Ili uchumi wetu upande tuwekeze kwenye bidhaa mpya

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,345
8,268
Ili uchumi wetu upande tuwekeze kwenye bidhaa mpya.

Gross Domestic Product (GDP) yetu per capital ni ndogo mnoo na hii ni kwasababu hatuzalishi bidhaa mpya bado tupo na bidhaa za zamani zilezile.

Hebu Tujiongeze tuanze kuzalisha bidhaa mpya ambazo zinahitajika na mataifa mbalimbali.

Tuzalishe bidhaa zifuatazo

1. Natural Gas, LNG,
2.Kemikali zinazotokana na gesi mfano mbolea, methanol, n.k
2. Helium,
2. Madini ya Lithium kwaajili ya beteri
3. Madini ya Nickel
4. Madini Cobalt
5. Madini ya platinum
6. Madini ya Chromium
7. Madini ya Manganes
8.Madini ya Copper
9.Nishati

Tukiuza bidhaa hizo zenye thamani tutapata fedha nyingi zitakuza GDP yetu, mwishowe tutajikuta tunaacha kutoza kodi. Lakini hatuwezi kuacha kutoza kodi kwasasa kwasababu hatuna vyanzo mbadala vya mapato ya uhakika ya kuaminika ambayo yanaweza kufinance miradi yetu ya maendeleo na huduma za jamii katika taifa letu.

Hivyo tuweke mikakati huko kwenye bidhaa mpya. Nilikua nikimsiliza Dr. Askofu Kwajima amezungumzia kuhusiana na rasilimali watu ambazo ndio nyenzo muhimu kwenye kuzalisha hizo bidha mpya.

Sasa angalia TANZANIA tumesomesha wataalam wa madini, wataalam wa mafuta na gesi, cha ajabu wote ni jobless, wapo tu watu wanazeeka na maarifa na uwezo wao.

Kampuni ya serikali inaajiri wataalam wawili ndio wazalishe bidhaa mpya, yaani hao ndio walete impact kwenye industry kweli. Lazima tuwe serious tukitaka kufikia uchumi tunaoutaka.

Serikali imesomesha wataalam wa mafuta na gesi wote jobless kwanini isiajiri wataalam hao watafute mafuta na hizo gesi kwa wingi. Badala yake serikali imebaki na wataalam wazee wanakaa tu ofisini no impact in the industry, ajiri vijana waliotoka shule wafanye kazi.
 
Back
Top Bottom