Tanzania leo wanawake wanakufa kwa mimba, nusu ya watoto wa kike hawamalizi elimu ya secondary, Maradhi kama malaria yanaua watoto wasiopungua millioni kila mwaka na kadhalika. Hivyo itazame ilani ya Chadema kwa mengo ya ponya kwanza kabla hujafikiria mbele. Na ndio maana wapo wengi wanaopinga hata Ufisadi kuwa agenda kuu ya Chadema hali wanashindwa kuelewa kwamba huwezi kuweka ahadi ya ELIMU hali nusu ya billioni utakazo allocate zitapotea mifukoni mwa watalawa.
Labda kwa kifupi tu, nizungumzie nilichokielewa mimi:-
Chadema wanapompigia sifa Nyerere ni ktk kukumbuka fikra zake ktk kulijenga Taifa letu. Ni sawa na kusifia architecture blueprint ya nyumba unayotaka kujenga kwa ajili ya familia yako. Sasa makosa ya mwalimu yalikuja ktk Ujenzi wake ambapo tunaweza kusema aliweza kutupa ramani nzuri sana lakini jinsi alivyopanga ku raise fedha za ujenzi wa hilo jengo ndipo tulipokwama..Lakini hii haina maana mpango mzima wa ujenzi wa nyumba hiyo ulikuwa na makosa. QUOTE]
Hili ni tatizo jingine. Haiwezekani uandike kuwa miaka 50 ya CCM (kwa mujibu wa CHADEMA) na ukumbuke nusu ya miaka hiyo Nyerere ndiyo alikuwa kiongozi eti Tanzania imeendelea kuwa katika lindi la umasikini. Halafu mbeleni unasema kuwa aliweka misingi imara. Kamwe haiwezi kuwa misingi imara km haijatufikisha tulipokusudia. Misingi imara ni pamoja uongozi bora. Sasa utaona wanajichanganya. Upande mwingine quotes za Nyerere zinawekwa na upande wa pili anaonekana na yeye kaifikisha nchi hapa tulipo
Binafsi siku zote natumia mfano wa makao makuu ya Dodoma, Tutapingana sana humu janvini lakini binafsi naamini kabisa maamuzi ya kupeleka makao makuu Dodoma was a perfect idea isipokuwa tu ndio hivyo tuli fail kama tulivyofail kiuchumi na tunaendelea ku fail kwa sababu tumeshindwa kurudi nyuma na kutazama malengo ya mwalimu japokuwa alishindwa hata yeye kukamilisha.
Halafu ktk hoja yako ya kuendelea umeshindwa kuelewa kwamba kuendelea kunakozungumziwa ni makuzi ya Kitaifa.. Nchi inaweza kuendelea kwa kusuasua haina maana bado ni mbaya na remote kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita, hapana kila nchi duniani inaendelea kwa kiasi fulani hata huko Haiti au Guinea Biissau wanaendelea ukilinganisha na miaka 50 iliyopita isipokuwa tunapowaweka ktk mzani wanabakia masiokini wa wisho na ndio tunasema ni maendeleo ya kusuasua.QUOTE]
Mkandara nakushauri kwa hili ujipe fursa uipitie ilani km hujafanya hivyo. Maana wanasema kuwa masikini wameongezeka kutoka mil 10-13. Yaani wanaosihi chini ya dola 1 kwa siku. Upande mwingine wanasema wanataka waongeze kasi ya maendeleo kutoka taratibu kwenda kwa kasi. Hapo unatetea nini sasa. The arguments are typical contradictory.
Maswala mengine ya Elimu na Afya nadhani Chadema wako karibu na jamii zaidi yangu mimi na wewe hivyo siwezi kuwapinga zaidi ya kuwasikiliza wananchi wapiga kura. Nimeona watu wakipinga kabisa elimu na Afya ya bure, lakini nchi nyingi zilizoendelea zimetokea huko. Hawakuvamia elimu na afya ya kulipia wakati wakiwa ndani ya matatizo tena basi hizo shule na Hospital za makanisa ndizo zilikuwa bure zamani kupinga mfumo wa kulipia baada ya nchi nyingi za Ulaya ku adapt system ya kulipia.
Hivyo utakuta kwamba sisi tumerukia na kudandia hili treni la kulipia wakati sisi bado ni Wajinga wengi kuliko wasomi, maskini wasiokuwa na uwezo kuliko wenye uwezo tena kwa asilmia zaidi ya 70..Nusu ya wananchi wetu wenye uwezo wa kufanya kazi hawana kazi kutokana na kutokuwa na elimu..Na hata wale waliosoma wamesoma ili wapatiwe ajira ambazo ni adimu badala ya kuwa wao kuwa wabunifu wa vifaa ambavyo vitakidhi mahitaji yetu na nje.
Kwa hiyo tuna kila sababu ya kuomba maendeleo ya haraka ktk sekta ambazo ni muhimu sana hasa Elimu, Afya na Ajira. Na hivi vitu haviwezi kupatikana pasipo kuweka malengo ya juu zaidi kiasi kwamba hata nusu yake ikifanikiwa basi tutakuwa tumepiga hatua zaidi ya kusuasua.QUOTE]
Mwisho nakubaliana na wewe, Watanzania wanayahitaji saana maendeleo kuliko kipindi kingine chochote ambayo pia yanaweza kuainishwa kiuhalisia na kiukweli.