Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Ilikuwaje TANU Ikasalimika na Udini?

Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.

Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.

Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.

Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.

Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.

Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.

Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.

Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.

Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.

Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.

Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.

Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukrist

Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Laiti kina Sykes wangelifanikiwa kudai uhuru kama Waislam labda Tanganyika ingegawanywa na Wakristu wangalikuwa na nchi bora kuliko hii inayoendeshwa na ccm. Na nyie mngekuwa na Pakistan yenu.
 
Hii ndio ilitakiwa kuwa TITLE ya Kitabu chako

Hao unaowaita Waislam, sisi tunawatambua kama Wachagga, Wahaya, Wamakonde, Wanyamwezi, Wahehe, Wasukuma, etc
Title ya kitabu ni: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
 
Mpwimbe,
Hakuna wa kukukataza wala mimi sioni vibaya kwani huo ni ukweli.
 
Chama chochote cha siasa kuegemea kwenye udini ni mbaya na hatari kwa afya ya jamii na mustakabali wa taifa, Nyerere alijitahidi kujenga nchi na jamii isiyoegemea udini na kwa hilo alifanikiwa na ni miongoni mwa maeneo aliyoweza kufanikiwa
 
Title ya kitabu ni: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
ni muda sasa nakitafuta hiki kitabu nikisome, nitakipata wapi?
 
1783490108674.png
 
TANU hawakuwa wabinafsi mission yao ilikuwa moja kudai uhuru, ndo maana hata alipokuja mwalimu watangulizi wake waliona wamwachie bila kumuwekea figisu kulikuwa na Viongozi wenye maono na wasio wabinafsi, CCM ya sasa imejaa Wezi Wabinafsi na wenye tamaa, wana roho ya nkikosa tuharibikiwe wote. Walianza na hoja mkiwachagua wapinzani ni chama changa wakaja Upinzani wa Lipumba una misimamo ya udini wakati huo huo anagombea na kikwete muislam kama yeye Wakaja na hoja ya CHADEMA ni ukanda wa kaskazin chama cha kikabila Wakaja Chama cha mabeberu wakaja chama kinasupport Ushoga, sahivi wanasema Chama cha kikatoliki, na sasa wanawekeza nguvu kubwa kutoa pesa kwa KKKT na bakwata wakidhan wanajenga taasisi imara za kidini kumbe ndo wanavuruga, kirusi kwenye Taifa hili ni mtu yeyote mwenye ukaribu na CCM
Hii ndio HOJA yenyewe. Tatizo ni chama dola - CCM. udini, kanda, uzanzibari, n.k. vinatumika tu kupambana na wanaopinga chama dola na magenge yake kuendelea kuhodhi madaraka na mamlaka kinyume cha katiba ya JMT. Kama kuna malalamiko basi yaelekezwe kwenye kupambana na mfumo wa chama dola unaoendelea kulitesa taifa. Huo mfumo umehodhi rasilimali, mamlaka, fikra na tunu zote za taifa na kuwahamasisha wananchi kufukuzia mizuka (ghosts) ya udini, uzanzibari, mabeberu, wapinzani, wasaliti, vibaraka, n.k. kama ndio sababu za matatizo yao badala ya kupambana na tatizo lenyewe.

Mleta mada, MSA, anachofanya ni kuziba pengo kubwa lililoko kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika. Nimesoma baadhi ya maandiko yake na ya waandishi mbalimbali wa nje kuhusu historia ya Nyerere, TANU na Tanganyika ambayo yanathibitisha pengo hilo ambalo ni kama liliwekwa kwa makusudi pengine "kuwarahisishia" Watanzania wasisumbuke sana na historia ya nchi yao bali wazingatie zaidi yajayo - labda kwa lengo maalum alilolijua Nyerere na watu wake.

Sijaona uthibitisho wowote wa MSA kudhamiria kuleta udini kwenye maandiko yake. Maandiko yake ni ya muda mrefu na hayajawahi kuleta shida. Tatizo ni kuwa wengi wa watu muhimu (notable historical figures) katika pengo lililopo kwenye historia ya nchi hii ni waislamu. Wako wakristo wachache pia ambao vijana wengi hawajahi kuwasikia au kujua habari zao kama kina: J. P. Kasella Bantu, C.K. Tumbo, J. Rupia, Alexander M. Tobias, Dr Michael Lugazia, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo, Patrick Aoko, n.k..

Bahati mbaya yako mengi sana ambayo, kwa bahati mbaya, yamo kwenye vitabu vilivyoandikwa kwa undani kwa kiingereza ambacho hapa kwetu ni ugomvi mwingine. Na kwamba siku hizi vijana wengi hawana muda wa kusoma vitabu bali hutegemea zaidi kupata habari toka JF, Facebook, instagram, X, n.k. ni suala jingine.

