Ila maisha

dah! kukosa mia leo tu, mbona naona kama afadhalli...

kuna mwingine mwaka wa 4 sasa analala kituo cha daladala ana box lake la kulalia, ambalo saiv limeloa na mvua na hajui atapata wap lingine lini..
Mwenyezi Mungu atafanyie wepesi na atujaalie Moyo wa kutokukata Tamaa...
 
Changamoto ni nyingi kwenye maisha.
Unashangaa kulala njaa mkuu?

Ulishawahi kulamba maziwa ya unga siku nzima. Maisha haya acha tu sitaki kuongea mengi
Ni kwel, hata mm naelewa ugumu wa maisha ndo maana nimemuulza! mara nyingi mtu akileta thread ya hv nawazaga atakua labda ni graduate kapanga hana mazingira mazuri hv 🤔
We unasema maziwa ya unga? Mi na experience ya dhiki kuu nikikusimulia bendera itashushwa nusu mlingoti mtalia sana
 
Njoo piem mkuu, kama unadanganya utajua mwenyewe.
 
Ngoja nami nijaribu....ila mbeya hata usiwe na mia kama unaishi vyema na watu unaweza jikuta wagongewa kutwa nzima kuulizwa why umejifungia ndani....na ukashiba mpaka kesho
Si mbea tu,popote,kikubwa uishi na watu vizuri pale unapoweza. Lakini pia inategemea na unakaa na watu wa aina gani. Midada hata kama ni ile chakavu,wengi wao wakisoma mazingira wakaona hueleweki,watakuibukia. Ila mijama inayosaga majani sasa,itakuona we Babylon tu.
Kikubwa tu na wewe ukijaliwa,usiwe mchoyo,kula na wenzio hasa wale unaojua hawajawasha jiko.
 
Lakini mkuu,kumbuka,japo shida hazina umetokea wapi,nadhani mtoa mada ameongelea wale hasa mipango haiko sawa,ila walikuwa na lamani au wengine ndo hivyo wametelekezwa.
Hao unaowaongelea binafsi siwachukulii hivyo,japo haiondoi kuwa na wao ni viumbe hai. Mtu kazamia tu,kisa aishi mjini. Haendi kwa ndugu,haendi kufanya kazi yoyote,haenda kwa ajiri ya mchongo, ni yeye tu hataki kuishi kijijini(au wanaoishi maisha ya kuiga).
Jiulize kwa nini watu wazima wakifikia umri flani,mjini wamejenga,ila wanahamia vijijini!
Bahati nzuri ni kwamba hata Marekani inayojisifu kwa kuendelea na hawa watu,inao. Ila,shughuli ndogo ndogo tunazodhalau nankuchukulia poa,zinawainua wengi.
Sasa mjini una shida na milioni,kodi tu. Wa kijijini ana shida na laki moja ya ku hukulia mzigo wa biashara. Hawa watu wawili si tofauti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…