Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Uandaliwe mdahalo wa Zemanda na Mohamed Said

Ova
Mrangi,
Nadhani unanifahamu kwa kusoma niandikayo.

Naamini pia unamfahamu ndugu yangu anavyoandika.

Mdahalo unahitaji adabu na heshima.

Mdahalo unapendeza pale watu wenyewe uwezo sawa au angalau unaokaribiana wanapopambana.

Lakini tambua pia kuwa kitabu hiki kina miaka 28 na kilipotoka mwaka wa 1998 na baada ya book reviews tatu za John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History nilialikwa University of Iowa.

Nilikizungumza kitabu na mtu niliyepambananae sana alikuwa James Brennan.

Mgongano huu ulisababisha mimi kupewa mwaliko hapo hapo kwenda Northwestern University, Chicago kufanya mjadala mwengine sawa na ule wa Iowa.

Mjadala wa Iowa ulikuwa moto.
James Brennan ndiye aliyenichukua hadi Chicago na gari yake.

Brennan hakuzungumza sana Northwestern University wala washiriki wengine.

Nakurudisha nyuma.

James Brennan alipomaliza Ph D yake Northwestern University alikwenda kusomesha SOAS.

Brennan kanishukuru katika Thesis yake kwani alikuja Tanga nilipokuwa nafanya kazi wakati anafanya utafiti wake na mtu aliyemshauri aje kwangu ni Mwalimu wake Jonathon Glassman aliyemsomesha hapo Northwestern University.

Jonathon Glassman tulijuana miaka mingi nyuma.

Nakueleza haya yote ili unifahamu.

Naamini umenielewa.

Mimi siko hapa kufanya maskhara.

1783593422333.png

James Brennan kila akija Dar es Salaam huwa tunakuwa sote hizi ni picha
za miaka tofauti.
 
Mrangi,
Nadhani unanifahamu kwa kusoma niandikayo.

Naamini pia unamfahamu ndugu yangu anavyoandika.

Mdahalo inahitaji adabu na heshima.

Mdahalo unapendeza pale watu wenyewe uwezo unaokaribiana wanapopambana.

Lakini tambua kuwa kitabu kina miaka 28 na kilipotoka na baada ya book reviews tatu za John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan nilialikwa University of Iowa.

Nilikizungumza kitabu na mtu niliyepambananae sana alikuwa James Brennan.

James Brennan alipomalixa Ph D yake Northwestern University alikwenda kusomesha SOAS.

Brennan kanishukuru katika Thesis yake kwani alikuja Tanga nilipokuwa nafanya kazi wakati anafanya utafiti wake na mtu aliyemshauri aje kwangu ni Mwalimu wake Jonathon Glassman.

Nakueleza haya yote ili unifahamu.
Naamini umenielewa.

Mimi siko hapa kufanya maskhara.
Ni kweli lugha za staha zinahitajika
Ndomana toka mwanzo nlikuambia hao wakina Sykes walikuwa mbele ya muda
Tofauti yao na nyerere ni falsafa tu wakina Sykes nyerere aliona kama wako kipebari zaidi huku JKN akiamini ujamaa na kujitegemea

Ova
 
Economist,
Ungepunguza hamaki ukauliza ungeongeza maarifa yako.

Nyerere hakika alishinda uchaguzi ule lakini uchaguzi ulikuwa umepangwa kuwa uongozi wa TAA apewe Mwalimu ili kuepusha TANU iliyokuwa inatayarishwa isiwe na viongozi walewale wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).

Nyerere alishinda kwa kura chache sana.

Unaweza kusoma historia ya uchaguzi huu katika kitabu cha Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," (1965).

Wazee wangu walitaka TANU iwe na sura ya chama cha siasa ambacho hakionyeshi kutawaliwa na Waislamu katika viongozi na wanachama wake:

View attachment 3618456
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akimsindikiza Nyerere Mahakamani 1958.
Kama alishinda kwa kura chache si ina maana mchuano ulikuwa mkali?
 
Kama alishinda kwa kura chache si ina maana mchuano ulikuwa mkali?
Magnificio,
Hakika mchuano ulikuwa mkali kwa kuwa kuna baadhi ya wanachama
hawakukubali ule mpango wa kukitoa chama kwa Julius Nyerere.