Yawezekana MSA kawekeza zaidi katika kuandika yanayohusu "wazee wake" wa Mzizima waliosahaulika au kufutwa kabisa katika historia Tanganyika na hivyo kuonekana "mdini". Na hao Indio walikuwa wengi zaidi na instrumental katika kuanzisha TAA baadaye TANU. (Naongezea pia klabu za Simba na Yanga). Hivyo, naweza kuzielewa hisia hizo za MSA.

Naamini kulikuwa na namna Serikali ingeweza kuweka sawa mambo haya katika mizania ya historia rasmi ya taifa iliyochapishwa badala ya kuyafunikafunika tu. Na ndio hivyo hivyo ilivyofanyika kuhusu masuala ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano na kuyapelekea kuyafanya NYETI sana hadi yakageuka kuwa moto mkali kuanzia visiwani kwenyewe hadi sasa "Tanganyika". Mhispania George Santayana alisema: "those who cannot remember the past, are condemned to repeat it".

Ushauri wangu kwa wote, someni maandiko ya MSA kwa akili iliyo wazi (open and critical mind) kama kweli mnataka kuelimika kuhusu historia ya Tanganyika. Tafuteni na mengine yaliyoko ili kujithibitishia na kuelimika zaidi. Ya Sheikh Mwaipopo, machawa wote wa CCM na wajinga wengine (wa dini zote) hayahusiki kabisa Katika msimulizi ya MSA. Sijaona MSA akifanya endorsement yoyote kwa watu hao wala misimamo yao ya kijinga. Mnaweza kumfanyia critique (uchambuzi yakinifu) lakini si kumpuuza kabisa.
 
Hii ndio ilitakiwa kuwa TITLE ya Kitabu chako

Hao unaowaita Waislam, sisi tunawatambua kama Wachagga, Wahaya, Wamakonde, Wanyamwezi, Wahehe, Wasukuma, etc
Mzee wa hovyo sana huyu. Mtu umri umeenda anahangaika kufunza vijana mambo ya kipuuzi ambayo yatatengeza mazingira magumu kwao kuishi pamoja na wengine.
Mzee ni MDINI.
 
Hii ndio HOJA yenyewe. Tatizo ni chama dola - CCM. udini, kanda, uzanzibari, n.k. vinatumika tu kupambana na wanaopinga chama dola na magenge yake kuendelea kuhodhi madaraka na mamlaka kinyume cha katiba ya JMT. Kama kuna malalamiko basi yaelekezwe kwenye kupambana na mfumo wa chama dola unaoendelea kulitesa taifa. Huo mfumo umehodhi rasilimali, mamlaka, fikra na tunu zote za taifa na kuwahamasisha wananchi kufukuzia mizuka (ghosts) ya udini, uzanzibari, mabeberu, wapinzani, wasaliti, vibaraka, n.k. kama ndio sababu za matatizo yao badala ya kupambana na tatizo lenyewe.

Mleta mada, MSA, anachofanya ni kuziba pengo kubwa lililoko kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika. Nimesoma baadhi ya maandiko yake na ya waandishi mbalimbali wa nje kuhusu historia ya Nyerere, TANU na Tanganyika ambayo yanathibitisha pengo hilo ambalo ni kama liliwekwa kwa makusudi pengine "kuwarahisishia" Watanzania wasisumbuke sana na historia ya nchi yao bali wazingatie zaidi yajayo - labda kwa lengo maalum alilolijua Nyerere na watu wake.

Sijaona uthibitisho wowote wa MSA kudhamiria kuleta udini kwenye maandiko yake. Maandiko yake ni ya muda mrefu na hayajawahi kuleta shida. Tatizo ni kuwa wengi wa watu muhimu (notable historical figures) katika pengo lililopo kwenye historia ya nchi hii ni waislamu. Wako wakristo wachache pia ambao vijana wengi hawajahi kuwasikia au kujua habari zao kama kina: J. P. Kasella Bantu, C.K. Tumbo, J. Rupia, Alexander M. Tobias, Dr Michael Lugazia, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo, Patrick Aoko, n.k..

Bahati mbaya yako mengi sana ambayo, kwa bahati mbaya, yamo kwenye vitabu vilivyoandikwa kwa undani kwa kiingereza ambacho hapa kwetu ni ugomvi mwingine. Na kwamba siku hizi vijana wengi hawana muda wa kusoma vitabu bali hutegemea zaidi kupata habari toka JF, Facebook, instagram, X, n.k. ni suala jingine.

