Ilani ya CCM Uchaguzi 2010.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya CCM Uchaguzi 2010....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 24, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Angalia kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010 yafuatayo ni mafanikio ya miaka mitano ya kwanza ya Ari, Kasi Nguvu Mpya.

  1. Mtanzania wa kwanza kufanya kazi Ikulu ya Obama
  2. Mtanzania wa Kwanza kucheza NBA
  3. Mtanzania Nusu wa Kwanza kwenda nje ya Sayari
  4. Bendera ya Tanzania imefika Mwezini na kujulishwa kwa wawekezaji kutoka Mars
  5. Rais wa Kwanza kutoka Tanzania kugonga nyundo ya soko la mitaji NASDAQ
  6. Rais wa kwanza kumleta Rais wa Marekani kutembelea nchi
  7. Rais wa Kwanza kuongea na Watanzania kutumia Tovuti, Luninga na Simu kwa wakati mmoja


  Endeleza listi....
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Rais wa kwanza kuwaadhibu wafanyakazi wa BOT watovu wa nidhamu kwa pesa ya Serikali.
  Rais wa kwanza wa Tanzania kutembelea nchi nyingi Duniani(Marekani ndio kama Nyumbani)
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  ..kuoa wake wawili zaidi....na vimada kibao.....

  si mumeona juzi ...last week yote alikuw likizo ngorongoro ..na mama ziara ya kitaifa morogoro..[offcourse akipokewa na mkuu wa mkoa na viongozi wote na kukaa naye wiki nzima .....nadhani Pinda ambaye piya alikuwa morogoro alikosa uzito..tuseme kikatiba nafasi ya mke wa rais ipo juu ya waziri mkuu..auuu]....na mama ni mkarimu sana amewaacha wenzake wawili wafurahiye likizo na mzee ngorongoro hana hiyana ...naomba kinamama wengine muige mfano wake....ila pia muda umefika sasa kwa muhashimiwa kuwatambulisha rasmi wake zake wapya...atakuwa hajavunja sheria yeyote ..dini inaruhusu na atakuwa anaonesha mfano mwema wa kuwa muwazi......kuliko kufanya kama anajifisha wakati ni wake zake...
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Hi kali sio mchezo
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehehehe we philemon naona unafaa kuwa mwandishi wa masuala binafsi ya muungwana hehehe (uteuzi utafanyika hivi karibuni) hehehe u made my day.
  nimeipenda hiyo bold

  listi inaendelea.....

  8. Rais wa kwanza kutoka Tanzania kuingia fainali ya marais wenye mvuto duniani
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mchungaji siku hizi haeleweki ... ???!!!!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Rais wa kwanza Afrika kuonyesha tabasamu muda wote hata pale pasipostahili! 2. Rais wa kwanza Afrika kukataa ushauri wa Madaktari wake!
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  1.Rais wa kwanza kuwapeleka vigogo mahakamani,(Yona,Mgonja, Mramba etc),
  2. Rais wa Kwanza kujenga chuo kikuu cha serikali cn=henye uwezo wa kuchukua wananfunzi 40,000 p.a
  3. Rais wa kwanza kumtosa waziri mkuu wake??
   
 9. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  1. Raisi ya kwanza kuingilia kazi za mihimili mingine ya dola - hadi kusamehe waizi wa mali za umma na kula na mafisadi.

  2.Raisi wa kwanza kuambiwa kwamba amewekwa mfukoni yy na serikali yake lakini anachekelea tu.
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ila mkuu kishoka umekuwa ABSTRACT sana siku chache hizi, vipi umeshachukua uamuzi wa kujipima ubavu na mhishimiwa?
   
 11. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  chuo hicho hakiwezi hata kuimili wanafunzi 7,000 wewe unaongelea elfu kumi
  nyerere na mwinyi wamewatosa mawaziri wakuu kibao

  rais wa kwanza kuingia madarakani kutumia pesa za wizi kutoka benki kuu
   
 12. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Rais wa kwanza kuwa na baraza kubwa la mawaziri.

  List inaendelea...
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Msanii,

  Siku moja nikiwa Dar, nilikuwa natoka msibani Kwembe narudi zangu Ubungo.

  Tulipofika pale Mbezi Louis, tukaanza foleni ya kuja Dar tena kubwa na ilikuwa Jumamosi takriban Saa 12 na nusu Usiku.

  Upande wa pili wa magari yanayotoka Dar kwenda mikoani, nako wakasimamishwa.

  Sisi wa kwenda Dar tukaenda kinalenale taratibu, lakini utitiri wa msongamano unaongezeka pande zote mbili. Kufika pale Mbezi kwa Msuguri, hapakuwa na gari lolote kutoka Dar linalokwenda nje ya mji. Sisi nasi tukapigwa stop, hatuondoki.

  Jamaa mmoja akadodosa, "Yawezekana mwenye nchi anarudi jijini"! Nikauliza anatokea wapi? wakasema anatokea kwenye mji wake Msoga ambao ni umbali fulani kutoka Chalinze.

  Pindi si muda, msururu wa magari 22 ukapita fwap, mkukumkuku na vingora tele, roketi launcha na mbwembwe.

  Mwinyi Fuadi akapita akitoka kwenye Kasri yake ya Msoga anaelekea Magogoni.

  Sasa kumbe mwenzetu anapita ile zigizaga. Nilipokuwa nashangaa mbona hakuna magari kutoka Dar, kumbe wao walikuwa wanapisha njia, sawa na Yohana mbatizaji aliposema "yanyoosheni mapito"! na sisi kusimamisha ilikuwa ili huko mbele, msafara wake ucheze mayenu na kutamba ule upande wa kuingia Dar.

  NIkauliza, kwa nini hatumii Helikopta kwenda Msoga?

  Wakaniuliza wenzangu, "kwa nini atumie helikopta na ni gharama na rahisi kutunguliwa?"

  Nikawauliza, je gharama ni ipi kati ya msafara wake kusimamisha mfumo wa Uchukuzi wa kuingia Dar kwa takriban masaa manne ambako hakuna kinachotoka wala kuingia Dar, magari yote yaliyosimama foleni na mafuta yanayoungua? Maana Msoga na Dar ni takriban masaa mawili!

  Nikauliza tena la ziada la kuhusu usalama, nikasema "je usalama wake ukoje kama kwa mwendo huu wa mkukumkuku wa kilometa 100 kwa saa akatokea kiazi au duwanzi mmoja akachomoza akakatisha krosi kisha msafara wote upige breki za afanaleki, je si Taifa tutapigwa kofi la Kelb kama lile la Mzee Mwinyi?

  Jamaa wakacheka, ksiha wakasema nilikuwa sahihi.

  Sasa maana ya mimi kutoa hadithi hii ni hii, Raisi kila wikiendi huenda nyumbani Msoga, na zaidi barabara hufungwa na hakuna gari, basi au lori linapita. KUtoka Dar mpaka Msoga, kila kitu kinachotumia barabara kinatumia masaa ya ziada kumsubiri Mwinyi Fuadi apite.

  Sasa kama yeye anaoina foleni kubwa hizo na jinsi msafara wake unavyoleta shida katika mfumo wa uchukuzi, je ni vipi tuseme kuwa Rais hajui kuwa barabara zetu ni ndogo, kuna foleni kubwa na zinachelewsha mambo mengi?

  NIkajiuliza, ikiwa kuna msongamano mkubwa namna hiyo kisha labda kwa bahati mbaya kuna janga limetoea iwe ni Dar au Chalinze, je itatuchukua muda gani kufika kwenye janga au kama ni kupeleka Jeshi kulinda upande mmoja?

  Hivyo bwana Msanii, katika ABSTRACT ya Mchungaji ni kuonyesha kuwa sisi kama Taifa tunakubali tuu mambo hata yale ya kipuuzi na yasiyo na msingi na kuyainua na kuyaweka kuwa ndio ya msingi!
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda ananena kwa lugha
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Lazima uwe Mkorintho, Mwefeso au Mgalatia kunielewa! kwi kwi kwi
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280

  Ni utamaduni wa chama chetu kumuachia Rais aliyeko madarakani amalize vipindi vyake vya awamu mbili hata kama uongozi wa nchi umemshinda. Hili ni katika kuweka mbele maslahi ya "chama chetu" na pia kutilia maanani kwamba Kikwete ni mwenzetu na wala "hana" makundi.
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Rais wa kwanza hajauwa Tanzania.
  Rais wa kwanza hajafunga jela wapinzani wake.
  Rais wa kwanza mvumilivu kwa wakosowaji wake.
  Rais wa kwanza kuruhusu uhuru mpana sana wa kutoa maoni.
  Rais wa kwanza kuanza kusafisha wezi serikalini (japo kiuwongo uwongo)
   
 18. C

  Charuka Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hilo la chuo kikuu mnamvimbisha kichwa bure, mpango huo ulianza enzi za BWM
   
 19. C

  Charuka Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Rais wa kwanza BOYS II MEN wake kuchomolewa kwenye ulaji kwa kashfa, na yeye akakubali achomoke
   
 20. C

  Charuka Member

  #20
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  rais wa kwanza bongo kuwa na motorcade ya mabima (BMW)
   
Loading...