Kila mtu anaandika anachoweza sisi tunatazama ukweli wa unachosema.
Maandiko yako yana ukweli ila umeyafunga katika bahasha ya upotoshaji.
Wewe hauna tofauti na Mama wa familia ambaye anaachiwa matumizi na baba alfajiri kabla jua halijachomoza kisha yeye ndie wa kuwapatia watoto matunzo halafu miaka ikishaenda anawaambia watoto kuwa yeye ndie amewatunza siku zote kwa kuwapa chakula,kuwapeleka hospitali,kuwauguza,kuwanunulia mavazi,kuwapa madaftari na kila kitu.
Na watoto wasio na akili ya kujiuliza watasema ni kweli mama ndie kila kitu baba hajafanya lolote nani kama Mama.
Kumbe ukweli ni mama aliiandika historia kwa kutumia matukio muhimu na kuna matukio hakuhadithia watoto ukweli kama kusema baba ndie mlipa bili ya kila kitu na mlinzi wa familia.
Wewe umeandika historia na kutaka kuwaaminisha watanganyika kiwa mzee Sykes na waislamu wa wakati huo ndio wapigania uhuru halisi wa TANGANYIKA ila maswali ya msingi haujibu.
1. Kwanini walimuweka Nyerere mbele kwani wao wangesimama ingeshindikana udai uhuru?
Umejitetea kule juu kwa kusema sababu ya Waislam na chama chao cha TAA kumsimika nyerere ni kwasababu hawakutaka chama kionekane cha kidini( huu ni uongo wa mchana kweupe ambao umeufubricate kwa kichwa chako ila sio marejeo ya kihistoria,kama ni kweli tupe marejeo ya kikao kilichokuja na maamuzi hayo,nje ya hapo acha unafiki wewe mzee usiye na nia nzuri na watanganyika)
2. Unasema Nyerere alipora mchakato, kwahiyo alipopora why hakukuwa na resistance? Bibi titi na baadhi walishajaribu kupora madaraka na ushahidi upo hata wanachama wa miaka hiyo walimsema sana kama msaliti na yeye alikiri na kuomba msamaha,wewe tupe ushahidi wa kuporwa mchakato wa uhuru.
3. TANGANYIKA nzima ina makabila zaidi ya 120 ambayo kihistoria yalipambana na wakoloni independently bila kuungana,haya utuambie wewe ikawaje haya makibila yote yamtambue Nyerere ila wewe kutwa kuchwa unamuweka Sykes kama ndie Nyerere original,kwamba Sykes alizunguka TANGANYIKA zima halafu points tano akachukua nyerere, we mzee upo serious kweli na maisha yako uliyoishi duniani unayatumia kutudanganya wajukuu zao aibu hauna ptuuuuuuuuuh.
4. Nyerere maandiko yake na shughuli zake zipo documented wewe mbona shughuli mzee Sykes za uhuru unaziongelea wewe as if yeye hakuwa akijua umuhimu wa mchango wake? Kuna sehemu aliandika kulalamikia hilo au wewe na kimbelembele chako na huu uandishi wako wa miaka zaidi ya 28 unakazania kumpigia Debe mtu ambaye si baba yako wala mzazi wako,familia yake wapo kimya wewe kutwa nzima kututengenezea visa na hekaya za abunuasi hapa,why unatia aibu namna hii?
Naweka rekodi sawa hapa. Wazee wetu wa dar es salaam sio waislamu ,wazee wa dar es salaam pamoja na miji mingine kama Kilimanjaro,tabora,mtwara na kwengineko chini ya uongozi wa kikakamavu wa baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliongoza raia wenzao katika harakati za kupigania uhuru na hatimae kufanikisha kuupata.
Hizi mbaga zako za uchambuzi wa nani alifanya nini ndio mwanzo wa utapeli wako. Kama unaowataja walifanya kazi kubwa then tuambie ilikuwaje jamii isiwatambue na kuwafuta katika vitabu vya historia muhimu ukizingatia walikuwa na uzito mkubwa sana katika harakati.
Wewe mzee hauchelewi kuja kumfuta maria sarungi katika historia ya mapambano dhidi ya udhalimu wa CCM halafu ukaja kuweka sheikh ponda na zitto kabwe kuwa ndie waliongoza mapambano dhidi udhalimu wa ccm.
We mzee ni tapeli tapeli sana. Na natamani tukutane kwenye mdahalo nakwambia utaondoka umeufyata na utanuna mwezi mzima maana nitakukaanga kwa hoja nzito na maswali lazima utakaaa chini.
Hebu usituchafulie historia ya TANGANYIKA yetu. Acha upuuzi kabisa mzee.
Zemanda,
1. Abdul Sykes angechukua uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954
wakaunda TANU na Abdul Sykes akawa President wa TANU ingekuwa ndiyo
yale yale TANU haina tofauti na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja
wa Waislam wa Tanganyika).
2. Sijasema popote Nyerere ''alipora.''
Hiyo si lugha yangu.
3. "Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":
"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."
“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”
(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda).
4.
Kulia ni Kleist Sykes 1894 - 1949 (Secretary) na Mzee bin Sudi 1896 - 1972 (President) African Assocation na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) |
Ukurasa Kutoka Kitabu, ''Modern Tanzanians,'' Kilichohaririwa na John Iliffe Mwandishi ni Daisy Sykes mtoto wa Abdul Sykes na mjukuu wa Kleist Sykes kutoka sura ''The Townsman: Kleist Sykes.'' Seminar Paper (1968)ipo East Africana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Zemanda,
Mimi nimesoma historia hii na nimetafiti na kuandika na nimeizungumza kwenye vyuo vikuu ndani na nje ya Tanzania.
Sibahatishi.
Kitabu: ''Nyerere Biography'' imetaja maktaba tatu zilizosheheni historia ya Julius Nyerere:
Maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Maktaba ya Mohamed Said na Maktaba ya Brig. General
Hashim Mbita.
Nilijumuishwa katika watu ambao waandishi wa ''Nyerere Biography'' waliwahoji kuhusu Nyerere.
Walitaka kujua siku za mwanzo Nyerere alipofika Dar es Salaam na kwa hakika hii ni historia ya
Nyerere na Abdul Sykes.
Mbali na mahojiano niliwapa na baadhi ya Nyaraka za Sykes walizoziomba.
Nilihojiwa na Jopo la Waandishi (Prof. Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wanza Kamata) mara mbili.
Prof. Shivji na Prof. Saida Yahya Othman
Nyaraka za Sykes niliyoipa Jopo la Waandishi wa ''Nyerere Biography''
Mengine nimeamua kuwa kimya kwa kuwa naona lugha zimekuwa kali:
''We mzee ni tapeli tapeli sana. Na natamani tukutane kwenye mdahalo nakwambia utaondoka umeufyata na utanuna mwezi mzima maana nitakukaanga kwa hoja nzito na maswali lazima utakaaa chini.
Hebu usituchafulie historia ya TANGANYIKA yetu. Acha upuuzi kabisa mzee.''