Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Yaani namhurumia mtoto tu, maskini
Alilia sana kuona babaake nanyang'anyiwa mithili ya kitoweo hadi askari wa kike wakapata huruma, pia amesaidia maana waliona ni vigumu wahalifu kutembea na mtoto mdogo.....muda wote alilia baba...baba...twende nyumbani!
 
Kutokana na sikukuu iliyo mbele yetu ya Eid el haji, nilifunga safari kuelekea Tanga ambapo ndiyo chimbuko la ukoo wangu.

Nilifika salama salmini na kwa kuwa niliwahi kuanza ujenzi siku za nyuma huko maeneo ya Mabokweni (mji ulio mbele ya Amboni na ni halmashauri ya Jiji la Tanga) nikaona nichukue nafasi hii nikamalizie kabisa kwa kuweka madirisha na milango ili nimweke japo mtu akae kwa kuwa sina malengo ya kuishi huko kwa sasa.

Kazi imeanza jana na leo ilikuwa ni siku ya kumaliza shughuli hiyo hivyo niliondoka na mafundi wangu asubuhi na kuelekea kwenye ujenzi, ilipofika jioni kama saa kumi na mbili na nusu kazi ikawa imekwisha hivyo tukaanza safari ya kurudi.

Nilikuwa na gari aina ya Carina nikiendesha huku ndani nikiwa mimi , mtoto wa kiume wa dada yangu wa miaka kama 21, mwanangu wa kiume wa miaka minne pamoja na mafundi watatu.

Ilikuwa ni safari yenye maongezi na furaha huku kukiwa na mziki mzito kutoka katika gari na nikiendesha kwa mwendo wa taratibu tu, ila kufika maeneo ya Mikocheni (karibu na amboni) nikasimamishwa na askari mmoja aliyesimama katikati ya barabara huku pembeni kuna gari ya polisi aina ya Land rover.

Nilianza kusimama lakini nikakumbuka leseni yangu imekwisha muda mrefu hivyo baada ya kujadiliana na wenzangu wakanipa moyo kuwa TEMBEA.

Nikaondoka taratibu ila kufika mbele kidogo nikagundua lile Land Rover linakuja kwa kasi kunifuata, hapa nikajikuta akili haipo na wenzangu wamechanganyikiwa pia hivyo nikaongeza speed zaidi na kujikuta kila ninavyotembea lakini ile gari bado naiona hali iliyopelekea kuitembeza gari kwa speed ya kutisha na bado nikihisi haitembei.

Hali ilikuwa ya kutisha maana pamoja na kuwa barabarani miaka mingi lakini hapa nilinusa harufu ya kufa (wanaoijua njia hiyo wanatambua vema namna ilivyo), hata hivyo tukashauriana na kuona ni bora niingie njia ya mtaani na mpaka hapo jamaa niliwaacha mbali sana lakini cha ajabu nilipoingia njia hiyo tu kwa kuwa kulikuwa na taa taa nikawaona wakiwa nao wanakuja kwa kasi na nusura wagonge watu watatu! Kwa kuwa njia ile ilikuwa mbaya sana na mashimo makubwa niona nizunguke na kuingia tena kwenye lami na nikanyooka tena, ni hofu kubwa niliyonayo na haswa ukizingatia nilijua hayatakuwa hayo yote hivyo nikajikuta sina ujasiri haswa kwa hofu ya kuiangusha gari maana speed ilishanipa wasiwasi.

Ghafla nikawaona jamaa wakiwa karibu kabisa na hapo nikaamua mwenyewe nipaki pembeni na wao wakapaki kwa mbele yetu na kuruka kwa kasi na kuivamia gari yetu huku wakiwa kama nane na bunduki mkononi.

Tukapigwa sana na kubebwa juu juu na kupakizwa katika bodi la gari yao huku kipigo cha bakora, makofi na virungu vikiendelea, wakasema nimewasumbua sana na kufika pale walishakoki bunduki ili kutushambulia iwe ni matairi au hata sisi......wakasema kwamba moja kwa moja walihisi sisi ni magaidi toka mapangoni na kuniadhibu sana huku wakiniuliza kwa nini nikimbie wakati najua wazi hali ilivyo hapa Tanga hivyo tungekufa kwa uzembe! Pia wakanilaumu kwa wao kuwakosa kosa watu kuwagonga,

Wenzangu wakaendelea kupigwa huku wamelala kwenye bodi na mimi nikatolewa nje chini ya ulinzi na kuambiwa niiwashe gari yangu maana niliizima na kuiwasha inataka maujanja maana switch haifanyi kazi, nikaiwasha na wakaiendesha wao na mimi nikapakizwa mbele katika gari la polisi.

Hatua kadhaa mbele tukakutana na gari nyingine mbili za polisi zikitoka Tanga mjini na tukasimama, kumbe mawasiliano yalifanyika wakati nawatoka polisi hivyo hawa walikuja kuniwekea target.

Hapo gari ikafunguliwa buti na kuanza kuipekua wakakuta tu kigunia kidogo cha mkaa na vifaa vya mafundi, hawakuridhika mkaa wakaumwaga wote kujiridhisha, wakachukua speak tyre na kuitoa upepo ili kujiridhisha na pia wakaipekua gari yote kila mahali lakini hawajakuta chochote kibaya.

Wakasema wao wanakuwa doria kwa sababu ya hali ya usalama eneo lile na pia kuzuia mirungi toka Kenya.

Nilijikaza kiume kwa kuona 'nimeshayakanyaga' na kuomba tuyajenge ila ilikuwa mbinde maana walishakuwa si chini ya thelathini wanawake kwa wanaume maana wengine walikuja kwa gari ndogo aina ya Mark x.......muda wote huo mwanangu alikuwa akilia sana kuona babaake nikila makofi hali iliyopelekea askari wa kike kupatwa na huruma na kukaribisha mazungumzo.

Niliyamaliza ki utu uzima na tukapewa gari yetu na kuendelea na safari japo wenzangu kule kumbe walichezea virungu zaidi.

Najiuliza iwapo ningeitia gari darajani kwa mwendo ule pengine tungekuwa chumba cha maiti sasa......najiuliza iwapo wangemimina risasi kwa mimi kukaidi agizo lao la kusimama, saa hizi tungekuwa chumba cha maiti......najiuliza kwa nini nisinge simama pale pale tu!
Japo hapa nilipo masikio bado yana mwangwi kwa sababu ya makofi mazito ya mfululizo na magoti yanawaka moto kwa virungu lakini bado naona yangekuwa makubwa zaidi hivyo nimejifunza mengi na namshukuru Mungu kwa yote.

KWELI KUZALIWA SIKU MOJA NA KUFA SIKU MOJA.
huo ni ujinga unaweza ukala shaba kisa kugopa watakagua leseni ambalo ni kosa dogo tu...nyambafu sana ww
 
Kwanza mkuu nikupe pole kwa kuchezea kadebra kidogo!!!pole nyingine ni kuwa tumeshajua gari lako mbovu switch haifanyi kazi!!(mkuu hapa usinitusi mi mwenyewe sina hata baiskel)pole ingine bhana ni kwa uwoga siku nyingine usifanye hivyo kwani una bahati sana hao askari wamekustiri hawajachukua maamuzi magumu maana vitendea kazi walikuwa navyo!!ila kosa lako lingine umetoa rushwa asee!!! Vipi mkuu uliwapa bei gani!!
Pole zote nazipokea mkuu, na ni kweli switch haikuwa sawa na ndiyo iliyoninusuru nikatolewa mule kwenye bodi na nikaepuka virungu.
 
Kutokana na sikukuu iliyo mbele yetu ya Eid el haji, nilifunga safari kuelekea Tanga ambapo ndiyo chimbuko la ukoo wangu.

Nilifika salama salmini na kwa kuwa niliwahi kuanza ujenzi siku za nyuma huko maeneo ya Mabokweni (mji ulio mbele ya Amboni na ni halmashauri ya Jiji la Tanga) nikaona nichukue nafasi hii nikamalizie kabisa kwa kuweka madirisha na milango ili nimweke japo mtu akae kwa kuwa sina malengo ya kuishi huko kwa sasa.

Kazi imeanza jana na leo ilikuwa ni siku ya kumaliza shughuli hiyo hivyo niliondoka na mafundi wangu asubuhi na kuelekea kwenye ujenzi, ilipofika jioni kama saa kumi na mbili na nusu kazi ikawa imekwisha hivyo tukaanza safari ya kurudi.

Nilikuwa na gari aina ya Carina nikiendesha huku ndani nikiwa mimi , mtoto wa kiume wa dada yangu wa miaka kama 21, mwanangu wa kiume wa miaka minne pamoja na mafundi watatu.

Ilikuwa ni safari yenye maongezi na furaha huku kukiwa na mziki mzito kutoka katika gari na nikiendesha kwa mwendo wa taratibu tu, ila kufika maeneo ya Mikocheni (karibu na amboni) nikasimamishwa na askari mmoja aliyesimama katikati ya barabara huku pembeni kuna gari ya polisi aina ya Land rover.

Nilianza kusimama lakini nikakumbuka leseni yangu imekwisha muda mrefu hivyo baada ya kujadiliana na wenzangu wakanipa moyo kuwa TEMBEA.

Nikaondoka taratibu ila kufika mbele kidogo nikagundua lile Land Rover linakuja kwa kasi kunifuata, hapa nikajikuta akili haipo na wenzangu wamechanganyikiwa pia hivyo nikaongeza speed zaidi na kujikuta kila ninavyotembea lakini ile gari bado naiona hali iliyopelekea kuitembeza gari kwa speed ya kutisha na bado nikihisi haitembei.

Hali ilikuwa ya kutisha maana pamoja na kuwa barabarani miaka mingi lakini hapa nilinusa harufu ya kufa (wanaoijua njia hiyo wanatambua vema namna ilivyo), hata hivyo tukashauriana na kuona ni bora niingie njia ya mtaani na mpaka hapo jamaa niliwaacha mbali sana lakini cha ajabu nilipoingia njia hiyo tu kwa kuwa kulikuwa na taa taa nikawaona wakiwa nao wanakuja kwa kasi na nusura wagonge watu watatu! Kwa kuwa njia ile ilikuwa mbaya sana na mashimo makubwa niona nizunguke na kuingia tena kwenye lami na nikanyooka tena, ni hofu kubwa niliyonayo na haswa ukizingatia nilijua hayatakuwa hayo yote hivyo nikajikuta sina ujasiri haswa kwa hofu ya kuiangusha gari maana speed ilishanipa wasiwasi.

Ghafla nikawaona jamaa wakiwa karibu kabisa na hapo nikaamua mwenyewe nipaki pembeni na wao wakapaki kwa mbele yetu na kuruka kwa kasi na kuivamia gari yetu huku wakiwa kama nane na bunduki mkononi.

Tukapigwa sana na kubebwa juu juu na kupakizwa katika bodi la gari yao huku kipigo cha bakora, makofi na virungu vikiendelea, wakasema nimewasumbua sana na kufika pale walishakoki bunduki ili kutushambulia iwe ni matairi au hata sisi......wakasema kwamba moja kwa moja walihisi sisi ni magaidi toka mapangoni na kuniadhibu sana huku wakiniuliza kwa nini nikimbie wakati najua wazi hali ilivyo hapa Tanga hivyo tungekufa kwa uzembe! Pia wakanilaumu kwa wao kuwakosa kosa watu kuwagonga,

Wenzangu wakaendelea kupigwa huku wamelala kwenye bodi na mimi nikatolewa nje chini ya ulinzi na kuambiwa niiwashe gari yangu maana niliizima na kuiwasha inataka maujanja maana switch haifanyi kazi, nikaiwasha na wakaiendesha wao na mimi nikapakizwa mbele katika gari la polisi.

Hatua kadhaa mbele tukakutana na gari nyingine mbili za polisi zikitoka Tanga mjini na tukasimama, kumbe mawasiliano yalifanyika wakati nawatoka polisi hivyo hawa walikuja kuniwekea target.

Hapo gari ikafunguliwa buti na kuanza kuipekua wakakuta tu kigunia kidogo cha mkaa na vifaa vya mafundi, hawakuridhika mkaa wakaumwaga wote kujiridhisha, wakachukua speak tyre na kuitoa upepo ili kujiridhisha na pia wakaipekua gari yote kila mahali lakini hawajakuta chochote kibaya.

Wakasema wao wanakuwa doria kwa sababu ya hali ya usalama eneo lile na pia kuzuia mirungi toka Kenya.

Nilijikaza kiume kwa kuona 'nimeshayakanyaga' na kuomba tuyajenge ila ilikuwa mbinde maana walishakuwa si chini ya thelathini wanawake kwa wanaume maana wengine walikuja kwa gari ndogo aina ya Mark x.......muda wote huo mwanangu alikuwa akilia sana kuona babaake nikila makofi hali iliyopelekea askari wa kike kupatwa na huruma na kukaribisha mazungumzo.

Niliyamaliza ki utu uzima na tukapewa gari yetu na kuendelea na safari japo wenzangu kule kumbe walichezea virungu zaidi.

Najiuliza iwapo ningeitia gari darajani kwa mwendo ule pengine tungekuwa chumba cha maiti sasa......najiuliza iwapo wangemimina risasi kwa mimi kukaidi agizo lao la kusimama, saa hizi tungekuwa chumba cha maiti......najiuliza kwa nini nisinge simama pale pale tu!
Japo hapa nilipo masikio bado yana mwangwi kwa sababu ya makofi mazito ya mfululizo na magoti yanawaka moto kwa virungu lakini bado naona yangekuwa makubwa zaidi hivyo nimejifunza mengi na namshukuru Mungu kwa yote.

KWELI KUZALIWA SIKU MOJA NA KUFA SIKU MOJA.
Oh! Usiwe unadanganyika humu ndani JF, na maneno sijui Polisiccm na upuuzi mwingine hao makamanda wanapiga kazi na kwa hali ilivyo huko Tanga hadi sasa sijaelewa kwanini ulichukua uamuzi wa kipumbavu kama huo natamani ningekuwa karibu nikuongeze makonzi kwa kuhatarisha maisha ya mtoto mdogo.
 
Pole sana mkuu lkn siku ingine jitaidi kutii sheria bila shuruti
Mkuu akhsante sana, kuanzia sasa hata askari akijikuna shavu ninaweza nikapaki, jambo kubwa nashukuru kulala kwangu mda huu maana hali ilikuwa inatisha.
 
Tukio lako limenikumbusha ajali mbaya ya mti pale Njombe mjini. Kwenye mteremko wa kwenda Njombe mjini ukitoka Kibena Hospital, alisimama askari wa usalama barabarani kwa kazi moja tu kusimamisha magari yasiende Njombe mjini kwa muda. Jamaa mmoja mjanja feki akiwa na Carina aliposimamishwa akakaidi na kuongeza mwendo zaidi, hamadi kwenye kona na mti unaanguka. Mti ukaangukia gari lake na kukandamizwa vibaya.

Yaliyofuata ni historia.
Rip marehemu.....hata mimi nilikuwa speed ya kutisha na bado nikahisi gari haitembei.....kweli yale magari yao yanatembea mno.
 
Yaan lesen unakimbia?!!!
Ila nmecheka sana eti masikio mazito
 
huo ni ujinga unaweza ukala shaba kisa kugopa watakagua leseni ambalo ni kosa dogo tu...nyambafu sana ww
Nikushukuru kwa kuniona nyamafu kwa sababu umeshaujua mwanzo na mwisho.....mimi sikuujua mwisho mpaka yaliponifika na nimeleta hapa kwa nia njema ili wengine yasije wakuta yaishie kwangu tu.
 
Hawa ndio aina ya watanzania, waoga kama kuku, huna akili kabisa, kosa la sh 30,000 linahatarisha maisha! Mjinga kabisa, wakati mimi naendeshaga gari lenye makosa hata zaidi ya matatu toka dar to mikoani bila hata kulipa sent moja!!!
Jiamini wewe hawa ni watz wenzio tu
 
Oh! Usiwe unadanganyika humu ndani JF, na maneno sijui Polisiccm na upuuzi mwingine hao makamanda wanapiga kazi na kwa hali ilivyo huko Tanga hadi sasa sijaelewa kwanini ulichukua uamuzi wa kipumbavu kama huo natamani ningekuwa karibu nikuongeze makonzi kwa kuhatarisha maisha ya mtoto mdogo.
Makonzi au makofi hayakunifanya niwaze bali niliwaza makubwa zaidi ya hapo......hata hivyo hakuna aliyejua kama yangekuwa hayo kati yetu bali nilijua wakinimaind watachukua namba tu.
 
Pole sana mkuu, ila hukujua ulizani watakuuliza lesni, bima na mambo mengine ya barabarani, kumbe wanalengo lingine, Hii inaweza mtokea mtu yeyote hauko peke yako.
Unampa pole mzembe!!!
Kosa hilo faini yake ni tsh 30,000 tu kwanin ahatarishe maisha na akubali ushauri wa watu wasio madereva!
 
Pole sana mkuu, kweli JF kiboko, pamoja na kuchezea kipigo cha mbwa mwizi bado umejikongoja kupost....
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Amepata la kuanzishia uzi
 
Yaan lesen unakimbia?!!!
Ila nmecheka sana eti masikio mazito
Si unajua wazee hawana dogo hata kwa vitu vidogo? Hivyo mambo mengine unaamua kuyahamishia siku nyingine.
Ni kweli masikio mazito kwa makofi kama mpira wa kona.
 
Ee bwana ee! mdigo gani muoga wa polisi hivi 😀?! Unakimbia kwa kutokua na leseni tu na una mtoto mdogo ndani? Sasa mlima ule wa amboni ungeshukaje kwa spidi kali hivyo na chini kuna daraja tena chini yake mto wenye maji na pengine mamba na njia nyembamba! kungekua na magari mengine upande wa pili? Duuh. Hatari sana ulifanya. Hata hivyo pole ndugu.
 
Back
Top Bottom