Denis Phombeah alimfanyia Nyerere kampeni kubwa akiwapitia wanachama
na pikipiki yake BSA wamchague Nyerere.

Abdul Sykes hakufanya kampeni yoyote.

Kwa kweli laiti Nyerere angaliandika maisha yake tungepata mengi au hata
angeeleza uhusiano wake na Sykes brothers.
 
NAONA UKUMBI UKO KIMYA KUTWA NZIMA TOKA ASUBUHI NA JUA LINAZAMA

Kwa kawaida huwa ikiwa kimya nami huwa kimya lakini kulikuwa na jeuri na kejeli ndiyo nimevunja mwiko.

Hivi ndivyo inavyokuwa kila mjadala.
Sijapata kushindwa.

Si hapa wala si nje ya mipaka ya Tanzania.

Ukiandika kwa herufi kubwa tupu maana yake ni kuwa unapiga kelele yaani SHOUTING.
 
Economist,
Ungepunguza hamaki ukauliza ungeongeza maarifa yako.

Nyerere hakika alishinda uchaguzi ule lakini uchaguzi ulikuwa umepangwa kuwa uongozi wa TAA apewe Mwalimu ili kuepusha TANU iliyokuwa inatayarishwa isiwe na viongozi walewale wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).

Nyerere alishinda kwa kura chache sana.

Unaweza kusoma historia ya uchaguzi huu katika kitabu cha Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," (1965).

Wazee wangu walitaka TANU iwe na sura ya chama cha siasa ambacho hakionyeshi kutawaliwa na Waislamu katika viongozi na wanachama wake:

View attachment 3618456
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akimsindikiza Nyerere Mahakamani 1958.
Hivi kati ya Nyerere na Sykes na wanae nani alikuwa kasoma zaidi ya mwenzie
 
Hivi kati ya Nyerere na Sykes na wanae nani alikuwa kasoma zaidi ya mwenzie
Camerlengo,
Umeuliza swali ambako tayari jibu unalijua na unalo.

Wakati Nyerere anakutana na Abdul Sykes 1952 Nyerere alikuwa tayari kamaliza Masters Degree University of Edinburgh.

Abdul Sykes yeye alipata admission Princeton University mwaka wa 1953 lakini hakwenda.
 
Kwa hiyo Nyerere alikuwa na merits?
 
Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.

Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.

Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.

Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.

Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.

Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.

Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.

Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.

Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.

Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.

Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.

Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukristo.

Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Ukweli uliopo Nyerere alikuepo amesoma na alikuwa msomi na hao wa shehe wengi walikuepo hawana elimu Dunia . Walitaka kuendesha nchi kwa kutumia mshahafu kitu ambacho ilikuepo ni vigumu . Pia Tanganyika ilikuepo na mpaka Sasa wakristo ni wengi zaidi kuliko waislam wakristo ni 65% na waislam ni kama 33% ingekuwa vigumu waislam kukabidhiwa nchi
 
DASM,
Nanufaika na haya uliyoandika.
Endelea kutupa historia hii.
 
Camerlengo,
Naomba ufafanuzi.

Hii "utoto wa mjini" na "ushamba" ina uhusiano gani na huu mjadala wetu.

Dhana hii umeitoa wapi?
 
Shubamit!
Tuko zama za AI bado watu mmekalia historia za kishamba.
Nyokweeeeeeeeer !
 
Unajua bakwata ipo chini ya nini bwamdogo? Au ushawai kusikia shehe gani akiwa chama chochote cha upinzani?
 
Umekuwa ukiijenga kwa muda mrefu!
We read between the lines!
Camerlengo,
Huwezi kutegemea dhana katika kutafuta ukweli.

Mimi sina sababu ya kuficha ukweli kwa kumuhofia mtu.

Mimi sijaandika matusi wala kejeli.

Siku zote nataka kusomesha watu waniamini.

Soma kitabu cha Abdul Sykes uone vipi nimemueleza Mwalimu Nyerere kwa sifa na uwezo wake ambao ni stahili yake.

Kitabu kina miaka 28 tunakwenda toleo la tano watu wamekipenda kitabu.

Ningeandika upuuzi ningekiua kitabu changu.
 
Historia ndivyo zilivyo
Ndomana huwezi sikia wakina kambona au John okelo wakitajwa
Bora hata hao wakina Sykes
Wanatajwa,na washashika nyadhifa kadhaa nchini

Ova
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom