Ilala: Madiwani CCM, CHADEMA ‘wazichapa kavukavu’

Ilala: Madiwani CCM, CHADEMA ‘wazichapa kavukavu’

Inasemwa kuwa Madiwani wa CCM idadi yao ni 26, wa Upinzaani nao ni 26. Kura zilipopigwa wa CCM akaibuka na kura 27 dhidi ya 26(?) za mpinzani... Kama ni kweli hiyo kura moja imetoka wapi, labda kama mpinzani kapata 25 basi itakuwa mmojawao kauza...
Mbona kichwa cha habari cha mleta mada kinaonesha 27 kwa 0 !!
 
Inasemwa kuwa Madiwani wa CCM idadi yao ni 26, wa Upinzaani nao ni 26. Kura zilipopigwa wa CCM akaibuka na kura 27 dhidi ya 26(?) za mpinzani... Kama ni kweli hiyo kura moja imetoka wapi, ila vyanzo vingine vinasema mpinzani kapata 25, basi hapo inaonekana kuwa mmojawao kauza...
Acha kudhanidhani....fungua clip umuone msimamizi wa uchaguzi akitangaza matokeo
 
Ina maana madiwani wa Vyama vya Upinzani hawakuingia kwenye uchaguzi au wameamua wote Kumbimoto apite bila kupingwa, maana hapo ni kama wasingefanya uchaguzi.
Kamuulize msimamizi wa uchaguzi.
 
Ametaja matokeo ya mshindi wa kwanza na wa tatu, amemruka wa pili. Lengo lake ionekane wa tatu alipata kura 0, wakati ndio makubaliano yao kwamba jina lake liwepo tu ila apigiwe kura yule wa pili, ili ikitokea fisiemu wameweka kipingamizi kwa huyo wa pili, kusiwepo kupita bila kupingwa
hatujasikia kama kuna wengine waliopigiwa kura zaidi ya hao waliotajwa...usituletee hadithi za kudhani dhani
 
Mimi naongelea kilichotokea jana na hata vyombho vyote vya habari vimetangaza, wala sihitaji kufungua ulichokiweka hapo...
wewe soma hayo magazeti yako sisi tunamsikiliza msimamizi wa matokeo kama alivyotangaza. 27 kwa 0 kama umeonewa nenda mahakani ziko wazi kwa ajili kutatua utata na kutoa haki.
 
Ametaja matokeo ya mshindi wa kwanza na wa tatu, amemruka wa pili. Lengo lake ionekane wa tatu alipata kura 0, wakati ndio makubaliano yao kwamba jina lake liwepo tu ila apigiwe kura yule wa pili, ili ikitokea fisiemu wameweka kipingamizi kwa huyo wa pili, kusiwepo kupita bila kupingwa
 
wewe soma hayo magazeti yako sisi tunamsikiliza msimamizi wa matokeo kama alivyotangaza. 27 kwa 0 kama umeonewa nenda mahakani ziko wazi kwa ajili kutatua utata na kutoa haki.
Acha ubishi wa kitoto wewe! Unajitahidi kubishana ili kuhalalisha unachoshabikia utadhani unalipwa wakati hata vituo vya televisheni vimetangaza tangu jana na watu wote wameona. Hiyo labda Ilala ya Syria...
 
Acha watwangane ili heshima iwepo, maana kuna upande unachukuliwa kama mazezeta
Wapuuzi kweli, wakiwa wenyewe wanapigishana magoti kwenye vikao kama mazezeta, wakikumbana na wapinzani wanajifanya kuvimba kwa vile Polisi wako jirani. Sasa mtindo ni piga tuu
 
Wapuuzi kweli, wakiwa wenyewe wanapigishana magoti kwenye vikao kama mazezeta, wakikumbana na wapinzani wanajifanya kuvimba kwa vile Polisi wako jirani. Sasa mtindo ni piga tuu
Baadae itahamia kitaa ili kujenga heshima
 
Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ‘wamezichapa kavukavu’ katika uchaguzi wa Naibu Meya Ilala baada ya Chadema kudai kura zao zimechakachuliwa.

Uchaguzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Anatoglou jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 3, ambapo katika uchaguzi huo, Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omar Kumbilamoto (CCM), amefanikiwa kutetea kiti hicho baada ya kushinda kwa kura 27, huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Adam Rajabu, akipata kura 25 na Patrick Assenga (Chadema) akiambulia kura 0.

Vurugu hizo zilianza baada ya madiwani kupiga kura na kwenda kuhesabiwa katika chumba cha kuhesabia kura, mgombea wa Chadema alitoka akipiga kelele kuwa CCM wameanza kuharibu uchaguzi.

Baada ya kusema hivyo maaskari waliokuwapo ukumbini hapo waliingia katika chumba hicho, Assenga alidai askari walimwamuru mgombea wa CUF kurudisha kura alizokuwa amehesabiwa mkononi ambazo zilikuwa 27 katika sanduku la kura na matokeo yake kura hizo akapewa Kumbilamoto.

Wakala wa Kumbilamoto baada ya kuhesabiwa kura hizo alitoka akishangilia ambapo alikutana na Assenga akiwa na madiwani wa Chadema akilalamika kuibiwa kura ambapo madiwani hao waliinuka na kuanza kurushiana ngumi na kutoleana matusi.
Kila jambo lina mwisho wake uonevu huu haukubaliki hata kidogo
 
Back
Top Bottom