndio mnataka wizara ya afya itoke kujibu kwanini inapeleka watumishi hospitali za kanisa au inasamehe kodi pesa za Wazungu wanazotoa kwa makanosa??
 
Nakuwekea hayo hapo chini na nitashukuru sana kupata mawazo yako:

Hizo asilimia ni kitaifa?

Kama ni kitaifa zina ukweli kiasi gani?

Kama ni kitaifa nina wasiwasi na hizo takwimu.
 
Nyakubonga,
Nilitaka uyajue haya.
Ikiwa unaona ni uongo hapana neno.
Umesusa mzee?

Nilitaka kujua ukweli wa takwimu hizo

na

Nikasema nina wasiwasi nazo sijazikataa moja kwa moja...

Na wasiwasi wangu ni njia iliyotumika kukusanya takwimu hizo...

Nahofu isije kuwa ni zile hisia zilizosababisha tukamwona mama Ndalichako anatufelisha...
 
Hapana.
Nimekujibu kuwa ikiwa huamini hayo niliyoweka kwangu ni sawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom