usatrumpjr
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 2,237
- 2,900
Ccm wanafikiria kua kila uchaguzi police watakua nyuma yao sasa leo police wamekuta mtu kashachezea vitasa vya usoni
Na huu ndio ukweli chanzo ni hao CCM!CCM ndiyo wakatazwe kuacha ukorofi kwani wao ndiyo chimbuko la fujo, bila CCM kufanya vurugu kusingekuwa na fujo
Na huu mtindo wa kuwanyuka bora uendelee tuu. Hao polisi kwanza wanaingia ukumbini wao wajumbe? Wao wangekaa nje wasubiri kuambiwa njoni na ambulance muchukue mizigo kadhaa ya kijani mkafukie. Ndio njia ya kuheshimiana tuuHawakupigana bali baadhi ya madiwani wa chadema wakiongozwa na yule aliyekuwa kavaa dark kaunda suti waliwapiga madiwani wa ccm. Sheria ichukue mkondo wake ili liwe fundisho kwa madiwani wenye tabia kama hizo. Na kama kuna aliyewatuma kufanya kitendo hicho naye achukuliwe hatua kali kwa mjibu wa sheria.
Kwa hiyo mukiungana ndio mnaingiza majina mawili kwenye kinyang'anyio? Mnajua kabisa baada ya hamahama ya madiwani CCM ina ziada ya idadi, hivi ingetokea assenga kukubalika na baadhi ya wapiga kura, ushindi wa huo muungano ungepatikanaje? Ndio mnajidai vichwani mwenu kuna kitu?Vitu vingine ukikaa kimya ingeweza kuwa vigumu kujua kama kichwani hakuna kitu! Hivi mnashindwa kuelewa kuwa hata madiwani wa CUF na CHADEMA waliungana?
Unafiki wa watanzania unajiliza wee hutaki kusema waI kinachokuliza unajipiga piga tu,pasua nani kapigana na kwa nini ashitakiwe baada ya hiyo miaka 7Ya kutoa lugha Kali na chafu Kwa watumishi yamevumiliwa, haya ya kupigana tusema hapana.
Narudia kusema, wenye akili wameelewa na wapo kimyaKwa hiyo mukiungana ndio mnaingiza majina mawili kwenye kinyang'anyio? Mnajua kabisa baada ya hamahama ya madiwani CCM ina ziada ya idadi, hivi ingetokea assenga kukubalika na baadhi ya wapiga kura, ushindi wa huo muungano ungepatikanaje? Ndio mnajidai vichwani mwenu kuna kitu?
Viongozi wetu ni wahuni, hawana maadili na ni majambazi.Hivi ndivyo ninavyoweza kuwaaeleza viongozi wanaofikia hatua ya kupigana tena ofisini.Kwani kuna nini hasa cha mno mpaka watu mfikie hatua hiyo?Most likely ni kwa sababu ya ulaji na kuchumia matumbo.Ni ukosefu wa nidhamu uliopitiliza.Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ‘wamezichapa kavukavu’ katika uchaguzi wa Naibu Meya Ilala baada ya Chadema kudai kura zao zimechakachuliwa.
Uchaguzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Anatoglou jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 3, ambapo katika uchaguzi huo, Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omar Kumbilamoto (CCM), amefanikiwa kutetea kiti hicho baada ya kushinda kwa kura 27, huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Adam Rajabu, akipata kura 25 na Patrick Assenga (Chadema) akiambulia kura 0.
Vurugu hizo zilianza baada ya madiwani kupiga kura na kwenda kuhesabiwa katika chumba cha kuhesabia kura, mgombea wa Chadema alitoka akipiga kelele kuwa CCM wameanza kuharibu uchaguzi.
Baada ya kusema hivyo maaskari waliokuwapo ukumbini hapo waliingia katika chumba hicho, Assenga alidai askari walimwamuru mgombea wa CUF kurudisha kura alizokuwa amehesabiwa mkononi ambazo zilikuwa 27 katika sanduku la kura na matokeo yake kura hizo akapewa Kumbilamoto.
Wakala wa Kumbilamoto baada ya kuhesabiwa kura hizo alitoka akishangilia ambapo alikutana na Assenga akiwa na madiwani wa Chadema akilalamika kuibiwa kura ambapo madiwani hao waliinuka na kuanza kurushiana ngumi na kutoleana matusi.
Inasemwa kuwa Madiwani wa CCM idadi yao ni 26, wa Upinzaani nao ni 26. Kura zilipopigwa wa CCM akaibuka na kura 27 dhidi ya 26(?) za mpinzani... Kama ni kweli hiyo kura moja imetoka wapi, ila vyanzo vingine vinasema mpinzani kapata 25, basi hapo inaonekana kuwa mmojawao kauza...Ina maana madiwani wa Vyama vya Upinzani hawakuingia kwenye uchaguzi au wameamua wote Kumbimoto apite bila kupingwa, maana hapo ni kama wasingefanya uchaguzi.