Yawezekana MSA kawekeza zaidi katika kuandika yanayohusu "wazee wake" wa Mzizima waliosahaulika au kufutwa kabisa katika historia Tanganyika na hivyo kuonekana "mdini". Na hao Indio walikuwa wengi zaidi na instrumental katika kuanzisha TAA baadaye TANU. (Naongezea pia klabu za Simba na Yanga). Hivyo, naweza kuzielewa hisia hizo za MSA.

Naamini kulikuwa na namna Serikali ingeweza kuweka sawa mambo haya katika mizania ya historia rasmi ya taifa iliyochapishwa badala ya kuyafunikafunika tu. Na ndio hivyo hivyo ilivyofanyika kuhusu masuala ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano na kuyapelekea kuyafanya NYETI sana hadi yakageuka kuwa moto mkali kuanzia visiwani kwenyewe hadi sasa "Tanganyika". Mhispania George Santayana alisema: "those who cannot remember the past, are condemned to repeat it".

Ushauri wangu kwa wote, someni maandiko ya MSA kwa akili iliyo wazi (open and critical mind) kama kweli mnataka kuelimika kuhusu historia ya Tanganyika. Tafuteni na mengine yaliyoko ili kujithibitishia na kuelimika zaidi. Ya Sheikh Mwaipopo, machawa wote wa CCM na wajinga wengine (wa dini zote) hayahusiki kabisa Katika msimulizi ya MSA. Sijaona MSA akifanya endorsement yoyote kwa watu hao wala misimamo yao ya kijinga. Mnaweza kumfanyia critique (uchambuzi yakinifu) lakini si kumpuuza kabisa.
Na wewe bado haujaelewa hata kidogo sisi tunamuhoji nini huyu mzee wako.

So Tanzania nzima movement ilikuwa ni TAA?🤔 Ninyi mnataka kuiandika upya historia ya TANGANYIKA mnadhani sisi hatujaisoma?

Huyu mzee ni msanii na anatumika kutengeneza ajenda ya uislam na udini iingie katika mifumo ya elimu na taifa. Hapo kichwani mwake anajiona ni descendant wa waarabu, hana ubantu hata kidogo huyu mzee namna alivyo msalitii.

Muogope sana mtu anaekana asili yake na kujifananisha au kujinasibisha kwa asili nyingine. Huyu mzee na waaarabu huwezi mwambia kitu anaona wale ndio super human beings na ndio maana anapambana sana na dini ya waarabu ishike mamlaka. Huu ni udini na pia ni ushamba.

Huko Kilimanjaro kulikuwa na vyama kibao, iringa,mbeya mwanza, na mikoa mingine mingi kulikuwa na harakati za uhuru na wanainchi walijiunga na hivi vyama kuperform harakati.

Nyerere alijitahidi kuviunganisha na kutengeneza one movement isiyo na makundi.

Huyu mzee wa hovyo anatoka huko na kuanza kuibua mjadala wa kipuuzi kuwa waislam ndio chanzo cha uhuru,wewe mzee unawajua wachagga wewe na vyama vyao vya enzi za uhuru? Unawajua machifu wa MBEYA na harakati zao?

Mzee anataka kutumia mbinu ya kizamani sana kwamba yeye ni mzee na kaona mengi na anajua uhalisia wa mambo? Wazee wa namna hii ukiwaachia jukwaa hawachelewi kutengeneza story na kuunda ukweli wao wao. Na anauamini.

Huyu mzee advantage aliyonayo ni kuwa ana miaka 70 duniani na amekuwapo nayakati za uhuru. Sasa anataka kutumia hiyo nafasi kujinasibisha kama mwanahistoria anayejua historia ya msingi ya taifa hili.

Ukitaka kumjua mtanganyika mzalendo tazama anavyoiongelea TANGANYIKA ya sasa.

Huyu mzee anataka hii inchi historia yake iandikwe kwa mtazamo wake of which ni jambo la kipumbavu sana kutaka watu wachukue sehemu ya ukweli mdogo na kuugeuza ni ukweli mkuu?

Tukisema kila mkoa utoe historia yake ya mchango wa harakati za uhuru hicho kitabu cha Historia ya uhuru si kitajaa majina tupu.

Kila mtu hawezi andikwa katika historia kwa wasifu wake tena kwa mapana ikifanyika hivyo then hiyo itakiwa historia ya ajabu kuwahi kuandikwa kuhusu uhuru wa taifa lolote.

Ndio maana kuna mataifa raia wake walipigana vita na wanawakumbuka ila wameweka tu majina yao katika ubao wa memorials kuwatambua basi. Haimaanishi kuwa hawana uzito katika historia bali ni utawaandika wangapi?
 
Orodha yote ya wapigania Uhuru mpaka kina Kinjekitile Ngwale, Mkwawa, Mirambo, na Mangungo hana habari nao

Hao kina Sykes hatujawahi kusikia wamepigana vita yoyote wala resistance yoyote.

Stori inaanzia Gerezani tu
 
Imagine watu walikuwa wanapambana na mkoloni kwa silaha sio mikwala wala maneno halafu huyu mzee anakuja na story zake za kufuma.

Kusikiliza na kusoma mawazo na fikra za mtu ni jambo zuri,ila kusoma bila kuchakata huo ndio uzwazwa.

Huyu mzee anataka tusome na kumeza tu anachoandika hapa jukwaani bila kumchallenge taarifa zake. Hivi inawezekana vipi Tanzania nzima iwe ni waislamu karne ya 21 mwaka 2026?😂😂

Unatakiwa kuwa na akili za kitoto sana kuwa na akili za namna ya huyu mzee anavyoitazama dunia katika mtazamo wa kidini.

Tumeishi miaka yote hii karibu sabini tukichangamana yeye kwake hilo ni tatizo,anataka aondoke duniani ameacha mbegu ya chuki namna alivyokosa hekima za mtu mzima.

Vijana msimuamini kila mtu mzima kwasasa hata watu wa hovyo pia huzeeka na akili zao.

Huyu mzee ni dhahiri ana chuki dhidi ya uafrika na anahusudu sana waarabu kama mabwana na viongozi wake. Huyu mzee anawatazama waarabu kama first class humans (angejua ukweli wa waarabu sijui angesemaje). Angekuwa marekani wangemuita "Uncle Tom" kumaanisha mtu anaye tetea "white people supremacy ". Huyu sasa tutamwita Mzee Tiputipu kwa maana anawaabudu waarabu under the disguise ya dini ya uislamu.

Anachofanya hapa ni propaganda project kusimika fikra na mitazamo yake katika akili za vijana wa sasa. Asichokijua ni kuwa miaka hii ni ngumu sana kumbrainwash kijana yoyote yule wakati vyanzo vya taarifa vimejaa tele.

Mzee ni mpindisha ukweli, msuka taarifa,mficha taarifa,msema kweli nusu,mdini,na aidha hana taarifa za ukweli au anazo ila kazificha.

Atuambie hapa,je, Tanganyika nzima ilikuwa under huyo mzee skykes na TAA?

Kwamba TANGANYIKA nzima hakukuwa na organization zingine za uhuru both formally organized na informally organized? Kama wakina kinjeketile hawakuwa wanakwenda na documents wao ni ngumi mkononi? Wangoni,wasukuma,wajita,hao wote hawakuwa na documented movements je na wao amewaongelea?

Mzee ni mdini,muongo na MFITINISHAJI.
 
Orodha yote ya wapigania Uhuru mpaka kina Kinjekitile Ngwale, Mkwawa, Mirambo, na Mangungo hana habari nao

Hao kina Sykes hatujawahi kusikia wamepigana vita yoyote wala resistance yoyote.

Stori inaanzia Gerezani tu
Mpwimbe,
Naam.

Historia ya African Association inaanza nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Ndanda, Mission Quarter.

Hapa ndipo walipokusanyika waasisi wa chama hicho mwaka wa 1929.

Waasisi wa African Association ni Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Gerezani inaingia zaidi kwa kuwa Kleist Sykes alikuwa anaishi Mtaa wa Kupata na watoto wake waliishi hapo na walishiriki katika uongozi wa African Association hadi kuasisi chama cha TANU.

Lakini zaidi pia ni kuwa Dossa Aziz alikuwa anaishi Mtaa wa Mbaruku na Congo na mitaa hii Iko Gerezani.
Halikadhalika Ibrahim Hamisi mmoja katika waasisi wa African Association alikuwa anaishi Mtaa wa Kipata.

Clement Mohamed Mtamila alikuwa anaishi Mtaa wa Kipata.
Clement Mtamila alikuwa Secretary wa African Association Rais akiwa Thomas Saudtz Plantan.

Uongozi huu wa wazee ulipinduliwa mwaka wa 1950 na uongozi mpya wa vijana ukachukua madaraka Dr. Vedasto Kyaruzi akawa President na Abdulwahid Sykes, Secretary.

Barua ya Kamati Kuu ya TANU kujadili barua aliyoandikiwa Nyerere na waajiri wake Wamishionari achague kazi yake ya ualimu au TANU kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Clement Mtamila Mtaa wa Kipata.

