Ili niwe Rubani wa Ndege Nifanyeje?

Kuwa rubani ni kazi kidogo na sio lazima uwe PGM ndio uweze kuwa cha mhimu hesabu na kiingereza.

Na familiya yako iwe na fedha na si vijisent ndo utaweza kusoma Tanzania unaweza kwenda ulizia JNIA terminal one huwa naona kama wapo chuo cha umma nadhani hakuna.mshirikishe mungu sana unaweza ingekuwa ni gharama ndogo marubani wagejaa
 
Mkuu bei ya kusomea hapa Tanzania ni Dola 20,00 upate leseni ya kuwa rubani wa kuendesha ndege za abiria yaaniUganda unaweza kupata kwa dola elfu 10 hadi kumi na tano. hayo ma PGM sijui PCM sio lazima.

Wewe tayarisha hela uchague chuo kati ya MOSSwood kwa Tanzania na Soroti kwa Uganda, pia unaweza kwenda ethiopia na SA ila bei zao ni juu ya hapo, inafika mpaka dola elfu 30. Kwa hiyo wewe jitayarishe tu kifedha, ongea na wazazi na ndugu kama wanaweza kukuchangia
 
Nyongeza tu anza kusomea urubani ukiwa kijana mdogo ili upate muda wa kutosha wa kurusha ndege "Flying hours" hii itakusaidia sana kuelekea kwenye kuwa pilot wa Commercial Airlines kubwa. Kama ukipenda nenda kaanzie private pilot kipo chuo hapo Julius Nyerere Int.

Airport Terminal 1 building. Nafikiri Tropical Air nao walikuwa wanafundisha hiyo kozi. Ukiwa na ubavu nenda South Africa kuna vyuo vizuri.

Unaweza kusomea urubani hata ukiwa navelimu ya form 4 lakini english, math muhimu uvijue ukiimudu na physics ni mtaji mzuri. Jiografia ni mbwembwe tu.
 
Niliangalia documentary ya British Airways walikuwa wanafanya intensive training ya miezi 18, wengine walikuwa na degree nyingine za sayansi lakini uwe una first class.

Course ilikuwa very crucial walianza na theory wakapelekwa kwenye assimilation air line engines wakipass mtihani wanaanza kurusha ndege. Mshahara wa kuanzia ilikuwa £100,000 kwa mwaka.
 
Hizi ndoto nilikua nazo shule ya msingi baada ya siku moja kuona Helicopter ikiruka live, nilifurahi sana, ilinipa changamoto ya kusoma kwa bidii, nahisi ndoto hazikuvuka darasa la 7,
 
Back
Top Bottom