Naibu waziri kigahe: tbs, tmda & sido elimisheni wajasiriamali namna ya kuzalisha bidhaa zenye ubora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amewaagiza wataalam wa uthibitisho wa ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), TMDA na SIDO kuwaelimisha wajasiriamali namna ya kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Mhe. Kigahe amebainisha hayo Oktoba 18, 2023 alipozindua maonesho ya biashara ya Tanzanite wilayani Zindagi mkoani Manyara ambapo pia ameutaka Mkoa wa Manyara na halmashauri zake kuendelea kushirikiana na waratibu wa Bodi ya Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kusogeza huduma karibu ili wajasiriamali washiriki.

Kwa upande mwingine Mhe.Kigahe amezitaka Taasisi za serikali na binafsi zikiboresha mazingira ya uwekezaji kwani zitatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza na kukuza uchumi wa mkoa na Taifa kwa kuwa wataweza kuzalisha bidhaa zitakazopata soko katika masoko ya Dunia.

Mhe. Kigahe pia Amebainisha kuwa uhamasishaji wa umma juu ya bidhaa zinazozalishwa nchini, madini na viwanda mbalimbali utakwwnda kuongezeka.

Aidha, ameutaka mkoa huo kutenga eneo maalum na kuweka miundombinu ya kisasa kwa ajili ya kuboresha maonesho hayo.

Nae Meneja masoko wa Kampuni ya Mati Super Brand Ltd Elvis Peter amesema maonesho hayo yanaunga mkono nia ya serikali ya kuharakisha maendeleo katika kuwasaidia wajasiliamali na wawekezaji kukidhi mahitaji ya jamii.

Na kwa upande wa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Manyara, Musa Msuya ameishukuru serikali kwa kukubali kujenga kiwanja cha ndege katika mkoa huo kwakuwa utaongeza idadi ya wawekezaji na watalii.

F8vbH2BW0AA1EeM.jpg
F8vbISwXUAA28jR.jpg
F8vbL8rWYAAnQ-Z.jpg
F8vbO32WoAEMfTD.jpg
 
Back
Top Bottom