Wakati huo Clement Mtamila alikuwa Mwenyekiti wa TANU.
Bi. Tatu bint Mzee alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU na alihudhuria kikao hicho.

Bi. Tatu bint Mzee alikuwa akiishi Mtaa wa Kirk.

Ramadhani Mashado Plantan aliyekuwa akichapa gazeti la Waafrika Zuhra alikuwa mkazi wa Mtaa wa Kiungani, Gerezani.

Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyeji sana Mtaa wa Kipata na Mtaa wa Mbaruku na Congo.

Bi. Mugaya Nyang'ombe mama yake Nyerere alipohamia Dar es Salaam yeye na mwanae Sophia wakawa hawapungui nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa, mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes Mtaa wa Kirk nao pia uko Gerezani.

Majina yote niliyotaja hapa kwa njia moja au nyingine ni sehemu ya historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na hawa ndiyo chanzo cha chama cha TANU.

Huwezi kuiondoa TANU na harakati za kudai uhuru Gerezani.
 
Mpwimbe,
Naam.

Historia ya African Association inaanza nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Ndanda, Mission Quarter.

Hapa ndipo walipokusanyika waasisi wa chama hicho mwaka wa 1929.

Waasisi wa African Association ni Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Gerezani inaingia zaidi kwa kuwa Kleist Sykes alikuwa anaishi Mtaa wa Kupata na watoto wake waliishi hapo na walishiriki katika uongozi wa African Association hadi kuasisi chama cha TANU.

Lakini zaidi pia ni kuwa Dossa Aziz alikuwa anaishi Mtaa wa Mbaruku na Congo na mitaa hii Iko Gerezani.

Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyeji sana Mtaa wa Kipata na Mtaa wa Mbaruku na Congo.

Bi. Mugaya Nyang'ombe mama yake Nyerere alipohamia Dar es Salaam yeye na mwanae Sophia wakawa hawapungui nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa, mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes Mtaa wa Kirk nao pia uko Gerezani.

Majina yote niliyotaja hapa kwa njia moja au nyingine ni sehemu ya historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na hawa ndiyo chanzo cha chama cha TANU.

Huwezi kuiondoa TANU Gerezani.
Hao wazee ni wazee wema, wenye utu.

Sidhani kama wema wao ulitokana na DINI.

Nadhni, Nyerere angeweka Kambi Kilimanjaro, leo tungesema CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO ndio wapigania Uhuru, baada ya kumkaribisha Nyerere.

Hali ya nchi iko vibaya sana kwasasa, kama Waislam walipigania Uhuru kwanini hatuoni mapambano hayo leo, badala yake tunaona ULAJI, WIZI na MAUAJI tu.
 
Umemuuliza maswali ya msingi sana. Anajaribu kujenga hoja ila anajidhihirisha tena mwenyewe ndani ya hiyo hoja kuwa ni mdini.
 
Nyakubonga,
Unadhani ushahidi huo wako unaweza kunitia mimi hatiani mahakamani?

Unajua kuna hotuba Mwalimu Nyerere alisema, " Wakristo tulikuwa mimi na John Rupia?"
Nani akushitaki mahakamani?

Najaribu kukuonesha madhara ya kalamu yako tu...
 
Hao wazee ni wazee wema, wenye utu.

Sidhani kama wema wao ulitokana na DINI.

Nadhni, Nyerere angeweka Kambi Kilimanjaro, leo tungesema CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO ndio wapigania Uhuru, baada ya kumkaribisha Nyerere.

Hali ya nchi iko vibaya sana kwasasa, kama Waislam walipigania Uhuru kwanini hatuoni mapambano hayo leo, badala yake tunaona ULAJI, WIZI na MAUAJI tu.
Mpwimbe,
Kuna maswali mimi sina majibu yake.
Utaalamu wangu uko kwenye historia ya Tanganyika.
 
Nani akushitaki mahakamani?

Najaribu kukuonesha madhara ya kalamu yako tu...
Nyakubonga,
Nimeandika vitabu na mada nyingi toka ujana wangu na hakuna hata moja iliyokataliwa kwa kuwa ilikuwa ina hatarisha amani ya nchi.
 
Mpwimbe,
Kuna maswali mimi sina majibu yake.

Utaalamu wangu uko kwenye historia ya Tanganyika.
Iko wapi hiyo historia?

Mbona tunaona historia ya Sykes peke yake.

Au historia ya Sykes ndio historia ya Tanganyika??

Maana hata historia ya Nyerere siyo historia ya Tanganyika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom