Ilikua mwaka 1979

Ilikua mwaka 1979

Hiz kitu nilikuwa nasoma magazetin tu miaka hiyo sijui avalon, new chox, empres...
 
Kwani ya leo ni rahisi kupatikana?! . Hii ya leo imeshushwa na uchumi unaokuwa kisiasa na si kiuhalisia.

Nakumbuka miaka nikiwa shule ya msingi 1973 Mwl akinituma kumnunulia nyama buchani kilo shs 1.70 mchanganyiko na steki shs. 2.50, lakini leo shs 6000/= mpaka 9000/=.
Kupatikana hela sasa ni rahisi.ila haina thamani.ukibeba zege haukosi 15000.kwa siku ila matumizi sasa.tofauti na zaman pesa ilikuwa kupatikana ngumu ila ilikuwa na thamani.
 
Mkuu umenikumbusha mbali, huku kwetu tulikuwa na Liberty cinema & Tivoli cinema .
Mwanza hiyo tulikuwa tunaenda kuokota magazeti ya kihindi yenye sura za mastaa ...tukayaita "makava"

Ilikuwa Hatari pale liberty cinema then tukitoka hapo tunakwenda Salama koni kumungunya koni..yule mhindi wa CONI kama hajatajirika ndo basi tena maana lile nyomi pale daah!
 
Kupatikana hela sasa ni rahisi.ila haina thamani.ukibeba zege haukosi 15000.kwa siku ila matumizi sasa.tofauti na zaman pesa ilikuwa kupatikana ngumu ila ilikuwa na thamani.
Sasa kipi kizuri uwe na hela nyingi lakini haina value au uwe na pesa kidogo lakini yenye thamani ??!!. Kitu chochote kizuri ni chenye thamani .

Mwaka 1979 alioutaja mleta hoja ndiyo mambo yalianza kutuharibikia baada ya vita vya Kagera tulipoambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18 lakini hali haikurekebika. Na ukumbuke na tuliingia vita baada tu EAC kuvunjika hivyo uchumi haukurekebika. Na hii ilipelekea pesa yetu kushuka kila wakati.
 
Bora zaman.
 
Inaelekea wengi humu bado vijana wadogo. Kwa wale wa Tanga nafikiri watakuwa wanakumbuka majestic cinema,regal cinema na pale railway barabara ya 3. cc Sky Eclat
 
arusha, ilikuwa ni ELITE CINEMA na METROPOLE CINEMA
 
Kumbe tupo wengi wa miaka ileeeee! Maisha yalikuwa murua jijini. Kulikuwa na restaurant nyingi mjini za wahindi ilikuwa ukikatiza mitaa hiyo samora na pembezoni mwa samora mitaa ya jamhuri mkwepu etc kulikuwa na harufu nzuri sana ya ubwabwa wa viungo unashiba kabla ya kula. Sinema ilikuwa moja ya burudani! them old golden days 😀
 
Back
Top Bottom